Naombeni muongozo jinsi ya kupata mita ya luku.
Nyumba niliyopo ina umeme tayari,lakini tunataka kugawana kila mtu na kuku yake.
Napaswa kuwa na vigezo gani mpaka nipate?
Na itachukua muda gani baada ya kutimiza hivyo vigezo?

Asanteni
 
Tanesco napenda kuwapa hongera sana kwa mwaka huu hakika mmejitahidi sana katika suala la ukataji umeme hovyo...Ila sifa hizi nimpe zaidi Rais wetu, maana kama si yeye inaelekea kulikuwa na watendaji wabovu ambao bila Rais kuwa mkali wasingekuwa na nidhamu kama sasa walivyo..

Hongereni, endeleeni hivyo hivyo, mnatiisha imani kuwa nchi ya viwanda
 
Kuna tatizo limetokea jana waya wenu umekatika hapa kitunda kati ukimaliza shule ya Sekondary na msingi waya unamoto ni hatari kweli kweli
Nimepiga simu jana Tanesco emergency wamesema wanakuja lakini mbaka hivi sasa kimya
Mnasubiri wafe watu ndio mje
Namba yangu ya sim ni 0782 018210
 
Habari za Kazi, Mimi naishi Mbezi-mpigi magoe, ni mda wa miezi mitatu(3) sasa nimelipia umeme Ofisi za Tanesco-Mbezi Mwisho kuunganishiwa(Nguzo Moja) lakini napigwa kalenda tu, sasa nataka kujua hivi mmnanicheleweshea na wakati nimelipa pesa yangu laki 535,000/= kwa nini hamna huruma na pesa za watu nyie Jamaa.
 
Nimewaza kwa haraka kwa nn muwe msoma na si dar kwenye wateja wengi ? Kwa nn malipo kwanza ....mhhh kuna kulizwa hapa
 
Habari..
Sisi wakazi wa mtaa wa MABIRA uliopo wilaya ya kyerwa mkoani Kageara tunasikitika kuwa hatuna huduma ya umeme toka mwezi wa 6 transfoma ilipoharibika... Tangu wakati huo hatuoni dalili zozote licha ya kutoa taarifa kwa wahusika tanesco.. Pia hapa tuna shule ya watoto wenye Mahitaji maalumu hivyo usalama wa hawa watoto na umeme ni muhimu sana.
Tunatanguliza shukrani za dhati kama tutasikilizwa.... Wakazi wa Mabira
 
Mimi mkazi Wa eneo la Mkokozi wilaya ya Mkuranga, kwenye mradi Wa REA, eneo langu liko tayari na nimekamilisha mahitaji yote ikiwemo malipo ya mita.

Wenzetu waliokaguliwa mapema wameishawashiwa Umeme, mm sababu ya SAVEYA, kutoonekana mapema nimelipia wenzagu wakiwa tayari.

Sasa nitegemee kusubiria kwa muda gani? Waziri alifika kuzindua Umeme na kueleza kwa kirefu yasiyomfurahisha ambayo ni kero kisha akatoa siku 10. Tulifurahi lkn naona kama ilikuwa amri ya kisiasa ,tupeni jibu la kitaalam, lini na ss tutatembea kifua mbele.
 
Tanesco huu Uzi mumeanzisha wa nn? Mbona hamjibu malalamiko ya wateja? Kama VP ufuteni
 
MTU kuwa bubu ni ulemavu lakini shirika la umma kushindwa kujibu tuhuma ni kukiri udhaifu na uzembe!
 
Taratibu mmeenda mnakuwa vizuri kwenye huduma zenu.

Tanesco Katavi nawapongeza sana ila kwenye kuunganisha wateja wapya naona kuna kuchelewa chelewa.

Ila kwa huduma zingine mko vzr 24/7 mnafanya kazi
 
Juzi nimebadilishiwa matumizi ya umeme kutoka matumizi ya kawaida kwenda matumizi madogo(Tarrif) nikanunua umeme wa Tsh 9250 nikapata units 75 nikapewa na namba za kuingiza kabla ya kuweka token cha ajabu umeme mpaka leo umegoma. TANESCO what should I do to resolve the problem?
 
Mbona TANESCO kimya sisi tunauliza maswali yetu muhimu humu jukwaani
 
Nataka uliza umeme Kijiji cha Ngongongare kilichopo arusha barabara ya snake farm shika chini upande wa shule ya msingi ni kwamba Rea hampo huko au maana imekuwa story au mnasubiri tuvute kwa nguvu zetu au sisi hatuhutaji umeme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kufahamu shida nini Tanesco Makambako mjini nimelipia umeme toka mwezi wa 5 hadi leo..sababu naambiwa hamna nguzo au hadi mh waziri akija ziarani ndio tutawekewa umeme?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…