TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kwani Bei halali ya kuwekewa umeme usio wa REA ni shilingi ngapi? TANESCO Maana ukienda unaambiwa bei tofauti tofauti
 
TANESCO Pia kuna kijiji kinaitwa IGUNDU kiko wilayani Chunya kata ya Sangambi. Nguzo zimesimikwa na waya zimewekwa mpaka kijijini, lakini hakuna kinachoendelea yapata mwaka sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
#Say no to lockdown.
#Say no vaccine test for COVID-19 To fellow Africans
 
TANESCO walipewa maelekezo ya kutoruka makazi ya watu pindi wanaposambaza umeme.

Katika eneo la Naliendele mkoani Mtwara umeme uko ktk mitaa ya Pwani, Mnali halafu wakaruka nyumba 400+ zilizopo pachoto A na Pachoto B wakaenda kuweka Sogea.

Wananchi wa Pachoto A na Pachoto B wanaamini kuwa walirukwa makusudi na wanasema nyumba za Sogea zinamilikiwa na vigogo wa taasisi mbalimbali ndomaana mradi wa REA wa Pachoto A na Pachoto B ukakimbizwa kule.

Wanatamani siku Mh Rais atakapokuja wamwombe awasaidie umeme kwa gharama yoyote hata kamasi wa REA

Wanaamini watendaji wa TANESCO Mtwara wana laana.

TANESCO Tanzania kazi kwenu. Meneja wenu alimuuziaga transformer mwekezaji Mh Rais akaingilia, leo mnafanya tena uhuni ngoja aje tena maana hamwezi bila kusukumwa.

Mh Rais karibu sana Mtwara baada ya likizo, karibu ili umkague mkandarasi wa barabara ya Mtwara-Newala, karibu ushangae maajabu ya TANESCO

Sent using COVID-19
Habari huku Urambo Kijiji Cha Kasela D kata ya uyogo umeme wa REA umekomea Shuleni tu na mitaaa michache lakini mitaa mingine hawajasimika nguzo na tunahitaji kwa ajili ya matumizi na mashine za kusaga na kukoboa.
Sijui Kijiji kizima kitawekewa lini?naamini Kama TANESCO wangekuwa serious na biashara wateja ni wengi lakini hawataki kuwafikia 0623644349
 
Kwahili, mjomba Wala usisite, wapatie no za simu dukuduku lote litakwisha.

Binafsi nimepata ufumbuzi mwingi kupitia jamii Forum- Tanesco. Hivi Sasa Sina shaka kabisa na utendaji wao ukurasa huu uko Makini.

Bravo Tanesco.
Wewe mtumishi wa TANESCO sahivi tunamsubiri kwa hamu mzee wetu tumwambie nyie endeleeni kusubiri namba ya simu

Sent using COVID-19
 
TANESCO walipewa maelekezo ya kutoruka makazi ya watu pindi wanaposambaza umeme.

Katika eneo la Naliendele mkoani Mtwara umeme uko ktk mitaa ya Pwani, Mnali halafu wakaruka nyumba 400+ zilizopo pachoto A na Pachoto B wakaenda kuweka Sogea.

Wananchi wa Pachoto A na Pachoto B wanaamini kuwa walirukwa makusudi na wanasema nyumba za Sogea zinamilikiwa na vigogo wa taasisi mbalimbali ndomaana mradi wa REA wa Pachoto A na Pachoto B ukakimbizwa kule.

Wanatamani siku Mh Rais atakapokuja wamwombe awasaidie umeme kwa gharama yoyote hata kamasi wa REA

Wanaamini watendaji wa TANESCO Mtwara wana laana.

TANESCO Tanzania kazi kwenu. Meneja wenu alimuuziaga transformer mwekezaji Mh Rais akaingilia, leo mnafanya tena uhuni ngoja aje tena maana hamwezi bila kusukumwa.

Mh Rais karibu sana Mtwara baada ya likizo, karibu ili umkague mkandarasi wa barabara ya Mtwara-Newala, karibu ushangae maajabu ya TANESCO

Sent using COVID-19
Sasa TANESCO hapa nimeshataja maeneo mlio ruka, ni Pachoto A na Pachoto B kata ya Naliendele mkoani Mtwara. Meneja wenu anajua hili kuwa ameruka nyumba za maskini 400+ na kwenda kwa vigogo eneo la Sogea.

Sasa wananchi watamwomba Mh ili waletewe umeme hata kwa 300,000 nyie endeleeni kusubiri namba ya simu.

Sent using COVID-19
 
Wewe mtumishi wa TANESCO sahivi tunamsubiri kwa hamu mzee wetu tumwambie nyie endeleeni kusubiri namba ya simu

Sent using COVID-19
Hapana , jomba mm sifanyi kazi Tanesco na Wala sikuzuii kusonga mbele.
Ila mm jamii forum - Tanesco imenifumbulia utata wote niliowahi kukutana nao.

Mara ya Mwisho March 2020 walinizingua upatikanaji wa control number ofisi za Mkuranga kupitia humu nikapata ufumbuzi.

Niko ndani ya kipindi cha siku 60 kusubiria huduma yao , nilifanya malipo 27/03/2020 nasubiri mpaka 27/05/2020 Kama bado ntafika ofisi zao kwa kupata taarifa nn tatizo.

Nikiona moja haikai, mbili haikai mkombozi wangu ni JAMII FORUM- TANESCO.

Hivyo sisiti kutoa pongezi na lawama inapobidi hata Kama utaniona mm ni mwajiriwa Tanesco.
 
Jamani TANESCO naomba msaada hiyo remote imeandika sleep tu nafanyaje hapo nataka kuweka umeme nashindwa
IMG_20200405_201722.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa case niliyoripoti nadhani haina haja ya namba. Kuna kipindi tuliripoti kuwa meneja wa TANESCO Mtwara kauza transformer kwa mwekezaji, badala ya ku solve wakaomba namba ya simu.

Mh Rais alivyokuja akaingilia kati na mwekezaji akalipwa fedha na TANESCO. Sasa nawaambia ujinga walioufanya kwa kuruka nyumba 400+ pia wanaomba namba za simu, sasa waendelee kusubiri namba ya simu wasichukue hatua yoyote tuone

Sent using COVID-19
Nashukuru, kwa kunitoa utumishi wa TANESCO .
 
Hivi tanesco mnashindwa nn suala la LUKU kufanya km vocha kwamba ukishanunua unaingiza tu kwenye simu moja kwa moja. Nyie ukinunua luku uende tena ukaingize kwenye limita lenu, kwanini isiwe ukinunua inaingia yenywe automatically wakati namba ni ile ile?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Isitoshe vile vi limoti vyao vya mita vinasumbua kinoma especially umeme unapokuwa umeisha kabisa, pia suala la umeme kwa waliopanga ni pasua kichwa mno, ingefaa TANESCO warahisishe gharama ya kununua mita, ikiwezekana kila chumba kiwe na mita yake.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Habari.
Miaka miwili iliyopita,waziri wa nishati, medard kalemani, alifanya ziara eneo LA bulale kata ya buhongwa jijinj mwanza, ikiwa ni maagizo ya waziri mkuu wakati akifungua zahanati ya bulalebaada ya wananchi kulalamika kuhusu ukosefu wa umeme katika eneo hili.
Katika ziara hiyo waziri aliagiza umeme uwake ndani ya wiki moja na katika kurahisisha zoezi hilo, Tanesco wafungue ofisi ya muda bulale ili wansnchi wapate huduma karibu.
Miaka zaidi ya miwili baadaye, wakazi wengi wamefanya "wiring" na kujaza fomu( mimj mmoja wao) nguzo zimewekwa transfoma imefungwa lakini umujitokeza ubaguzi kuwaunganisha wateja wapya.
Niko jirani na shule ya msingi Lumeke,eneo LA tarazo, nimeshuhudia jumanne ya wiki hii nyumba mbili zikifungwa umeme huku sisi tulio jirani na nyumba hizo tukibaki midomo wazi!
Iweje nyumba hizo, tena zilizojengwa nyuma yetu zipewe huduma hiyo ilihali, tuliojaza fomu na kuziwasilisha tanesco nyamagana, tumebaguliwa?
Vigezo gani vimetumika kuziunganisha nyumba hizo na huduma ya umeme na kutuacha wengine tena kwa kuruka nyumba nyingine?
Tunakusudia kuchukua hatua zaidi ikiwa hadi kufikia wiki ijayo, tutakuwa hatujapata maelezo sahihi ya kwanini baadhj yetu tumerukwa kupata huduma hii ilihali wengine katika eneo LA ndani ya mita 10, 20, 30 na ambako tayari kuna nguzo kwa zaidi ya miezi sita sasa hatupati huduma hizo.

Tanesco, yanayofanywa na ofisi zenu huku chini yanajionyesha pia hata kwenu kwenye huu Uzi.

Nimewasilisha maelezo yangu tangu jumamosi lakini hakuna majibu yaliyotolewa hadi muda huu.
Pia, suala LA kudai namba za simu wakati mwingine ni kufanya kazi kwa mazoea au kuna vitu. Vingine mnatafuta? Haiingi akilini kwa maelezo kama haya niliyotoa nayo udai namba za simu wakati kila kitu kinajieleza
 
Umeme bado unakatikakatika tu hadi leo ndio tuseme kiuno kimekuwa na uzoefu au maji yamekauka kwa mto? Tunaomba substation Manyoni maana mbunge wetu hata halioni hilo pamoja na viongozi wake.
Manyoni vijana wengi hatuna ajira kutokana na kuwa hakuna sehemu za utalii, madini yapo lkn ni hifadhi ya taifa na hatujui kwanini wasifanye tu ikawa sehemu ya utalii au ikawa ni mgodi na pia hakuna viwanda na viwanda vinahitaji umeme wa uhakika, ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom