Kwanza natoa shukrani zangu za dhati kabisa
Kwenu TANESCO
Jana nilitoa malalamiko yangu kupitia ukurasa huu.

Na nashukuru kwamba malalamiko yangu yamejibiwa.

Leo hii asubuhi watu wa TANESCO wamefika nyumbani hivi sasa ninavyoongea hapa umeme unawaka nyumbani kwangu.

Aksanteni sana TANESCO
Uwepo wenu humu si wa kuuza maneno
Mnasikiliza kero zetu na kwa kweli mnazitatua kwa wakati sikutegemea kabisa nimelalamika jana tena mtandaoni leo umeme unawaka nyumbani kwangu.

Na mimi mwenyewe vile vile najipongeza kuwepo humu JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu! TANESCO naona sasa wanafanya kazi kweli kweli.
 
TANESCO walipitisha umeme mkubwa kwa MAKUSUDI katika Kiwanja/Jengo letu lilokuwa linajengwa kwa ajili ya biashara,ukakaa miaka 10 tangu 2004 eti kwa kuwa wao ni shirika la serikali hawajatoa fidia hata kidogo bado wanapiga chenga mahakamani kwa kutumia wakili wao,Sipendi kusikia hilo jina... ndo maana na wao wanakaangwa na IPTL sababu hawapo makini,kazi kuwabana wazawa tu katika haki!
 
Toka january nahabgaikia umeme, nimeshakamilisha kila kitu, majibu ninayopewa mpaka leo tutakupigia simu, wakati nguzo ipo nyumba ya pili, je nichukue hatua gani? Nipo RUVUMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuan Uzi wa mkuu mmoja hapa analalamikia kuwa mnataka kumpokonya transiforma aliyo nunua kwa pesa yake mwenyewe.

Acheni Huluma....
 
Ndugu mpendwa mteja
Tunaomba taarifa kamili ya unachokitolea taarifa ili kukupatia ufafanuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu mpendwa mteja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hili lilishajibiwa mkuu Ushimen


Tizama majibu page ya 94 post ya 938
 


TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Wakuu/ Mkuu naomba mniweke sawa.

Nataka kuvuta umeme, Tanesco walivyofika wakasema zinahitajika nguzo 3 mpaka nilipo gharama zilizotajwa ni kila nguzo laki 2.

Nikawa nawashawishi majirani zangu tuchangie hizi gharama nikiwa naendelea na ushawishi nikakuta humu uzi unaoonyesha kua hizo gharama ni kubwa.

Nikaingia mtandao wenu nikatuma email ya kuuliza sikujibiwa, naomba mniambie kama hizo gharama ni halali au la?
 
gari lenye mamba za usajiri T 586 CMA (subaru) limegonga nguzo ya kubwa. Mafundi wanakwenda kuibadilisha sasa hivi ili wateja wapate huduma kwa haraka.

Maeneo yanayokosa ni Zena Kawawa, Quorter za BOT, maeneo ya rain bow, na baadhi ya maeneo ya Mbezi ya chini.Na gari hilo limeshikiliwa site kwa taratibu za kiofisi.

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Bei ya nguzo inategemea na eneo ulilopo, ukiwa mjini bei inakuwa tofauti na ukiwa mjini bei inakuwa tofauti.

Pia katika gharama ambazo tuweka zinaonyesha mwisho nguzo mbili kama kuna nguzo zaidi ya 2 unafanyiwa mahesabu na kupewa gharama halisi mku

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Imetokea hitilafu usiku na kusababisha baadhi ya wateja wa Maeneo Kisesa Sumve na wilaya ya Magu kukosa umeme juhudi zinaendelea kuhakikisha huduma inarejeshwa wakati

Tunaomba radhi

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 

Mimi nipo Njombe, Soliwaya, kwa hapo nilipo nguzo zinatakiwa kua shilingi ngapi?

Hii picha maelezo yake yameniacha, naona Chini imezungumzia REA. Pia imezungumzia njia, sijaelewa imemaanishwa njia ya kupita au kuna njia ambayo ni lugha ya Kitanesco
 
....Kuna member humu alileta uzi kwamba Tanesco baada ya kushindwa kupeleka umeme sehemu aliyojenga, alishauriwa anunue genereta iliyogharimu 6.5m , sasa anasema Tanesco wameifanya yao na hawataki kum refund gharama zake, na pia wanataka kuwaunganisha wateja wengine hata bila kumshirikisha. Hili likoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo limejibiwa post namba 938.
Page ya 94
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…