TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Je umepata changamoto wapi? Umeomba umeme kwa jina gani? Wilaya gani na namba ya simu tafadhali.
Asante kwa kujibu haraka,nimepata changamoto baada ya surveyor kumaliza kazi yake nilienda ofisi ya Meneja wilaya ya Urambo kufuatilia ili nifanye malipo akasema kuwa walikuwa bado hawatapewa mwongozo wa kuunganisha Umeme kwa wateja kufuatia tamko la Waziri Kalemani pamoja na waraka wa MD wa kuwaelekeza kuwa wateja wote tufungiwe umeme kwa 27,000.

Kwanza akasema Mameneja wote walihoji huo waraka haujafafanua ni mteja wa kuanzia nguzo ngapi au ni mita ngapi mpaka mita ngapi mteja anaruhusiwa kuwekewa kwa gharama ya shilingi 27,000!

Kwahiyo walikuwa wanasubiri ufafanuzi akawa anahisi labda ufafanuzi utatolewa tarehe 1 Julai 2021 ila aligusia kuwa wameambiwa kuwa ni mteja wa kuanzia nguzo moja mpaka nane ndiyo wanaruhusiwa kuunganishwa kwa shilingi 27,000 ila waraka wa kuelekeza bado.

Pili amemwambia surveyor asiendelee na wateja kuwaandikia walipe mpaka huo waraka wa mwongozo utoke anahisi labda tarehe moja Julai 2021 unaweza kutoka.akasema kuna zaidi ya form 100 ameziweka pending kwanza akisubiri mwongozo huo.

Jina nililotumia kwenye Form ni Tunkumbukage Mwamunyage Mabatini, Urambo namba yangu ya simu ni 0623644349.
 
Huu umeme unaokatika Mbezi beach maeneo ya Jogoo kila wakati shida ni nini jamani? Halafu mnakata siku nzima bila taarifa rasmi. Too much TANESCO
 
Habari ndugu
Napenda kujua je bei ya shilingi 27000 kuanganishiwa umeme kwa mimi myeja niliopo mbezi msumi ishaanza kutumika au bado?
 
Habari ndugu
Napenda kujua je bei ya shilingi 27000 kuanganishiwa umeme kwa mimi mteja niliopo mbezi msumi ishaanza kutumika au bado?
 
Tumelipia umeme baada ya survey kwa control number 991032358153 ,shilingi 27,000 za kitanzania.Tarehe 4 February 2021--Ila hadi leo hawajaja kufunga umeme.
 
Fafanua waliofikiwa na miundo mbinu mita ngapi au nguzo ngapi? Hapo fafanua
Tanesco mnashindwa nini kuweka tariffu ya kuwa kutoka mita kadhaa mpaka mita kadhaa shilingi hizi I mteja anachorewa na surveyor anajua tu kuwa jedwali linasoma hivi.kamq jedwali la EURA kuwa kutoka Dar mpaka Mwanza ni shilingi kadhaa hii inarahisisha sana
 
Tanesco mnashindwa nini kuweka tariffu ya kuwa kutoka mita kadhaa mpaka mita kadhaa shilingi hizi I mteja anachorewa na surveyor anajua tu kuwa jedwali linasoma hivi.kamq jedwali la EURA kuwa kutoka Dar mpaka Mwanza ni shilingi kadhaa hii inarahisisha sana
Hii inasababisha wateja kupewa Bill tofauti tofauti kutegemea na manavyoelewana
 
Ninaongea kwa masikitiko makubwa kihusiana na jamaa zetu wa tanesco.

Nipo kijijini kila nikitaka kununua umeme kwa njia ya simu haununuliki ni siku ya pili leo. Nawapigia simu wanasema tununue kwa mawakala.Hii haikubaliki hata kidogo. Ina maana saivi nitoe pesa kwenye simu kuna makato kisha nimfate wakala km 15 pia kuna makato.

Sasa kama nanunua umeme wa elfu tano iliyopo tigo pesa inabidi nitumie tsh 10000 nyengine kuweza kuupata huo umeme. Hii sio sawa haya si matumizi sahihi ya tehama katika kurahisisha huduma na kupunguza gharama.

Tanesco mjipange sana. Mnatuzingua kwa kweli.
 
Mnatojibu pia malalalmiko kuhusu kuunganishwa umeme wa REA vijijini?

Kijiji changu mwaka wa sita sasa sijaunganishwa umeme na kila nikienda kufuatilia taarifa zilizopo katika makaratasi yao inaonekana kijiji husika kishapata umeme nikachoka hata kufuatilia kwa sababu ukweli mpaka ninapoandika hapa kijiji hakina umeme na kilichopo nyuma ni hadithi nyingi sana zinachosha kusikiliza.
 
Mnatojibu pia malalalmiko kuhusu kuunganishwa umeme wa REA vijijini? Kijiji changu mwaka wa sita sasa sijaunganishwa umeme na kila nikienda kufuatilia taarifa zilizopo katika makaratasi yao inaonekana kijiji husika kishapata umeme nikachoka hata kufuatilia kwa sababu ukweli mpaka ninapoandika hapa kijiji hakina umeme na kilichopo nyuma ni hadithi nyingi sana zinachosha kusikiliza.
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Mtanzania yeyote mwenye matatizo kuhusu tanesco namba hiyo hapo, 0689877735
0768 985 100/ 022 219 4400

Tafadhali tunawasihi kutumia namba zetu za huduma kwa Wateja kutoa taarifa ili mpate namba za taarifa na huduma kwa wakati.

Huduma kwa Wateja

Makao Mkuu
 
TANESCO hivi huduma kwa wateja/emergency Kigamboni mbona simu zote hazipatikani? Hivi lini nyie mtakuwa serious?!
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina: KIJIJI CHA MPUGHA

Eneo: KIJIJI CHA MPUGHA/TARAFA YA NGOPOLYO

Wilaya:RUNGWE

Namba ya simu: 0715 454189/0769 250 699

Tatizo: UMEME HAUJAFIKA PAMOJA KUWEKWA NGUZO MIAKA 5 ILIYOPITA

Toka lini:2012

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Tanesco mbona mko kimya kuhusu ufafanuzi ni mteja yupi anastahili kuunganishwa umeme kwa 27,000?

Kwani tangu waraka wa MD wa tarehe 4 June 2021 ulioagiza kuwataja wafungiwe kwa 27,000 mameneja walihoji ni mteja wa nguzo ngapi afungiwe kwa gharama hizo hakuna jibu hii imepelekea wateja wote wapya wawekwe pending kusubiri huo waraka wa ufafanuzi.

Karibu mwezi unaisha hakuna mteja mpya anayeshughulikia. Kama mwezi mzima hamjaunganishia wateja wapya hamuoni shirika linaingia hasara?
 
Back
Top Bottom