TANESCO naomba kujua kwanini Kubadilishwa Tariff mpk mteja uje ofisii,kwanini luku zisiwe zinajibadlisha zenyewe? hiyo system yenu inashindwaje kugundua huyu mteja yuko chini ya unit 70 kwa mwezi?

Nahitaji kubadilishiwa Tariff sihitaji kuja ofisini kwenu,matumizi yangu n chini ya unit 70 na sasa ni zaidi ya mwaka Tariff haijabadilika,muda wa kufatilia sina ninachoomba toka kwenu ni Kuwekwa tariff ninayostahli.
 
Asante kwa namba,ila hazitusaidii sana.Hao jamaa wakishajua kwamba una grievance outstanding hawapokei simu yako,shida tupu.

Inabidi wajitafakari kabla ya kutembelewa na mtumbuaji kwa sababu bado hawajitambui kuwa hii ni awamu ya tano na jamaa hapendi kabisa watu ambao sio creative ili waende nae sambamba
 
Inabidi wajitafakari kabla ya kutembelewa na mtumbuaji kwa sababu bado hawajitambui kuwa hii ni awamu ya tano na jamaa hapendi kabisa watu ambao sio creative ili waende nae sambamba
TANESCO inahitaji overhaul kwa kukatwa vipande vipande vitatu: production,transmition na distribution &Marketing(REA?) pamoja na kuondoa undesirable elements,ziko nyingi sana,ili kuongeza efficiency.TANESCO it's business as usual,yaani hawajastuka kabisa.Ni mshirika mkuubwa ambao tija yake ni ndogo sana.
 
Mteja anapasqa kuja ofisini kwa kuwa kuwa form ya kujaza ambayo anajizatiti kwa kuijaza kikamilifu.Tambua wapo wateja wanaosafiri kwa muda mrefu unaweza kumbadilisha akirudi anakuta anazidi anapata penalt ndio maana lazima ujaze fomu tukukague

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fomu hi anajaza mwenye nyumba au mpangaji?

maana mwenye nyumba kanipangshia nyumba mimi

luku natumia mwenyewe,hii form anatakiwa akaijaze nani?
 
Tanesco mkoa wa songwe mnatia kinyaa meneja ajiudhuru umeme unakatika katika mpaka baadhi ya vifaa vyangu vya umeme vimeungua kila siku umeme. Unakatika msipo jirwkebisha tutawashitaki kwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli
Maana tushapata connection
 
Mbona hueleweki somo,ndio umeandika nini sasa?
 
Tanesco mkoa wa songwe mnatia kinyaa meneja ajiudhuru umeme unakatika katika mpaka baadhi ya vifaa vyangu vya umeme vimeungua kila siku umeme. Unakatika msipo jirwkebisha tutawashitaki kwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli
Maana tushapata connection
Umeme unakatika katika hovyo kila mahali mkuu,sio huko tu.TANESCO inabidi wajitathmini kwa kweli.
 
Kuna mambo lukuki.
Tusaidieni ufafanuzi. Waziri anasema gharama za nguzo ni suala la Tanesco. Ukienda ofisi za Tanesco wanatubamiza gharama hizo. Hii imekaaje?
Jirani yangu kaomba three phase line kapewa bill ya 3.5ml. Namna hii kweli mnataka wateja au mnawafukuza?
 
Kimara hakuma umeme tangu usiku mpaka sasa.
Hivi nyie watu tuwafanye nini ili mtuelewe?
Mvua haziishi leo wala kesho,ni nature,zipo tangu kuumbwa ulimwengu.
Lazima mjifunze kuishi na nature.Uwezekano wa kuwaka umeme huku mvua zikinyesha upo.Ni hiyo miundombinu yenu mibovu ya kizamani inasababisha huduma zenu hazina mwendelezo.Leo upo,yakipita manyunyu haupo.Huu ni ujima Tanesco badilikeni.Mnatia kinyaa kabisa.
Rais Magufuli ni bora umulike huduma mbovu za hili shirika.Linaturudisha nyuma sana watanzania.Tumelipia huduma zenu,tuna mita za umeme,tuna nguzo na waya nje,tumewekeza mitambo na wateja kibao,halafu wanakaa wanasubiri nyie mjisikie kurudisha huduma.Watu wamekaa ni gunia zao hapa wanasubiri unga wa ugali anao Tanesco!This is absolutely primitive!Mnatia kinyaa.Nchi yote mnalalamikiwa nyinyi,soma huu uzi uone.Hivi nyie ni wazuri kwenye lipi sasa?Tuwasifu kwa lipi?Hili shirika lipo kwa sababu zipi?Kwanini nalipa kodi,nafunga mita,nanunua Luku,for what ikiwa kila mara mnavuruga huduma zenu na hivyo pia mnavuruga biashara zetu,zinakosa continuity.Na hali ngumu hii.Serikali itafakari sana Tanesco.Im tired of this shit company!
 
Ndugu mpendwa mteja wetu tulipata hitilafu na kufanikiwa kuitatua kama bado unapata changamoto tafadhali tusaidie namba ya simu na eneo ulilopo kwa hatua zaidi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba barua ya makadirio aliyopewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boresheni Kitengo Cha Huduma Kwa Wateja Hasa Kwa Wanaotumia Simu kuwasiliana Na nyie.
Mfano. Nilipata shida sana kuwapata h
Kwa wakati. Nilipowapata shida yangu ilikua nikupewa change pin ya mita, hivi kweli group la namba zaidi ya 20 unamsomea mtu kwenye simu? Sawa nikaziandika kujaza zimekosewa, Kupiga tena natakiwa nizitaje tena namba za mita na nilizotajiwa, kweli jamani. Hamuwezi kuzituma kwa text tuu na some tym hiyo huduma si inaweza kumaliza na software za computer tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeme Tabata toka asubui unasumbua sana,umeumnguza mpaka vitu .tumenda pale Tanesco zaidi yamara mbili wanasema wanakuja .lakini mpaka saa MDA huu hatuna umeme nahawajaja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafadhali tuaidie namba yako ya simu na namba ya taarifa kama bado hauna umeme.Unapotoa taarifa ya hitilafu huwa tunaenda kwa wakwanza kutoa taarufa wakanza kufikiwa hivyo tunaomba uvumilivu wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…