TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Boresheni Kitengo Cha Huduma Kwa Wateja Hasa Kwa Wanaotumia Simu kuwasiliana Na nyie.
Mfano. Nilipata shida sana kuwapata h
Kwa wakati. Nilipowapata shida yangu ilikua nikupewa change pin ya mita, hivi kweli group la namba zaidi ya 20 unamsomea mtu kwenye simu? Sawa nikaziandika kujaza zimekosewa, Kupiga tena natakiwa nizitaje tena namba za mita na nilizotajiwa, kweli jamani. Hamuwezi kuzituma kwa text tuu na some tym hiyo huduma si inaweza kumaliza na software za computer tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumebiresha sana mpendwa mteja wetu ndio maana kuna njia mbadala kama hizi ungetaja namba ya mita namba ya simu na tatizi pia huku tungekuhudumia.Tupo kukusiliza na kukuhudumia mpendwa mteja wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada wenu nilikuwa nanunua umeme wa sh.9300 nikawa ninapata unit 75.4 siku nyingine unit 75.3.Tanesco wakanibadilishia tarrif.nilienda nikawaeleza Tanesco -Arusha si kwamba natumia umeme zaidi ya unit 75 bali kosa langu sikuwa na uelewa kwamba hizo point zitaniletea shida.naomba msaada wenu.mwezi dec nimenunua unit 26.mwezi huu January nimenunua unit 14.
 
Tanescko arusha ni watu wa ajabu sana waya wa umeme umekatika leo ni cku ya nne nymba zaudi yaw 50 hazina umeme sasa ,,,,sasa hawaonai wanapata hasara kwa watu kukosa umeme na ni kazi ndogo sana ni kuunganisha tu waya ulio katika nafikiri meneja wa tanesco arusha hafai kukaa ofsn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO kilosa last week mlitusumbua sana mnakata umeme hata taarifa hamtoi,mlitutia hasara wafanya biashara haswa wa chakula especially mimi nilipata hasara ya nyama kuharibika
20200123_131730.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mpendwa mteja wetu tulipata hitilafu na kufanikiwa kuitatua kama bado unapata changamoto tafadhali tusaidie namba ya simu na eneo ulilopo kwa hatua zaidi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya bwana TANESCO mimi nawe tutafikishana taratibu.Hayo mazungumzo yetu hapo juu ilikuwa jnne,ukasema ni hitilafu na mmeitatua.
Leo jmosi Kimara hakuna umeme asubuhi hii.Nayo utasema ni nini?It doesnt matter sababu unazotoa,nnachojaribu kukueleza ni hii hali ya kutokuwepo mwendelezo wa huduma yenu.Ni kitu kinatuathiri sana tunaotumia umeme hasa kwa matumizi ya kibiashara.Tunatumia umeme mwingi,ndio tunaolipa faida shirika lenu,lakini hamtuthamini,hamtoi huduma zenu moja kwa moja.Leo jmosi,ndio biashar nyingi zina peak weekend,mmekata umeme.Wewe utatoa sababu hapa,lakini tutaendelea kupeana sababu miaka na miaka na mie unaniumiza tu.Kwanini umeme ukatike hivi?Tanesco inakuwa na maana gani kwetu watanzania?
 
Sasa ni saa kumi jioni.Bado umeme haujarudi kuanzia Ubungo hadi Kimara Mwisho tangu asubuhi.Na mvua inanyesha.Mnasikitisha sana Tanesco.
 
Tanesco tabata mnataka kutuunguzia vitu maana mnakata na kurudisha umeme tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Boresheni Kitengo Cha Huduma Kwa Wateja Hasa Kwa Wanaotumia Simu kuwasiliana Na nyie.
Mfano. Nilipata shida sana kuwapata h
Kwa wakati. Nilipowapata shida yangu ilikua nikupewa change pin ya mita, hivi kweli group la namba zaidi ya 20 unamsomea mtu kwenye simu? Sawa nikaziandika kujaza zimekosewa, Kupiga tena natakiwa nizitaje tena namba za mita na nilizotajiwa, kweli jamani. Hamuwezi kuzituma kwa text tuu na some tym hiyo huduma si inaweza kumaliza na software za computer tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kama mteja unaweza kupendwa kusomewa uandike au kutumiwa hakuna kizuizi katika hilo.Tunashukuru kwa taarifa yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO itapendeza sana mkiwa mnajibu au kutoa ushauri.nadhani ndio lengo la hii thread. Isiwe mnajibu baadhi tu za hoja za wateja.
 
Chain ya malalamiko inakwendaje wakuu kama naona wilayani sitendewi haki maana fomu yangu ya REA imeandikwa nisubiri nguzo za mradi wakati wengine wanawekewa tu nami nahitaji nguzo mbili tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada namba ya emergency tanesco tabata segerea


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
TANESCO naomba namba ya Mkurugenzi wa Tanesco au Waziri Kalimani, tumechoka na huduma zenu mbovu! Haiwezekani siku 4 tabata liwiti hamna umeme! Ripoti zimetolewa mara kibao lakin mafundi wanakuja kugesha vitu vyao baada ya masaa mawili umeme umekata! Sasa naomba namba za viongozi wenu tulireport ili swala.
 
TANESCO naomba namba ya Mkurugenzi wa Tanesco au Waziri Kalimani, tumechoka na huduma zenu mbovu! Haiwezekani siku 4 tabata liwiti hamna umeme! Ripoti zimetolewa mara kibao lakin mafundi wanakuja kugesha vitu vyao baada ya masaa mawili umeme umekata! Sasa naomba namba za viongozi wenu tulireport ili swala.
Je ni eneo kubwa au wewe mwenyewe? Tafadhali tusaidie namba yako ya simu na eneo ulilopo kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaman VP mifumo yenu ya LUKU kwa njia ya simu inashida gan nimenunua umeme kwa njia ya AIRTEL naambiwa Huduma hakuna nimejaribu VODACOM jibu n hillo hilo naomba toeni ufafanuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco Embu Shughulikieni Suala La Umeme Tangu Kumekucha Leo Tandika Hakuna Umeme Yani Shughuli Zimekwama Sana Ni Giza Totoro
 
Tangazo lenu mlisema umeme utarudi saa kumi na moja jioni baada ya kuzimika leo asubuhi..

Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi saa mbili na nusu bado umeme haujawaka.

Muwe mnatoa taarifa sahihi ili watu tujipange kukabiliana na giza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom