TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Baada ya Serikali kupunguza kulipia umeme Hadi 27,000 tanesco kwenye baadhi ya mikoa ,limeibuka tatizo la kukoseka kwa watumishi wanaojulikana kama ' surveyor, mfano kule Kilimanjaro ofisi ya tanesco mkoa ,kuna surveyor wawili, anaohudumia ofisi ya mkoa.

Hii imechangia kuongezeka kwa rushwa na ukiritimba mkubwa ili kupata umeme wa Tsh 27,000. Cha kushangaza graduates wamejaa mitaani Ila surveyor wa tanesco ni wawili mkoa mzima.

Tunaomba waziri mwenye dhamana na wizara ya nishati, atembelee ofisi ya tanesco mkoa wa Kilimanjaro ajionee maajabu.
 
Tunataka waziri,Naibu waziri na takataka zote za Tanesco ziondoke! Wameshindwa kazi
 
Kama kuna Tatizo toeni taarifa, kuanzia alfajiri ya leo Maeneo ya ubungo, kimara & mbezi (Sijajua kuhusu maeneo mengine) umeme unakatika kila baada ya dakika kadhaa. Kama mmepanga kuharibu mali za wananchi mseme tu
 
Tanesco ni shirika la umma jeuri kuliko yote...sasa hivi wanasema hiyo elfu 27 ni mpaka nguzo iwe karibu yako na kama unahitaji nguzo subiri mpaka Tanesco wakufikie.

Hao ma-surveyor bila pesa hawaji tena wamejiwekea viwango kulingana na maeneo.

TANESCO tulienae humu hana MENO..anakusanya data tu na kuomba namba za simu...ni Nyuki wa mashineni
 
Tanesco ni shirika la umma jeuri kuliko yote...sasa hivi wanasema hiyo elfu 27 ni mpaka nguzo iwe karibu yako na kama unahitaji nguzo subiri mpaka Tanesco wakufikie...
Hao ma-surveyor bila pesa hawaji tena wamejiwekea viwango kulingana na maeneo..
TANESCO tulienae humu hana MENO..anakusanya data tu na kuomba namba za simu...ni Nyuki wa mashineni
Gharama ya kuunganishiwa umeme ni T sh27000 tu kwa wateja ambao wamefikiwa na miundombinu ambao hawajafikiwa Shirika linaendelea kuchukua hatua za kusogeza huduma hii muhimu ili nawo wafikiwe kwa awamu zaijazo.

Tafadhali tambua malipo yote yanafanyika bank kupitia control number unayopatiwa malipo mengine yeyote nje ya hayo haruhusiwi
 
Gharama ya kuunganishiwa umeme ni T sh27000 tu kwa wateja ambao wamefikiwa na miundombinu ambao hawajafikiwa Shirika linaendelea kuchukua hatua za kusogeza huduma hii muhimu ili nawo wafikiwe kwa awamu zaijazo.Tafadhali tambua malipo yote yanafanyika bank kupitia control number unayopatiwa malipo
Gharama ya kuunganishiwa umeme ni T sh27000 tu kwa wateja ambao wamefikiwa na miundombinu ambao hawajafikiwa Shirika linaendelea kuchukua hatua za kusogeza huduma hii muhimu ili nawo wafikiwe kwa awamu zaijazo.Tafadhali tambua malipo yote yanafanyika bank kupitia control number unayopatiwa malipo mengine yeyote nje ya hayo

Gharama ya kuunganishiwa umeme ni T sh27000 tu kwa wateja ambao wamefikiwa na miundombinu ambao hawajafikiwa Shirika linaendelea kuchukua hatua za kusogeza huduma hii muhimu ili nawo wafikiwe kwa awamu zaijazo.Tafadhali tambua malipo yote yanafanyika bank kupitia control number unayopatiwa malipo mengine yeyote nje ya hayo haruhusiwi
Hivi mita za REA kigamboni mnaleta lini?..
 
Tunashukuru kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi.Tafadhali tambua usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali nchini unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo kila eneo litafikiwa kwa awamu zijazo
Ili umeme uwafikie wananchi kwa haraka waajiri kandarasi hata mijini kama wa REA ndiyo umeme utawafikia wananchi kwa haraka,ni kweli watu wengi mijini hawajaunganishwa na umeme kwasababu mbali mbali ikiwamo wa Tanesco kuwa na wafanyakazi wachache na vifaa unaweza kukuta wilaya haina mafundi wa kutosha kwahiyo inakuwa kazi kuunganisha wateja kwa wingi,halafu ikumbukwe wilaya zote hazina store ya vifaa mpaka mikoani.

Taensco walipanga hasa lakini utakuta kazi zinaenda taratibu.

Maoni wafanye sensa za kaya ambazo hazina umeme katika miji,wilaya na mikoa kisha wawape kandarasi watu wasimamishe nguzo pamoja na waya zake ,ibaki kazi rahisi ya kuingiza umeme kwa mteja
 
Naomba mawazo yenu kwa tatizo hili: natumia unit 8 kutwa.

Nina frigdge moja ndogo, taa energy saver kama 5 zinawaka saa 12 a day, tv mbili zinatumika kama saa 5 a day, . Nadhani unit 8 a day huu ni umeme mwingi ninao tumia.

Tatizo linaweza likawa wapi? Nimeleta fundi akacheki wiring akasema iko vizuri.

Ushauri tafadhali.

Asante
 
Back
Top Bottom