TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO umeme unakatika sana kwa siku zaidi ya mara tatu Kimara mwisho line ya Mavurunza.
Vitu vyetu vinaharibika sababu ya huku kukatikakatika.Siku mbili hizi jana na leo hali imekuwa serious sana.
Tatizo nini?
Narudia tena,ni Kimara mwisho line ya Mavurunza kuanzia Ubungo mpaka Kimara Matangini umeme unasumbua kwa kukatika hovyo mara nyingi kwa siku.
 
Umeme umerudi sasa hivi umeniunguzia motor.Ni heri mkate kabisa tujue hatuna umeme mpaka matatizo yenu yakiisha muuwashe kuliko huu ubabaishaji wa kukata na kurudisha kila baada ya dk 20,mnatutia hasara.Sasa hii motor yangu nije wapi niwadai hela ya mpya?​
 
Naomba mawazo yenu kwa tatizo hili: natumia unit 8 kutwa.

Nina frigdge moja ndogo, taa energy saver kama 5 zinawaka saa 12 a day, tv mbili zinatumika kama saa 5 a day, . Nadhani unit 8 a day huu ni umeme mwingi ninao tumia.

Tatizo linaweza likawa wapi? Nimeleta fundi akacheki wiring akasema iko vizuri.

Ushauri tafadhali.

Asante
Taa za Energy Saver Ni za Watt? 2.Friji ndogo Ni Watt ngapi na hiyo TV Ni Watt ngapi ili tucheki kimahesabu Kama hizo Unit hazifiki.
 
TANESCO umeme unakatika sana kwa siku zaidi ya mara tatu Kimara mwisho line ya Mavurunza.
Vitu vyetu vinaharibika sababu ya huku kukatikakatika.Siku mbili hizi jana na leo hali imekuwa serious sana.
Tatizo nini?
Narudia tena,ni Kimara mwisho line ya Mavurunza kuanzia Ubungo mpaka Kimara Matangini umeme unasumbua kwa kukatika hovyo mara nyingi kwa siku.
Eneo gani haswa Kimara na namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaratibu ni upi ? Nimemtuma kijana wangu ofisi za Tanesco Mkuranga akiwa na picha / kopi ya kitambulisho changu.

Kanyimwa fomu eti mpaka mm niwepo
 
Leo, nimemtuma kijana WANGU baada ya kukamilisha mahitaji ya passport size na kopi ya kitambulisho changu aende ofisi za Tanesco Mkuranga ili aniletee Fomu wamemkatalia.

Hii iko sawasawa
 
Back
Top Bottom