TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
inachukua mda gani kutumiwa sms ya kulipia baada ya sarveyor kusavei nina wiki mbili toka aje na aliniomba nauli nikanmyima, kimya had sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco...Kuna hitilafu eneo la Mjohoroni Shia- Moshi. imeripotiwa tangu tarehe 4. walifika wakakata waya. hawajaonekana tena japo gari la dharura linapita eneo hilo kila siku..
ripoti 0743.
 
Tatizo: mtaa wa Bomambuzi Moshi, umeme tangu jana hakuna, waya ulipiga shoti kwenye nguzo ikaripotiwa...hajafika fundi tangu jana 7.2.2020 na gari zinapita kila muda hapo substation Bomambuzi.
 
Imekua Kama kawaida vile kwa wakaazi wa kigamboni umeme kukataika hovyo hovyo, Yani bila hata taarifaa rasmi.

Mbaya zaidi, umeme umekua ukikatwa katwa Mara nyingi kwa interval ya sekunde 30-50, na Mara nyingi mida ya jion.

Sasa sisi wananchi wa kigamboni tunajiuliza je Tanesco mna nja gani na vyombo vyetu vya umeme? Mnataka kuviunguza au?

JIREKEBISHENI ASEE AU HADI MZEE BABA AJE ASEME?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO iringa mnazingua sana tangu jumapili hatuna umeme tunafatilia apo ofisin kwenu tunaambiwa tu mnakuja hivi punde.Jitafakarin then chukueni hatua
 
Nikiwa kama mteja siku moja jumatatu kama sikosei, nikiwa nasubiri huduma sikupendezwa na matusi yaliyo kuwa Yana mtoka staff mmoja was kiume kwenda kwa mdada mmoja.

Tena matusi na kumdhalilisha kuhusu elimu yake kwa kweli ni kitendo cha hovyo kufanyika katika ofisi ya uma tena mbele za wateja.

Staff Kisarawe mjirekebishe na kufuata maadili ya kazi zenu.
 
Nataka kununua umeme. Nilifungiwa meter wiki tatu zilizo pita na zile unit 10 nilizopewa zinaelekea ukingoni. Nimekwenda kununua umeme naambiwa mita haijasajiliwa. Nimekwenda ofisi za Tanesco wananiambia nisubili wiki mbili mbele. Naomba kuuliza. Je kusajili mita nalo limekuwa tatizo mpaka linachukua mwezi mzima na masiku, Tanesco mnakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO naomba namba ya Mkurugenzi wa Tanesco au Waziri Kalimani, tumechoka na huduma zenu mbovu! Haiwezekani siku 4 tabata liwiti hamna umeme! Ripoti zimetolewa mara kibao lakin mafundi wanakuja kugesha vitu vyao baada ya masaa mawili umeme umekata! Sasa naomba namba za viongozi wenu tulireport ili swala.
Mh Kalema na Mh Subira Mgalu namba zao zipo ila hawapokei sim kwa urahisi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO hapa penye hyo shida kuna transfomer, sasa nahisi limezidiwa sasa kuna lain 2 hapa huwa zinasumbua sana, lain yetu hii moja wapo maana nyumba ya mbele yetu ina umeme ila kuna nyumba kama 30 ndo zinakosaga umeme, ni kitu kinachojirudia rudia sana tena sana! Wakija wanaegesha baada ya masaa 2-3 unakatika au wakiegesha vizur week mnakaa bila shida lakini ukipita pale kwenye transfomer unaona kabisa fuse moja inaiva kwa moto kuwa nyekundu sana na hapa naandika hii comment saa hii hatuna umeme tayari apa kuja hawa jamaa kuegesha labda kesho.
Sasahv unaupika kama kimulimuli huku majumbani within the second unawaka na kukata fasta.
 
TANESCO Nomba mnifahamishe kwa undani. Katika vijiji vingi sasa hivi kuna mradi wa REA, sasa naomba kujua, kwa sehemu ambayo inahitaji nguzo mbili kwa mfano, Ni gharama kiasi gani mteja anatakiwa kulipa ili aunganishiwe umeme?

Pia nomba kufahamu, Mita za umeme huwa mnaziuza au mnatoa bure? Kama mnauza ni shilingi ngapi moja? na kuhusu waya za umeme, mteja analipia? kama jibu ni ndiyo, ni shilingi ngapi?

Na je kuhusu Survey, ni shilingi ngapi mteja anatakiwa kulipa?

TANESCO TANESCO TANESCO , Nimewaita mara tatu maana nanusa harufu ya wizi, Naombeni ufafanuzi mapema tafadhalini sana.
Walasam
Kidudu
 
Tanesco mnachokifanya huku chanika ni uhujumu uchumi, wakati hapa kidugalo hatuna umeme sababu nguzo hazijafika, nyie mmekuja kumwaga nguzo hapa mbele kidogo ya Masai wawili na mnaziacha zioee hapa tena zipo kwenye maji.

Basi njooni mzichukue mkawape wengine kuliko kuozea hapa.
IMG_20200214_163536.jpeg
IMG_20200214_163516.jpeg
IMG_20200214_163504.jpeg
IMG_20200214_164144.jpeg
IMG_20200214_164117.jpeg
IMG_20200214_163540.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
*TAARIFA KWA UMMA:*

*FEBRUARI 15, 2020*

*TAARIFA YA TAHADHARI KWA WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA MKONDO WA MAJI YATOKAYO KWENYE VYANZO VYA KUFUA UMEME KWA MAJI VYA MTERA NA KIDATU*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa taarifa kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bwawa la Mtera limejaa kwa kiwango cha juu na kina cha maji kimepanda hadi kufikia mita 698.50 juu ya usawa wa bahari na hivyo kulazimu ziada inayoendelea kuingia kuanza kutolewa kupitia milango mahususi kuanzia leo Februari 15, 2020 kwa ajili ya usalama wa Mabwawa na Mitambo.

Aidha, wastani wa mita za ujazo 1,200 kwa sekunde kinaendelea kutiririka bwawani.

TANESCO inaendelea kutoa tahadhari
kwa Wananchi hususani wale wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile Uvuvi, kulisha Mifugo, Kilimo na shughuli nyingine kwenye mkondo wa mto, vidimbwi au pembezoni mwa bwawa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu, kijamii na kiuchumi kwa kipindi hiki ambacho mvua za Vuli zikiwa zinaendelea kunyesha.

TANESCO itaendelea kutoa taarifa kadri hali ya kuruhusu ziada ya maji kupita upande wa pili itakavyokuwa inaendelea.

Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu
 
Shirika litangaze rasmi kama Temeke kwa sasa kuna mgao wa umeme, maana ishakuwa kero, nchi imejaa gesi hadi mabomba yanapasuka, kule bwawa la maji limejaa hadi raia wamepewa tahadhari wahame linaweza kupasuka, shirika lina kila kitu

Temeke imejaa viwanda na biashara muhim kama mgao umeingia tangazeni, na Waziri wa Nishati kama upo hapa fuatilia, Inaweza pita siku nzima hamna umeme, umeme kila siku wanakata hovyo hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom