Siyo leo tu naiona hii tabia ya Tanesco kukata kata umeme na ndani ya dakika moja Wanakuwa wamerudisha,
Kwa siku wanaweza fanya hivyo zaidi ya mara tano na sijui nini tatizo?

Leo tena naona hali hii imeanza hapa Dodoma ni mara ya pili sasa mnakata umeme na kurudisha,

TANESCO kumbukeni tuna mavitu yetu ya gharama kama mafriji, marice kuka makubwa makubwa kama ya Hashimu Rungwe tunapikia ubwabwa. Tunamacomputer, maprinter na Nk. Yanatumia huo umeme mnaokata kata kila dakika na kurudisha kama watoto, hivyo vitu vikiungua nani atalipa gharama.

Kama kuna shida mahala mtupe taarifa, au kama kuna shoti inayopelekea kujivyatua kwa socket braker yenu huko makao makuu ya Tanesco mtuambie.

Au pia kama kuna wanafunzi wa field wanafundishwa mmoja mmoja jinsi ya kuwasha na kuzima Menu switch ya kutusambazia umeme mtuambie.

Mnatukosesha Amani kwa kweli,leo hii mnavyofanya hivyo mkiunguza Rice cooker za mzee Rungwe wali wa kwenye kampeni tutakuwa tunakula wapi?

Kuweni na huruma Tanesco kama Tanesco.
 
... sijui nini tatizo?
....hakuna tatizo, lakini lazima wanaoishi kama malaika lazima washushwechini waishi kama mashetani, ili lipate kutimia neno la Mkombozi wa wanyonge, na si Tanzania ya viwanda tena
 
....hakuna tatizo, lakini lazima wanaoishi kama malaika lazima washushwechini waishi kama mashetani, ili lipate kutimia neno la Mkombozi wa wanyonge, na si Tanzania ya viwanda tena
Hofu yangu ni kwa Rice cooker za hashimu Rungwe zisije zikapigwa shot tukakosa kula ubwabwa,
 
Umejuaje mkuu
Mkuu kabla sijaufungua huu uzi wa jamaa alikuwa ameandika kichwa Cha habari Cha tofauti so nilipofungua nikaona mabadiliko.. so nikajua mods wameshacheza nao easy like that.. jamaa alikuwa kaandika ki zero iq Kama jina lake..😜
 
Au pia kama kuna wanafunzi wa field wanafundishwa mmoja mmoja jinsi ya kuwasha na kuzima Menu switch ya kutusambazia umeme mtuambie,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu ata TANESCO hawapendi hili litokee
Line zetu zimepita sehemu za porini na kusababisha tatizo kama hili

Unaweza kuta kuna miti ipo jirani na line na kusababisha group fault, na kutoa line na kurudi apo kwa papo

Kuna weak point labda mahali mvua inanyesha (shida kama hii inaweza kutokea pia)

Kumbuka line zetu zimetembea kilometers nyingi tu.

Kuna wale wanaochoma nguzo na kusababisha line kutoka kwa over current

Kuna sababu nyingi haya matatizo tungeyaepuka kwa asilimia nyingi kama tungekua Underground transimission line

Tutafika tu
 
Nimekusoma uzuri mkuu
Mkuu kabla sijaufungua huu uzi wa jamaa alikuwa ameandika kichwa Cha habari Cha tofauti so nilipofungua nikaona mabadiliko.. so nikajua mods wameshacheza nao easy like that.. jamaa alikuwa kaandika ki zero iq Kama jina lake..[emoji12]
 
mkuu TANESCO namba za simu za nini wakati umeme unakatika eneo kubwa?hebu angalia malalamiko haya humu angalia maeneo shughulikia.Unaambiwa,Ubungo,mwingine Msewe,Baruti,mimi nakuambia Kimara mwisho,Mbezi..bado hujajua hiyo ni wilaya moja ya kikazi Tanesco?Tanesco Kimara iko shida.Fuatilia utusaidie mkuu TANESCO .Umeme miezi ya nyuma ulitulia lakini sasa hivi unakatikakatika sana.Sometimes muda mrefu saomtimes for 20 to 30 minutes lakini hii haiondoi kero kwa mtumiaji.Tulizeni umeme jamani nyinyi watu.daah!sijui tuwaambieje yaani.
 
Tunapenda kupata mawasiliano ya mteja ili kumpigia na kumsikiliza zaidi kwani tatizo la Ubungo sio lazima liwe la Kimara tunakuletea elimu ya kwanini tunaomba taarifa kamilo hivi punde
 
*TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA*

NAMNA YA KUTOA TAARIFA SAHIHI KUPITIA SIMU NA MITANDAO YA KIJAMII ILI KURAHISISHA UFUMBUZI WA TATIZO HUSIKA.

1.ENEO HUSIKA

(Wateja wanaweza kuishi eneo moja lakini wakahudumiwa na njia (line) ya kusambaza umeme au Transfoma tofauti.)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine Wateja wa mtaa/eneo moja wanaweza kuwa na umeme na baadhi wakakosa umeme, hivyo ni rahisi kuwasiliana na Mteja husika kwa simu.)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Tupatie ufafanuzi wa jinsi ya kukufikia, ili mafundi wetu watatue hitilafu kwa haraka.)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA, UJUMBE GANI UNATOKEA MARA UWEKAPO UMEME?

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.IWAPO UNASHINDWA KUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA IPI?

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme.

TUNAENDELEA KUWAOMBA WATEJA WETU USHIRIKIANO WENU KATIKA UTOAJI TAARIFA SAHIHI ILI TUWEZE KUKUPATIA HUDUMA BORA ZAIDI.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

*TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO*

*Tovuti* www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

*Twitter* www.twitter.com/tanescoyetu,

*Facebook* https://www.facebook.com/tanescoyetultd.

IMETOLEWA NA:

*OFISI YA UHUSIANO*
*TANESCO MAKAO MAKUU*
 
Nafatilia sana kampeni za muh Mara nyingi na anaongea mengi mazuri hasa swala la vijiji vyote kupata umeme na kwa bei ya chini. Ninavyoamini kibiashara unapokua na wateja wengi ndivyo na mapato yanapokuwa mengi. Sasa hawa ndugu zetu Tanesco sidhani Kama wanalitambua hili, hasa hawa managers wa wilaya wengi ni ma Mungu watu, kusikiliza kero za wateja wao ni shida sana.

Mfano mimi nyumba yangu jirani yangu kama mita 50 tu hana umeme, nimeomba umeme sasa ni karibia mwaka unakwisha. Yani kuna umbali unapozidi mita 30 tu wanakwambia usubiri mradi. Na haijulikani huo mradi utachukua miaka mingapi!!

Kwa kweli imekua ni kero juu ya kero. Muh Magufuli hebu jaribu kuangalia hawa ma managers wengi wa wilaya ni kero sana, hawana kauli rafiki kwa wateja zao. Tunaomba wawe wanakwenda sambamba na kauli zako, wananchi tunakukubali sana kwa utendaji wako. Waangalie kwa jicho la pili.
 
Hapo Magu anaongea kisiasa lakini yaliomo ni uongo mtupu.Unaweza kuwalaum Tanesco lakini Magu ni muongo mpaka kupitiliza.
 
TAARIFA YA KUSITISHWA KWA TANGAZO LA AJIRA ZA KAZI MAALUMU MKOA WA TANGA
 
Hello. Hatuna umeme tangu jana. Ni nyumba yetu tu. Tuko Mikocheni Karibu na Five ways. Tunatazamana na babu jaza chips. Nyumba ya pili toka ofisi ya serikali za mitaa darajani, ukitokea Five ways. Umemem ulianza kucheza cheza sasa umezimika kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…