TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO HIVI TUNALAZIMIKA KUJA OFISINI KWENU MARA NGAPI ILI MTATUE KERO ZETU?

Nimeleta malalamiko ya kuharibika kwa meter ambayo tena ni ya zamani ( 04088164605) ambayo hajabadilishwa kwa sababu zisizojulikana na pamoja na kubisha hodi mara 4 ofisini mikocheni kilometer zisizozidi mbili toka sehemu ninakoishi na kupewa RF: 0210 huu unaenda ni mwezi wa Pili hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa- inasikitisha, nafikiria kwenda EWURA ku lodge malalamiko rasmi.
 
TANESCO HIVI TUNALAZIMIKA KUJA OFISINI KWENU MARA NGAPI ILI MTATUE KERO ZETU??
Nimeleta malalamiko ya kuharibika kwa meter ambayo tena ni ya zamani ( 04088164605) ambayo hajabadilishwa kwa sababu zisizojulikana na pamoja na kubisha hodi mara 4 ofisini mikocheni kilometer zisizozidi mbili toka sehemu ninakoishi na kupewa RF: 0210 huu unaenda ni mwezi wa Pili hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa- inasikitisha, nafikiria kwenda EWURA ku lodge malalamiko rasmi.
Ahsante kwa taarifa je namba ya taarifa ni ya mwezi gani na namba ya simu tafadhali
 
Tanesco mbona mko kimya kuhusu ufafanuzi ni mteja yupi anastahili kuunganishwa umeme kwa 27,000 ? Kwani tangu waraka wa MD wa tarehe 4 June 2021 ulioagiza kuwataja wafungiwe kwa 27,000 mameneja walihoji ni mteja wa nguzo ngapi afungiwe kwa gharama hizo hakuna jibu hii imepelekea wateja wote wapya wawekwe pending kusubiri huo waraka wa ufafanuzi. Karibu mwezi unaisha hakuna mteja mpya anayeshughulikia. Kama mwezi mzima hamjaunganishia wateja wapya hamuoni shirika linaingia hasara?
Wateja wote waliofikiwa na miundombinu ya umeme wanafungiwa kwa Tsh 27000, Wateja ambaoa hawajafikiwa na miundombinu kuna miradi inaendelea kwa awamu mbalimbali kuwafungia umeme hivyo hakuna changanoto kwenye muongozo uliotelewa
 
Ahsante kwa taarifa je namba ya taarifa ni ya mwezi gani na namba ya simu tafadhali

Ni ya mwezi wa tano na namba ya simu wanayo, ukiangalia data zangu kwenye hiyo meter namba na malalamiko niliyoleta utakuta namba yangu
 
Wateja wote waliofikiwa na miundombinu ya umeme wanafungiwa kwa Tsh 27000, Wateja ambaoa hawajafikiwa na miundombinu kuna miradi inaendelea kwa awamu mbalimbali kuwafungia umeme hivyo hakuna changanoto kwenye muongozo uliotelewa
Kwa watejwa tajwa inachukua muda gani kufungiwa umeme baada ya kufanya malipo??
 
Vipi Arusha Kuna mgao wa umeme kimyakimya? Nimesikia Njiro asubuhi haukuwepo umerudi jioni na sisi huku kijenge chini mmekata jioni saa kumi na mbili, mnamwangusha mheshimiwa kwa kuwa na mgao wa umeme bila taarifa
 
Tanesco tunaomba mnapokuwa na katizo la umeme mtoe taarifa kwa wateja jana kutwa nzima eneo lote la olasiti arusha hatukuwa na umeme. Hebu badilikeni muwe kibiashara jamani.
 
Wateja wote waliofikiwa na miundombinu ya umeme wanafungiwa kwa Tsh 27000, Wateja ambaoa hawajafikiwa na miundombinu kuna miradi inaendelea kwa awamu mbalimbali kuwafungia umeme hivyo hakuna changanoto kwenye muongozo uliotelewa
Mbona mimi surveyor alikuja kwangu tarehe 11 june 2021akapima ikapatikana mita 76 kutoka kwenye miundo mbinu lakini kakatazwa na Meneja kuwa utaratibu bado au mita 76 iko nje ya miundo mbinu?

Hata kupewa Bill tu imeshindikana kuwa wanasubiri utaratibu au waraka wa kunipa Bill ili nilipe ? Nikaambiwa kuwa form zetu zaidi ya 100 zipo pending zikisubiri
 
Wateja wote waliofikiwa na miundombinu ya umeme wanafungiwa kwa Tsh 27000, Wateja ambaoa hawajafikiwa na miundombinu kuna miradi inaendelea kwa awamu mbalimbali kuwafungia umeme hivyo hakuna changanoto kwenye muongozo uliotelewa
Fafanua kufikiwa na miundo mbinu ni mwisho mita ngapi? Hapo hujafafanua, mteja ni yupi ambaye amefikiwa na miundo mbinu ? Ni mita ngapi kutoka kwenye miundo mbinu ndiyo yumo kwenye huo mradi wa 27,000?

Ambao wako nje ya miundo mbinu ni kuanzia mita ngapi kutoka kwenye nguzo? Hapo fafanua please
 
Tunashukuru kwa maoni yako mpendwa mteja
Mita namba = 43002630549 button zake hazibonyezeki, kwa hiyo hatuwezi kuingiza tokeni. Takribani mwezi wa pili sasa hakuna msaada wowote kutoka ktk ofisi ya Tanesco tawi la Kibara wilaya ya BUNDA (licha ya kuwataarifu mapema sana).

Namba zangu ni 0623340895
Namba za ofisi ya Tanesco-tawi la kibara ni 0782788802. Tunaombeni msaada wenu, tuko gizani ni mwezi wa pili sasa.
 
Mita namba = 43002630549 button zake hazibonyezeki, kwa hiyo hatuwezi kuingiza tokeni. Takribani mwezi wa pili sasa hakuna msaada wowote kutoka ktk ofisi ya Tanesco tawi la Kibara wilaya ya BUNDA (licha ya kuwataarifu mapema sana).
Namba zangu ni 0623340895
Namba za ofisi ya Tanesco-tawi la kibara ni 0782788802
Tunaombeni msaada wenu, tuko gizani ni mwezi wa pili sasa.
Ahsante kwa taarifa mpendwa mteja wetu, tumepokea kwa hatua zaidi
 
Hili swali naona halijaonekana, naomba kuwauliza tena;Baada ya mteja wa Tzs 27000 kulipa inachukua muda gani kufungiwa umeme.?
 
Wakuu leo AIRTEL na TIGO, luku imegoma! naomba anaejua mitandao mwingine ninayoweza kununua umeme aniambie.
 
Mimi airtel nilinunua mchana walinipa token ila kwa kuchelewa, sasa hivi wanagoma kabisa voda pia.
 
Back
Top Bottom