TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Habari za muda huu, Nyumbani kwangu kuna tatizo la umeme ambalo linasababishwa na loose juu ya nguzo ikifikia kipindi km hichi cha mvua huwa napata tabu sana ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, mara ya kwanza nilitoa taarifa halikufanyiwa kazi sasa hivi nna siku ya tatu hakuna umeme unapofika katika mita yng, nilipiga simu emergency usiku kucha simu haipokelewi yaani hadi hapo sijaona umuhimu wa emergency calls ila sasa hali imezidi kuwa mbaya mita inarudisha umeme halafu inakata ht mara 10 siku nzima sasa sijui tanesco mnataka nitumie njia ipi sahihi ili niweze kupata huduma na kunusuru hali hii ya umeme kwangu taarifa nimetoa tangu jana baada ya kuona simu hazipokelewi nimeambatanisha na namba waliyonipa ofisini namba zangu za simu ni 0714434257 naishi kigogo mkwajuni View attachment 1243453
TUMEPOKEA TAARIFA KWA HATUA ZAIDI MPENDWA MTEJA WETU
 
Tanesco swali langu ni 1

Tuko wapangaji wa 5 ila tunatumia LUKU 1

Kila mpangaji kafungiwa sub meter vile vidogo vya kusoma unit

Ajabu ni kwamba

Wapangaji tunaweza kuweka umeme wote ina maana kila mpangaji atasoma kile ki meter kuona kama umeme wake umeisha au lah

Lakini kinachotokea kila mpangaji anaweza akawa umeme wake haujaisha lakini LUKU imekata umeme...Huo umeme unapotelea wapi?

TANESCO naomba jibu
@TANESCO naomba gharama za uwekaji hivi vifaa maana navihitaji sana kuepusha migogoro
 
TANESCO naitaji kubadilishwa mita nirudi matumizi ya kawaida mana simalizi hata unit moja kwa siku
 
Ndugu TANESCO,eneo kubwa la mji wa Kibaha halina umeme hivi ninavyoandika,na maeneo mengi ya wilaya hii kama vile Kwa Mathias,Kwa Mbonde, kata yote ya Mwendapole A na B,Kongowe n.k kuna tatizo la kukatikakatika umeme hata mara 8 kwa siku na ni tatizo la muda mrefu sana sasa.Sababu ni nini na mnachukua hatua gani kutatua tatizo?Hebu tulizeni hii mitambo yenu nchi itawalike jamani.
 
Tanesco mkoa wa kilimanjaro moshi mjini barabara ya kcmc kata ya kariwa na longuo tatizo umeme una ongezeka na kupungua na kusababisha usumbufu kwa watumiaji tatizo limeanza wiki ya pili sasa hamna suluhisho kamili.
 
Ni eneo gani haswa? Kuna kazi ilikuwa inaendelea eneo hilo na tulitoa taarifa kwa wateja wa Wilaya ya Kibaha
 
Tanesco mkoa wa kilimanjaro moshi mjini barabara ya kcmc kata ya kariwa na longuo tatizo umeme una ongezeka na kupungua na kusababisha usumbufu kwa watumiaji tatizo limeanza wiki ya pili sasa hamna suluhisho kamili.
TUNAOMBA NAMBA YAKO YA SIMU TAFADHALI
 
Habari za muda huu, Nyumbani kwangu kuna tatizo la umeme ambalo linasababishwa na loose juu ya nguzo ikifikia kipindi km hichi cha mvua huwa napata tabu sana ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, mara ya kwanza nilitoa taarifa halikufanyiwa kazi sasa hivi nna siku ya tatu hakuna umeme unapofika katika mita yng, nilipiga simu emergency usiku kucha simu haipokelewi yaani hadi hapo sijaona umuhimu wa emergency calls ila sasa hali imezidi kuwa mbaya mita inarudisha umeme halafu inakata ht mara 10 siku nzima sasa sijui tanesco mnataka nitumie njia ipi sahihi ili niweze kupata huduma na kunusuru hali hii ya umeme kwangu taarifa nimetoa tangu jana baada ya kuona simu hazipokelewi nimeambatanisha na namba waliyonipa ofisini namba zangu za simu ni 0714434257 naishi kigogo mkwajuni View attachment 1243453
TUMEPOKEA TAARIFA KWA HATUA ZAIDI
 
KERO YA MATENGENEZO YA UMEME.

Ktk Kata ya Rwinga Wilaya yaNamtumbo mkoani ruvuma kumekatika waya katika mtaa wa shule ya msingi Rwinga. Waya huo umekatika wakati watengenezaji wa barabara walipokata mti ambao uliangukia waya na kukatika.

Jana alipigiwa simu mhusika mmoja wa Tanesco Namtumbo majibu yake sio ya kujenga Bali ni kubomoa.
Alsema hawawezi fika hadi wamjue mkataji wa mti ni nani. Alielezwa ni vijana wanaotengeneza barabara ila bado alihitaji jina la mkata mti.
Tagu Jana hadi mda huu msimamo wao upo palepale.

Mm kama mteja na mdau wa umeme hii hali imenisikitisha sana na maswali ninayojiuliza ni mengi hasa weledi wa wasimamizi umeme wilaya.
Mtu mmoja au taasisi moja(barabara) inawezaje kukatisha huduma ya mtaa mzima kwa saizi ya siku mbili?

Naomba muwaambie waje waunganishe kwa faida yao na wananchi.

Ahsante.
 
sheria za tanesco zinasemaje juu ya kuhamisha mita kutoka nyumba A kwenda nyumba B?
 
Jambo TANESCO,,,,,
Maeneo ya katikati ya jiji la DSM limeamka na giza.
naudi wakati gani,?
sababu nini,?
tutegemee utarudi wakati gani,?
Ndugu mpendwa mteja wetu

Ilitokea hitilafu kwenye transfoma letu na wataalamu wetu wamechukua hatuaa stahiki kuhakikisha mnafurahia huduma
 
sheria za tanesco zinasemaje juu ya kuhamisha mita kutoka nyumba A kwenda nyumba B?
Mita haihamishiki ikishafungwa inapaswa kuwa kwenye nyumba hiyo kama kuna nyumba nyingine unashauriwa kuiombea mita mpya na kulipa
 
KERO YA MATENGENEZO YA UMEME.

Ktk Kata ya Rwinga Wilaya yaNamtumbo mkoani ruvuma kumekatika waya katika mtaa wa shule ya msingi Rwinga. Waya huo umekatika wakati watengenezaji wa barabara walipokata mti ambao uliangukia waya na kukatika.

Jana alipigiwa simu mhusika mmoja wa Tanesco Namtumbo majibu yake sio ya kujenga Bali ni kubomoa.
Alsema hawawezi fika hadi wamjue mkataji wa mti ni nani. Alielezwa ni vijana wanaotengeneza barabara ila bado alihitaji jina la mkata mti.
Tagu Jana hadi mda huu msimamo wao upo palepale.

Mm kama mteja na mdau wa umeme hii hali imenisikitisha sana na maswali ninayojiuliza ni mengi hasa weledi wa wasimamizi umeme wilaya.
Mtu mmoja au taasisi moja(barabara) inawezaje kukatisha huduma ya mtaa mzima kwa saizi ya siku mbili?

Naomba muwaambie waje waunganishe kwa faida yao na wananchi.

Ahsante.
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali
 
Mita haihamishiki ikishafungwa inapaswa kuwa kwenye nyumba hiyo kama kuna nyumba nyingine unashauriwa kuiombea mita mpya na kulipa
Kuna mfanyakazi wa Tanesco kahamisha mita kutoka nyumba A kwenda sehem nyingine.mmiliki wa mita alikuwa mpangaji kwenye chumba cha biashara,kashindwa kulipa pango la chumba.alipohama kamuuzia mfanyabiashara mwingine wa nyumba kama yatano hivi. na aliyekuja kuitoa ile mita ni mfanyakazi wenu.na wapangaji wa ile nyumba wengine waligomewa kuhamishwa kwa mita zao hili limekaa vipi?
 
habari,

mita ya TANESCO haihami kinachoweza kusogea au kuhama ni unit tu, hivyo tunaomba taarifa kamili za hilo tukio na wilaya na mkoa mhusika, tutashukuru sana kupata maelezo hayo hapa au kupitia kwenye private meseji ya Jamiiforum au kwa barua pepe yetu customer.service@tanesco.tz
 
Wapendwa TANESCO, mimi nawakumbusha tu kwa nia njema kuhusu suala la umeme wa REA kitongojini kwetu maana tuliambiwa tuzid kusubiria sasa hadi binafsi nachoka, tafadhali sema chochote kuhusu ombi langu la kupatiwa Umeme wa REA huko kwenye kitongoji cha KIJUKA kijiji Mabuye kata Kassambya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
 
kitambulisho cha huyo mfanyakazi wa Tanesco aliye hamisha hiyo mita.hili tatizo limetokea songea mjini. kata ya mjini nyumba ipo karibu na shule ya msingi mfaranyaki.na baazi ya wapangaji walienda kwa kaimu meneja wa tanesco ila kunahali inayoonekana ya kulindana
Tunashukuru kwa taarifa mpendwa mteja wetu tafadhali tunaomba namba yako ya simu
 
Back
Top Bottom