Na Kama ikifahamika inamatatizo. Mfano inasoma Umeme zaidi. Je kiwango kilichozidi kinaweza kurudishwa au ndio hasara yangu
 
Na Kama ikifahamika inamatatizo. Mfano inasoma Umeme zaidi. Je kiwango kilichozidi kinaweza kurudishwa au ndio hasara yangu
Kabla ya kulipia hio gharama, wanakupa maelezo kama hio mita itakuwa kweli inakula umeme zaidi na TANESCO tukaibadilisha tutakupa unit zenye thamani ya gharama uliolipia ya kufanyiwa uchunguzi yaani METER TEST ambayo ni shilingi 3000 tu


Asante

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Habari TANESCO hivi tatizo la mita temper linasababishwa na nini? maana inajirudia mara kwa mara na utatuzi wake wa kudumu ni upi, natanguliza shukrani
meter no 24217433721
 
Habari TANESCO hivi tatizo la mita temper linasababishwa na nini? maana inajirudia mara kwa mara na utatuzi wake wa kudumu ni upi, natanguliza shukrani
meter no 24217433721
Mita inaweza kutemper endapo unakosea kuweka umeme au kuingiza token zisizo au yenyewe inaweza kujitemper, hatua za kutatua mita itakapotemper ni mpaka wataalamu wetu wafike eneo lako kujua chanzo cha temper ni nin?

Mita imechezewa au imejichezea,
Kwa swala lako je nini kinakusibu,? Mita ukiingiza umeme inaonyesha nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna magari yanapita mkoani Dodoma, yamebeba mizigo yenye urefu mkubwa. Hivyo italazimika kuzima baadhi ya laini kwaajili ya usalama. Tunaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza katika kupita huko kwa magari hayo

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
maeneo ya Kiluvya gogoni, hondogo, pamoja na maeneo jirani kila siku umeme unakatika, asubuhi na jioni, imekuwa kero, kukatikakatika kwa umeme tunakosa uhakika wa kufanya shughuli zetu za kibiashara. tunaomba mtupe uhakika.
 
maeneo ya Kiluvya gogoni, hondogo, pamoja na maeneo jirani kila siku umeme unakatika, asubuhi na jioni, imekuwa kero, kukatikakatika kwa umeme tunakosa uhakika wa kufanya shughuli zetu za kibiashara. tunaomba mtupe uhakika.
Kwa siku ya jana kulikuwa na hitilafu kidogo na kazi ilifanyika vyema na kurudisha umeme kama wewe bado una tatizo tunaomba namba yako ya simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa hivi ni saa 12:29 umeme umekatika tena maeneo yote ya kiluvya gogoni, hondogo, kwa kawawa, hii ni zaidi ya kero.
 
maeneo haya umeme unakatika mara kwa mara, usumbufu mkubwa ktk shughuli zetu za uzalishaji.
 
umekatika mara ya tatu sasa maeneo ya kiluvya gogoni, kuanzia tisa jioni hii hadi sasa hakuna uzalishaji, hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu, hakuna maendeleo bila umeme wa uhakika,
unaweza kufanya mawasiliano na injinia wa kanda kuthibitisha ukatikaji huu unao endelea maeneo haya,
 
Mimi Nina shida na umeme lakini BEI IPO juu sana na nguzo IPO njee kwangu wala pia aifiki mita kumi naombeni majibu inakuwaje hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpendwa mteja wa Shirika la Umeme Tanzania

Tunapenda kukujulisha kuwa gharama za kufungiwa umeme sasa zimeshuka sana kutoka laki nne na kitu mpaka 321000 kwa wateja wa mijini waliopo ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo inayowalisha umeme na Tsh 177000 kwa wateja wa vijijini waliopo ndani ya umbali huo huo.

Aidha mteja anaweza kulipa kwa awamu tatu ili kufungiwa umeme (three installments) lakini atafungiwa umeme mara baada ha kumaliza malipo ya awamu ya tatu

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…