Kwani Bei halali ya kuwekewa umeme usio wa REA ni shilingi ngapi? TANESCO Maana ukienda unaambiwa bei tofauti tofauti
 
TANESCO Pia kuna kijiji kinaitwa IGUNDU kiko wilayani Chunya kata ya Sangambi. Nguzo zimesimikwa na waya zimewekwa mpaka kijijini, lakini hakuna kinachoendelea yapata mwaka sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
#Say no to lockdown.
#Say no vaccine test for COVID-19 To fellow Africans
 
Habari huku Urambo Kijiji Cha Kasela D kata ya uyogo umeme wa REA umekomea Shuleni tu na mitaaa michache lakini mitaa mingine hawajasimika nguzo na tunahitaji kwa ajili ya matumizi na mashine za kusaga na kukoboa.
Sijui Kijiji kizima kitawekewa lini?naamini Kama TANESCO wangekuwa serious na biashara wateja ni wengi lakini hawataki kuwafikia 0623644349
 
Kwahili, mjomba Wala usisite, wapatie no za simu dukuduku lote litakwisha.

Binafsi nimepata ufumbuzi mwingi kupitia jamii Forum- Tanesco. Hivi Sasa Sina shaka kabisa na utendaji wao ukurasa huu uko Makini.

Bravo Tanesco.
Wewe mtumishi wa TANESCO sahivi tunamsubiri kwa hamu mzee wetu tumwambie nyie endeleeni kusubiri namba ya simu

Sent using COVID-19
 
Sasa TANESCO hapa nimeshataja maeneo mlio ruka, ni Pachoto A na Pachoto B kata ya Naliendele mkoani Mtwara. Meneja wenu anajua hili kuwa ameruka nyumba za maskini 400+ na kwenda kwa vigogo eneo la Sogea.

Sasa wananchi watamwomba Mh ili waletewe umeme hata kwa 300,000 nyie endeleeni kusubiri namba ya simu.

Sent using COVID-19
 
Wewe mtumishi wa TANESCO sahivi tunamsubiri kwa hamu mzee wetu tumwambie nyie endeleeni kusubiri namba ya simu

Sent using COVID-19
Hapana , jomba mm sifanyi kazi Tanesco na Wala sikuzuii kusonga mbele.
Ila mm jamii forum - Tanesco imenifumbulia utata wote niliowahi kukutana nao.

Mara ya Mwisho March 2020 walinizingua upatikanaji wa control number ofisi za Mkuranga kupitia humu nikapata ufumbuzi.

Niko ndani ya kipindi cha siku 60 kusubiria huduma yao , nilifanya malipo 27/03/2020 nasubiri mpaka 27/05/2020 Kama bado ntafika ofisi zao kwa kupata taarifa nn tatizo.

Nikiona moja haikai, mbili haikai mkombozi wangu ni JAMII FORUM- TANESCO.

Hivyo sisiti kutoa pongezi na lawama inapobidi hata Kama utaniona mm ni mwajiriwa Tanesco.
 
Nashukuru, kwa kunitoa utumishi wa TANESCO .
 
Isitoshe vile vi limoti vyao vya mita vinasumbua kinoma especially umeme unapokuwa umeisha kabisa, pia suala la umeme kwa waliopanga ni pasua kichwa mno, ingefaa TANESCO warahisishe gharama ya kununua mita, ikiwezekana kila chumba kiwe na mita yake.
 
Reactions: rr4

Tanesco, yanayofanywa na ofisi zenu huku chini yanajionyesha pia hata kwenu kwenye huu Uzi.

Nimewasilisha maelezo yangu tangu jumamosi lakini hakuna majibu yaliyotolewa hadi muda huu.
Pia, suala LA kudai namba za simu wakati mwingine ni kufanya kazi kwa mazoea au kuna vitu. Vingine mnatafuta? Haiingi akilini kwa maelezo kama haya niliyotoa nayo udai namba za simu wakati kila kitu kinajieleza
 
Umeme bado unakatikakatika tu hadi leo ndio tuseme kiuno kimekuwa na uzoefu au maji yamekauka kwa mto? Tunaomba substation Manyoni maana mbunge wetu hata halioni hilo pamoja na viongozi wake.
Manyoni vijana wengi hatuna ajira kutokana na kuwa hakuna sehemu za utalii, madini yapo lkn ni hifadhi ya taifa na hatujui kwanini wasifanye tu ikawa sehemu ya utalii au ikawa ni mgodi na pia hakuna viwanda na viwanda vinahitaji umeme wa uhakika, ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…