TANESCO MBONA NIMEMNYANG’ANYA MPANGAJI WANGU REMOTE YA KUINGIZIA LUKU ILI ALALE GIZA KWAKUA AMEKATAA KUNILIPA KODI YANGU ILA NASHANGAA AMEWEZA KUWEKA UMEME BILA HIKI KIMITA CHA KUWEKEA UMEME, ATAKUWA AMETUMIA NJIA GANI NA NIFANYE NINI ILI KUDHIBITI NJIA HIYO.
 
Tanesco mna muhujumu mama sukuma gang haiwezekan kila juma mosi mnakata umeme
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Sema nyie watu Mungu anawaona...mnatukatia umeme mda huu sijui mnafanya magendo yapi
 
Poleni, wasije wakarudisha mgao wa umeme na mambo yao ya kutaka kuuza genereta na mafuta na sola....🤔.

Kukaa bila umeme ni kero inavumilika....

Ila kukaa bila maji kadhia...... huduma zote zinasimama 😅

Akili yangu ishawaza.....

Acha niende ibadani.
 
Nimejaribu kununua kwa Tigo pesa, Mpesa, Airtel Money , Simbanking haikubali
 
Na Makampuni ya mafuta petro station nying hawstoi tena resiti ya Kielectronic
 
Sorry : nahisi ilikua ni suala la network..now iko poa..@moderator futa huu uzi
 
Naomba kujua garama za kufunga mita mpya nataka kwa mtu anayetaka kutenganisha mita yake na ya wapangaji.
 
Habari za wikiendi wananchi wa JMT?
Sisi wakazi wa kijiji cha Merera,kata ya Chita wilaya mpya ya Mlimba (zamani Kilombero) mkoani Morogoro.

Tumeishi bila umeme tangu nchi yetu ipate uhuru japokuwa tupo karibu na bwawa la kuzalisha umeme la Kihansi.
Mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu walikuja kutuwekea nguzo za umeme kutokea CHITA na kutuahidi wangekuja kuweka umeme kabla ya uchaguzi na tuipigie kura CCM.

Cha kushangaza hadi muda huu 30/05/2021 hakuna waya walioweka kwenye nguzo hizo ili tupate umeme.
Nguzo zimesimama tu,watu tulifyeka miti kwenye maeneo yetu ili waweke nguzo na waya ili tupate umeme,cha ajabu wameweka nguzo tupu bila waya.

Ninaomba waziri mwenye dhamana atuangalie kwa huruma sisi wananchi wa MERERA ambao tupo zaidi ya elfu tatu na kuna nyumba tayari zina wiring tayari.

Kama mjuavyo umeme unachochea maendeleo kwa kasi nasi tunatamani kupata maendeleo hayo katika kijiji chetu.

CCM taifa,mkoa na wilaya hebu mtekeleze ahadi yenu ya sisi kupata umeme lasivyo tutaamini kuwa ulikuwa ni utapeli wa kisiasa kwa kuweka nguzo na ahadi ya umeme hewa ili mpate kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.
Naomba kuwasilisha.
 
Kwahiyo kuna watu huko ukiwaambia umeme ni nini inabidi utoe maelezo marefu sana. Kwamba hawajawahi kuuona Umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…