SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO MKOA WA MOROGORO .
TAARIFA YA KUOMBA RADHI KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME MAENEO YA MKOA WA MOROGORO .
Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Morogoro linaomba radhi wateja wake kutokana na kukosekana kwa huduma ya Umeme baadhi ya Maeneo ya Mkoa wa Morogoro.
TAREHE:26-01-2022.
Siku:Jumatano.
Sababu: ni kutokana na hitilafu iliyojitokeza katika Miundombinu ya Shirika na kupelekea Maeneo mengi ya Mkoa kukosa huduma ya Umeme.
Maeneo yanakosa huduma ya umeme kwasasa ni pamoja na Mzumbe,Mzinga,SUA,Kididimo,Mlali,Mgeta,Maguruwe,Area 5&6,Kola ,Manyuki na Maeneo mengine yanayotumia laini hiyo
Tahadhari usishike wala kukanyaga nyaya zilizolala chini toa taarifa emergency kupitia namba 0677063001,0684889272 au ...
Uongozi wa Shirika Mkoa wa Morogoro unaomba radhi kwa Usumbufu utakao kuwa umejitokeza.