Schedule Maintainance aliyotuambia January Makamba inaisha lini!???

Maana ni takribani miezi mitano sasa inakaribia hakuna kauli wala tumaini la kueleweka kuhusiana na kukamilika kwa ukarabati huu, kana kwamba hii mitambo nchi nzima ilinunuliwa kipindi kimoja hivyo yote kwa pamoja imechoka tena imechoka pamoja baada ya Kufariki Magufuli

Kiukweli naanza kuamini zile kauli za Magufuli kuwa matatizo ya umeme nchini ni 'mikono ya watu' wakishirikiana na viongozi wa Serikali kuanzia wizara husika mpaka Tanesco

Haiwezekani Kufariki kwa Magufuli tu na kuondolewa kwa Kalemani basi ndo matatizo ya umeme yaanze

Rais Samia chonde chonde amka Mamá yetu, umekaa na Hayati bega kwa bega miaka mitano tafadhali pita njia zile zile mlizokuwa pamoja ili tuzibe huu ufa ulioanzishwa na hawa wahuni, vingnevyo tutaja jenga ukuta kwa gharama kubwa
 
Toka jana umeme umekatwa saa 9 za usiku sababu tumeambiwa moto wa soko la karume na mkatoa tangazo maeneo yatakayo adhirika, swali langu huduma mtarudisha lini?
 
Mmezingua TANESCO kwa nini mnakata umeme asubuhi yote hii mnajua leo sijaenda shule nilikuwa nataka niangalie katuni boomerang tv za asubuhi ndio nzuri

Leo la nne wengi hatujaenda shule ni siku ya usafi watafanya madogo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Niliomba control number tokea Jumanne bado tu sijaipata
 
Nadhani alipokuwepo umeme ulikuwa haukatiki katiki kila mara ! Tuseme kweli tu !
Hata sasa haukatiki mara kwa mara,watu tumekuwa wanafiki na chuki zisizo na sababu umeme ukikatika kidogo tu inakuwa nongwa lakini ukweli hata wakati wa huyo mnayemuona mungu mtu hitilafu za hapa na pale zilikuwepo.
Haiwezekani umeme ukatike tu bila sababu.
 
Toka niripoti tatizo hili sijapata msaada, siku ya 5 leo sina umeme, nishawapigia simu nishafika ofisini majibu mepesi tu, DM mnanipa majibu mepesi tu, nyie jamaa bhana TANESCO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…