sawa, ile mmetulaza njaa wengine apa.
 
Tangu jana mnaonekana mna shida kwenye kununua luku. Baada ya ucheleweshaji nimepata token. Ila napoingiza umeme hauingii. Je hii itakuwa ni shida gani?

TANESCO
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza

Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Tanesco Yetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 18, 2021.
 
Swalilangu lijibiwe,kwakua tanesco mnajukumu lakuagiza mita ,mitazenu huingizwa nchini zikiwa kwa matumizi ya viwandani yaani zoote,hakuna inayokuja kwajili ya matumizi yanyumbani ila wananchi tukifungiwa na tukilalamika kuhusu matumizi utasikia andika barua kuomba ubadilishiwe matumizi swali linakuja kwann msiwe mnabadilisha matumizi akati mnawafungia hizo mitazenu?
 
Sasa si mseme tatizo litatatuliwa muda gani?
 
hakuna mbinu mbadala ya watu kupat umeme wakat mnashuhulika na hilo la mfumo ..
 
Umeme vijijini (umeme katika kila kijiji) uliishia wapi? Maana kuna vijiji vingine hadi leo havina umeme na ukiangalia distance kutoka sehemu kwenye umeme utabaki kukenua kinywa tu kwa mshangao.

Angalizo: usinipestie meseji yako bwana TANESCO
 
Imekaa poa sana ila vipi hili la kupata unit 2 kwa mita za majumbani yaani taa,tv,sabufa na hakuna pasi wala freezer?
 
Tanesco mbagala yote temeke yote hamna umeme nimeshtuka saa tisa mpaka muda huu saa kumi na moja asubui shida nini na hakuna mvua wala upepo
 
Tanesco mnakwama wapi simutoe njia mbadala wakati mkishugulikia tatizo la kugoma kwa ununuzi wa luku mnatutia hasara mjue halafu hamjali mpmpo tu
 
Au mnaona furaha kutulaza gizani na kututia hasara mnazingua sana. TANESCO
 
Habari waungwana wa jamii forum.

Leo kipekee kabisa napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mexence Melo na timu nzima ya Jamii forum kwa kutupa uwanja huu maridhawa ili tupate kusemea mambo mbalimbali yanayotusibu.

Leo naomba niangazie huduma za kijamii naongelea umeme, inafahamika kuwa umeme wa REA kwa sasa bei ni 27,000 kama maagizo ya serikali yanavyosema, tatizo linakuja kwenye utekelezaji, TANESCO Mkuranga wanaona kama wanatufanyia HISANI kutuwekea huu umeme.

Wananchi tunahangaika kufuatilia huu umeme bila mafanikio, mimi nina mwaka sasa toka nawafuatilia hawa watu, cha ajabu kuna watu wanaenda kuongea na Manager wa Mkuranga siku chache tu utakuta nguzo mtu analetewa anawashiwa umeme nyinyi wengine mnaangalia tu.

Waziri wa Nishati na Madini mulika hawa TANESCO mkuranga, hapo hapo wanatapeli wananchi na nguzo zenyewe hawawapi. Wale Surveyors wa pale wangebadilishwa, ni wala Rushwa wakubwa. Kuna wakati hadi nikaona ni vema hii 27,000 ikatolewa ikarudishwa bei ya zamani labda wananchi tungethaminika.

Muheshimiwa Rais ni kweli vijiji vingi umeme umewaka lakini ukitembelea ktk vijiji hivyo utakuta ni nyumba chache tu ndio zinawaka umeme nyingi haziwaki, na hawa TANESCO hawashughuliki. Wakija kwako wanakupa Takwimu kwambw kijiji fulani kinawaka lakini ukienda utakuta ni nyumba chache tu ndio zina hiyo huduma. Tembelea Mkoa wa Pwani, wilaya ya Mkuranga, kijiji cha picha ya ndege kitongoji cha Kamegele, pale pana nyumba za gharama wananchi wamejitahidi kujenga, lakini nyumba 15 tu ndio zinawaka umeme kati ya nyumba 1000+. Fikiria nyumba zote hizi zingekuwa na umeme Serikali ingekusanya shillingi ngapi? Mwenyekiti wa kitongoji anakula rushwa pamoja na TANESCO mwenye pesa analetewa nguzo, sasa wananchi wa hiko kitongoji wanataka kuandamana hadi TANESCO Mkuranga hili litakuwa ni doa kwa serikali yako. Tunaomba wahusika mliangalie jambo hili, umeme ni haki yetu na sio HISANI.
 
Ndugu mpendwa mteja wetu

Tafadhali tujulishe umeomba umeme kwa jina gani? Namba ya simu na umelipia mwezi gani kwa hatua zaidi.Unaweza kutuma taarifa hata inbox kwa hatua zaidi
 
Tanesco mbagala yote temeke yote hamna umeme nimeshtuka saa tisa mpaka muda huu saa kumi na moja asubui shida nini na hakuna mvua wala upepo
Huduma imerejea tafadhali
 
Tanesco mnakwama wapi simutoe njia mbadala wakati mkishugulikia tatizo la kugoma kwa ununuzi wa luku mnatutia hasara mjue halafu hamjali mpmpo tu
Ahsante kwa taarifa tunaifanyia kazi.Jm
 
Umeme vijijini (umeme katika kila kijiji) uliishia wapi? Maana kuna vijiji vingine hadi leo havina umeme na ukiangalia distance kutoka sehemu kwenye umeme utabaki kukenua kinywa tu kwa mshangao.

Angalizo: usinipestie meseji yako bwana TANESCO
Je unaongelea kijiji gani? TAFADHALI tambua huduma ya usambazaji wa umeme maeneo ambayo haujafika inaenda kwa awamu hivyo vijiji ambavyo havijapata vitafikiwa mwa awamu zijazo.Jm
 
Huduma ya luku ikirejea mtujulishe hapa hapa maana tumechoka kujaribu kila mara na hela zetu zinakatwa bila kupata token.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…