TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nina uchungu nimejaza form muda mrefu hiyo survey imechukua wiki 2 kupewa namba ya kulipia Sasa mwezi mzima taarifa zangu zipo kituo Cha tazara yombo ilala nijulishwe Kama Kuna shida Basi mtu tunajitahidi kuitafuta hiyo hela nyie mmatukwamisha naomba hiyo huduma Kama sistahili nijulishwe 0754228453

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa taarifa tunaifanyia kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Tanesco! Mimi nakaa Sakina Kwa Idd tumekuwa na tatizo la umeme kwa miaka zaidi ya miaka 17. Tatizo ni hilo hilo kila wakati transformer ya kama unaenda shule ya Trust ukipitia njia hii ya Kilimanjaro School ninavyo andika hivi hakuna umeme sasa najiuliza hakuna mafundi kwanini hakuna suluhisho la tatizo hili miaka yote hiyo. Hebu tatueni hili tatizo once and for all.


Sent using Jamii Forums mobile app
Tafadhali onyesha
Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua utaratibu wa kuomba kuunganishwa na umeme kwa yale maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji na kuna umeme uliopita karibu ambao ni mradi wa REA ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Peramiho - Songea DC, nimepeleka maombi ya kuunganishiwa umeme kama mteja mpya tangu tar 23/12/2019 kwa mpango wa REA lakini hadi leo hakuna Surveyor aliyefika. Na nyumba yangu ipo jirani tu na nguzo si zaidi ya Mita 30. Nimefuatilia mwezi February nikaambiwa niandike barua ya kuwakumbusha lakini bado hamajafika. Sasa nimechoka kusubiria kwa muda wote huu. Natafuta mawasiliano ya Waziri mwenye dhamana nimuwasilishie hili suala maana documents za ushahidi ninazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali onyesha
Eneo - Sakina kwa Iddi

Wilaya - Arumeru

Simu - 0621 282103

Tatizo - Kukatika kwa umeme mara kwa mara hata jana tumelala giza. Nitatizo gani hili lisilo isha kwa miaka hamjui kitu manachofanya au haiwezekani for 17 years tatizo ni hilo hilo.
 
Nipo Peramiho - Songea DC, nimepeleka maombi ya kuunganishiwa umeme kama mteja mpya tangu tar 23/12/2019 kwa mpango wa REA lakini hadi leo hakuna Surveyor aliyefika. Na nyumba yangu ipo jirani tu na nguzo si zaidi ya Mita 30. Nimefuatilia mwezi February nikaambiwa niandike barua ya kuwakumbusha lakini bado hamajafika. Sasa nimechoka kusubiria kwa muda wote huu. Natafuta mawasiliano ya Waziri mwenye dhamana nimuwasilishie hili suala maana documents za ushahidi ninazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Je umefanya kwa jina gani? Namba ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku ikifika saa tisa usiku mnakata hovyo umeme mtatuunguzia vifaa vyetu! Pili hizi luku zenu mpya zinakula sana umeme, umeshaona wapi mtu anatumia umeme wa elfu 10 kila baada ya siku 2???? Mi nataka mnirudishie luku system ya zamani huu ni wizi.
 
kuna umeme wa rea maeneo ya viwege kata majohe wilaya ilala Dar es salaam ila huduma imesimama eneo moja na wengine tunaotakakuwekewa ni ziadi ya miezi sita hakuna kinachoendelea licha ya kufuatilia tatizo limekuwa ni nguzo tufanyeje?

Bora nyie miezi sita [emoji16]sisi huku tuna miaka miwili tunasubiri jana ndo wameanza kufunga waya
 
Eneo Masaki kidugalo, wilaya Kisarawe, tatizo mita imeungua, huyo bibi anafatilia tangu january, march niliandika hapa wakaenda siku ya pili yake wakasema mita imeungua watarudi baada ya cku moja ndo hawajarud tena, kila wakifatwa wanadai wataenda na hawatokei
 
Habari ndugu zangu Tanesco, baada ya kuwatafuta na mkanipa response ,nikapigiwa na Tanesco Kisarawe wakasema vifaa hamna ila mwezi huu hauishi watakuwa wameshakuja, na akahidi kunipiga ndani ya siku 3 kunipa updates, lakini kimya mpaka leo na naona mwezi unaelekea ukingoni..


0743157095
HANSI J. MALEKANI
CHANIKA MWISHO..
 
Toka jana umeme haujatulia unakata unatudi unakata unarudi mda mwingine hata within seconds, hii ni hatari kwa vifaa vyetu vya umeme na tukipata hasara hamtulipi. So Kama umeme ni mdogo zimeni tu line kadhaa kwa wakati ili tusipate hasara, chondechonde wahandisi wetu wa umeme TUNAWAOMBA SANA MZINGATIE HILI!!!
 
Hili ni tatizo la taifa mkuu!
Kila kona hali ni hiyo!
Au ukute meneja wa tanesco eneo husika katongoza bibie wa mitaa yenu kakataliwa, hapo mtakoma.
 
Back
Top Bottom