Tanesco namba za simu na maeneo husika huwa mnaziomba za nini ikiwa changamoto zao hamzitatui na kila siku mnaomba namba na mahali mtu anapoishi kitaalamu haijakaa sawa hudumieni wananchi kwa kuzingatia usawa , mtu tu kupatiwa umeme anachukua kipindi kirefu hivi kuomba miundo mbinu imfikie utafikiri anasoma kozi fulani aisee
 
Mna tatizo gani kinyerezi Huku umeme unakatika Kama sio Tanzania bana
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka saa ngapi

Kwa hatua zaidi
Habari za leo,

Naitwa: Farid
Eneo: Ilala,
Simu: 0

Tatizo: Jana jioni/mchana kuna watu walikuja waliojitambulisha kuwa wanatoka tanesco wakakata umeme kwa madai kuna mita yangu ya awali ilikuwa na deni. Wakaacha barua na namba zao za simu, Licha ya hayo wakachukua namba zangu na kuanza kunipigia mara kadhaa.

Mpaka sasa sina umeme leo asubuhi nimeenda tanesco mzambarauni/gongo la mboto walipoangalia mita haina deni bt wamenielekeza niende makao makuu j3.


Naomba msaada plz
 
Ahsante kwa taarifa tunaifanyia kazi
Jmosi hii TANESCO umeme hakuna tena laini ya ya dawasco kimara mwisho.
Hebu mkuu angalia haya malalamiko yangu yamejaa kiasi gani humu kila baada ya siku mbili nipo nawe hapa,uelewe hali halisi ya umeme Kimara mwisho maeneo ya kuanzia korogwe ebonite,mavurunza,dawasco,matangini,Udart,Kimara polisi,hoapitali,kanisa katoliki,sokono,TRA,Michungwani mpaka makaroni (machinjioni).Hii line watu wanateseka na umeme mwezi wa tatu huu sasa.Ni tatizo gani hilo lisiloisha jamani?wiki hii kuanzia jtatu hadi alhamisi umeme unakatwa tu,jana pekee haukukatika ila leo jmosi tena zoezi limerudi.Hebu nyinyi tanesco vaeni viatu vya wananchi wa maeneo haya waliowekeza biashara zao kwenye umeme,muone mnavyotesa watu.
 
Mita za RUKU huwa zinakuwa na madeni au bado una mita ya enzi hizo
 
Tanesco tunaomba mtupatie Namba za simu za mameneja wa kila wilaya,anza na wilaya ya mbinga
 
Tanesco tunaomba mtupatie Namba za simu za mameneja wa kila wilaya,anza na wilaya ya mbinga
Tafadhali tumie huduma kwa wateja huu ndio mfumo sahihi kutoa taarifa
 
Kwa miaka mitatu sasa Wilaya ya Mpwapwa-Dodoma umeme haujawahi kufikisha saa 24 unawaka. Kila siku unakatika hadi mara 5.

Vipi hiki ndio kituo cha Tanesco cha mafunzo ya kukata umeme?

Au ndio mbinu ya kula overtime kwa kigezo cha kutafuta fault?

Au ni mbinu ya kupiga OC hasa mafuta ya patrol?
 
Tafadhali tumie huduma kwa wateja huu ndio mfumo sahihi kutoa taarifa
TANESCO kuna swala tena dogo Sana nimelifuatilia ofisi za wilaya nimeshidwa tatuliwa.Nimekuwa ni mtu wa kutembea kila siku njiani sababu ya wapuuzi wachache ambao lengo lao ni kutaka rushwa,, nimepatwa na hasira Sana sababu mnakela Sana.Tambueni hizo sio ofisi zenu ila ni ofisi za watanzania wote.Dhamira yangu ilikuwa kutoa taarifa kwa kiongozi wa juu kabisa ili nipatiwe ufumbuzi lakini nimeona sio vizuri ni bora nikaanza kumtaarifu meneja wa wilaya.Na nimeomba Namba ya meneja kwa sababu tatizo langu limeshindwa tatuliwa kwa hao mnaoita huduma kwa wateja.Na mnaniambia niwasiliane na huduma kwa wateja ilihali wao ndo wanaonisumbua.Sasa tutaoneshana, Namba ya mheshimiwa Waziri kalemani ninayo hii hapa 0754562366.Nitampigia kesho nikiwa ofisini kwao
 
Tunaomba pia Mlitafutie ufumbuzi tatizo la kukatika umeme Mara kwa Mara huku mtwara ,wilaya ya mtwara hasa maeneo ya vijijini. Tunafanya biashara inayohitaji umeme muda wote.tunapata hasara biashara haziendi. Tafadhalini Sana. Mfano Jana umekata kama Mara sita hivi. Na Leo ndo Tangia saa tano asbh hatuna umeme kabisa
Ahsnateni
 
Mmeshakata hapa Manyanya, B, Mkwajuni hata Moscow naona kama giza hivi.
 
Ikiwa nguzo haziuzwi je malipo ya kufungiwa mita mtu anashauriwa kulipa kabla au baada ya miundo mbinu kumfikia alipo?
 
Habari..

Alhamisi usiku nyaya zilipiga shoti, kesho yake wakaja watu wa service wakatoa waya na kuondoka huku wakisema watarudi kesho..
Mpaka leo hii hawajarudi na hatuna huduma ya umeme, tumewasiliana na huduma kwa wateja zaidi ya mara 10, wakaishia kutupa namba ya supervisor 0655989935, huyu mtu ukipiga simu hapokei kabisa, na ukituma meseji unakuwa umefanya kosa, anakuweka blacklist..
Hivyo tangu alhamisi hatuna umeme..

Chanika mwisho, gogo kwa ndevu mbili...
0765 050591..

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Habari..

Alhamisi usiku nyaya zilipiga shoti, kesho yake wakaja watu wa service wakatoa waya na kuondoka huku wakisema watarudi kesho..
Mpaka leo hii hawajarudi na hatuna huduma ya umeme, tumewasiliana na huduma kwa wateja zaidi ya mara 10, wakaishia kutupa namba ya supervisor 0655989935, huyu mtu ukipiga simu hapokei kabisa, na ukituma meseji unakuwa umefanya kosa, anakuweka blacklist..
Hivyo tangu alhamisi hatuna umeme..

Chanika mwisho, gogo kwa ndevu mbili...
0765 050591..

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…