Habari waungwana wa jamii forum.
Leo kipekee kabisa napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mexence Melo na timu nzima ya Jamii forum kwa kutupa uwanja huu maridhawa ili tupate kusemea mambo mbalimbali yanayotusibu.
Leo naomba niangazie huduma za kijamii naongelea umeme, inafahamika kuwa umeme wa REA kwa sasa bei ni 27,000 kama maagizo ya serikali yanavyosema, tatizo linakuja kwenye utekelezaji, TANESCO Mkuranga wanaona kama wanatufanyia HISANI kutuwekea huu umeme.
Wananchi tunahangaika kufuatilia huu umeme bila mafanikio, mimi nina mwaka sasa toka nawafuatilia hawa watu, cha ajabu kuna watu wanaenda kuongea na Manager wa Mkuranga siku chache tu utakuta nguzo mtu analetewa anawashiwa umeme nyinyi wengine mnaangalia tu.
Waziri wa Nishati na Madini mulika hawa TANESCO mkuranga, hapo hapo wanatapeli wananchi na nguzo zenyewe hawawapi. Wale Surveyors wa pale wangebadilishwa, ni wala Rushwa wakubwa. Kuna wakati hadi nikaona ni vema hii 27,000 ikatolewa ikarudishwa bei ya zamani labda wananchi tungethaminika.
Muheshimiwa Rais ni kweli vijiji vingi umeme umewaka lakini ukitembelea ktk vijiji hivyo utakuta ni nyumba chache tu ndio zinawaka umeme nyingi haziwaki, na hawa TANESCO hawashughuliki. Wakija kwako wanakupa Takwimu kwambw kijiji fulani kinawaka lakini ukienda utakuta ni nyumba chache tu ndio zina hiyo huduma. Tembelea Mkoa wa Pwani, wilaya ya Mkuranga, kijiji cha picha ya ndege kitongoji cha Kamegele, pale pana nyumba za gharama wananchi wamejitahidi kujenga, lakini nyumba 15 tu ndio zinawaka umeme kati ya nyumba 1000+. Fikiria nyumba zote hizi zingekuwa na umeme Serikali ingekusanya shillingi ngapi? Mwenyekiti wa kitongoji anakula rushwa pamoja na TANESCO mwenye pesa analetewa nguzo, sasa wananchi wa hiko kitongoji wanataka kuandamana hadi TANESCO Mkuranga hili litakuwa ni doa kwa serikali yako. Tunaomba wahusika mliangalie jambo hili, umeme ni haki yetu na sio HISANI.