TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Jamani tanesco ninapenda kuwaambia mmeshaleta nguzo na kuichimbia ,,mimi tatizo mbona hamniunganishi sasa?ni siku ya tano imechimbiwa,,,,
Tupatie taarifa zako zaidi na sisi tuweze kuifuatilia mkuu, upo mkoa na wikaya gani bila kusaau majina uliotumia kuombea umeme au namba ya fomu ya maombi ya awali

TANESCO
MAKAO MAKUU
HUDUMA KWA WATEJA
Kituo cha miito:0768985100 AU 022 2194400
Barua pepe:customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.twiter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescoyetu
 
Kero yangu ni pale mteja anapolipia hela yake ili awekewe Huduma ya umeme halafu hapati Huduma kwa wakati inachukua hata mwaka na mkiulizwa visingizio vinakuwa vingi utasikia hatuna nguzo, nyaya zimeisha subiri tumeagiza mita makao makuu dar es salaam. Mnatuboa sana sisi Wateja wenu tuliopo mikoani.
Pole sana mkuu, je unaweza kututajia namba ya fomu ya maombi ya umeme ili tuqeze kuifuatilia zaidi

TANESCO
MAKAO MAKUU
HUDUMA KWA WATEJA
Kituo cha miito:0768985100 AU 022 2194400
Barua pepe:customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.twiter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescoyetu
 
Afadhali namie niwaulize...hivi hizi meter zenu kuziweka juu...halafu hizi remote za kuingizia umeme ni mbovu sana ikitokea imedondoka kidogo hazifanyi tena kazi.

Nina mwezi kama watatu sijaweka umeme kwakua remote yangu imeharibika..nimeomba kushushiwa kila siku napewa ahadi....Mara nilipe elfu 70..Mara watakuja nisubiri...ukiangalia jengo ni LA ofisi ya kijiji pia kuna kisima ambacho wananchi wanapata maji....sasa hakuna tena hiyo huduma...nipeni majibu natakiwa nifanye nini?

au basi kama kushusha ngumu waje kuniwekea umeme wapande juu kule ya nguzo....maana ofisini kuna mlinzi shida ya kuwekewa meter ukutani ni IPI?
 
Afadhali namie niwaulize...hivi hizi meter zenu kuziweka juu...halafu hizi remote za kuingizia umeme ni mbovu sana ikitokea imedondoka kidogo hazifanyi tena kazi....Nina mwezi kama watatu sijaweka umeme kwakua remote yangu imeharibika..nimeomba kushushiwa kila siku napewa ahadi....Mara nilipe elfu 70..Mara watakuja nisubiri...ukiangalia jengo ni LA ofisi ya kijiji pia kuna kisima ambacho wananchi wanapata maji....sasa hakuna tena hiyo huduma...nipeni majibu natakiwa nifanye nini?au basi kama kushusha ngumu waje kuniwekea umeme wapande juu kule ya nguzo....maana ofisini kuna mlinzi shida ya kuwekewa meter ukutani ni IPI?
Mkoa
Wilaya
Namba ya simu
Namba ya taarifa

Je umeshalipa kiasi ulichoambiwa tanesco? Maana ukikiharibu inakuwa jukumu lako kukilipia tena
 
Siku hizi mnakata sana umeme bila sabab mwanza, umeme unawaka dakika tano unakata mara unarudi mnataka kutuunguzia vyombo au
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA MFUMO WA LUKU

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa jana majira ya Saa 5:39 usiku ilitokea hitilafu katika mfumo wetu wa LUKU iliyopelekea Wateja kukosa huduma ya LUKU.

JITIHADA ZILIZOFANYIKA

Wataalamu wetu walifanya jitihada za kurejesha huduma na majira ya Saa 01:54 Asubuhi ya leo Septemba 16 huduma ilirejea.

Iwapo bado unapata tatizo wasiliana nasi kupitia: Kituo cha miito ya simu Makao makuu 0222194400 au 0768 985100

Mitandao ya Kijamii
Tanesco Yetu,
Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

TANESCO
MAKAO MAKUU
HUDUMA KWA WATEJA
Kituo cha miito:0768985100 AU 022 2194400
Barua pepe:customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.twiter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescoyetu
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO*

*TAARIFA YA UBIRESHAJI WA MIUNDOMBINU MKOA WA TABORA*
Shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Tabora, linapenda kuwataarifu wateja wake wote wa wilaya ya Nzega kuwa kutakuwa na kazi ya uboreshaji wa miundombinu yaTanesco meeneo ya Uchama siku ya jumamosi ya tarehe 16/09/2017.

*MUDA* Kuanzia saa 2:00 asubuhi_12:00 jioni.

*MAENEO YATAKAYOATHIRIKA*
Nzega mjini, Honge, Itilo, Utwigu, Mwanhala, Mwambaha, Ngukumo, Nkiniziwa, Busondo, Puge na Ndala, Itobo, Bukene, Mbutu, Mambali na Ishihimulwa.

*TAHADHARI*Tafadhali usiguse, usikanyage wala usishike waya uliokatika maana ni hatari kwako.

*MAWASILIANO* Piga dawati la dharura:
0788 684535, 0786 558 810,
KITUO CHA MIITO MAKAO MAKUU: 0222194400/0768 985 100
*TOVUTI* www.tanesco.co.tz

*TANESCO INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA*

*IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO HUDUMA KWA WATEJA TANESCO MKOA WA TABORA.*
[15/09, 21:58] Vesso: SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME LAINI YA KIBARA 66KV SIKU YA JUMATATU NA ALHAMISI TAREHE 18 & 21 SEPT 2017 KUANZIA SAA 01:30 ASUBUHI HADI SAA 12:30 JIONI.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mara Wilaya ya Bunda linawataarifu wateja wake kuwa njia ya umeme ya msongo wa kilovolti 66 Bunda Kibara itazimwa ili kupisha matengenezo siku ya JUMATATU NA ALHAMISI 18 & 21 Septemba 2017, kuanzia Saa 07:30 Asubuhi hadi Saa 12:30 Jioni ili boresha hali ya upatikanaji wa umeme.

SABABU: Kubadilisha nguzo 18 zilizooza.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Kisiwa cha Ukerewe, Kibara, Sikiro, Kabirizi, Gege, Namalebe, Nakatuba, Masahinga, Bulendabufe, Mchigondo, Igundu, Chitengule, Busambara, Makwa, Mwitende.

UONGOZI UNAPENDA KUOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA, MAFUNDI WETU WATAKUWEPO KAZINI WAKIFANYA MAREKEBISHO KUHAKIKISHA MAENEO YOTE YANAPATA UMEME PINDI KAZI ITAKAPOKAMILIKA.

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini, toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe.

Wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: -

Kituo cha Miito ya Simu 2194400 na 0768 985100

Kitengo cha dharura Wilaya ya Bunda
0282621225/0683408068/0758531068

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja
TANESCO-MARA.
15/09/2017
[15/09, 22:15] Samuel Mandari: SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
(TANESCO)

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEME MKOA WA KILIMANJARO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kilimanjaro
kuwa kutakuwa na katizo la umeme kupisha zoezi la ukataji miti kwenye njia kuu za umeme na maboresho ya miundo mbinu.

Katizo la umeme litakuwa kama ifuatavyo:

16.09.2017 .Jumamosi
Kuanzia saa 02:00 asubuhi mpaka 11:00 jioni.
MAENEO YATAKAYOTHIRIKA

-Manispaa ya Moshi:-
NI.Kiborilon, KDC, Mbokomu, Old Moshi Tela, Majengo Ngangamfumuni na Rau Sabasaba,

-Wilayani Mwanga:- Kagongo,National nyabinda, Lang'ata, Kiti cha Mungu, Handeni, Bunge bora, na ustawi wa jamii.

17.09.2017
Jumapili Kuanzia saa 02:00 asubuhi mpaka 11:00 jioni.
MAENEO YATAKAYOTHIRIKA NI.

-Wilaya ya Mwanga :-
Kagongo, National nyabinda, Lang'ata, Kiti cha Mungu, Handeni, Bunge bora, na ustawi wa jamii.

Kwa dharura yoyote wasiliana na dawati.la dharura Mkoa wa Kilimanjaro kwa simu namba 0272755007/ 0272755008/0682771310/0765397925

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:
Ofisi ya Afisa uhusiano na huduma kwa wateja- TANESCO KILIMANJARO
15/09/2017
[15/09, 22:16] Robert Mbavai: SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME MKOA WA KAGERA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera linawataarifu baadhi ya wateja wake wa Mkoa wa Kagera kuwa kutakuwa na katizo la Umeme tarehe 16.9.2017 muda wa saa 02:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.

SABABU; kubadili Miundombinu chakavu na kukata miti iliyo karibu na laini.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Kibeta Busisi,Rwamishenye,kagondo,kyamzinga yote,yabugabo,kaifo,karuguru,Kyakairabwa,mugana,maeneo yote ya Kanyingo,maeneo yote ya Kashasha,Bugandika,Ruzinga na Kitobo.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Kagera : 0785 787898/0753 120701.

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano na huduma kwa Wateja
TANESCO -Kagera
14.09.2017

TANESCO
MAKAO MAKUU
HUDUMA KWA WATEJA
Kituo cha miito:0768985100 AU 022 2194400
Barua pepe:customer.service@tanesco.co.tz
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.twiter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescoyetu
 
TANESCO Kilimanjaro waanza kampeni ya Jihadhali na ajali za umeme.
Tutapita mtaa kwa mtaa, wilaya kwa wilaya, kijiji kwa kijiji na gari letu la Matangazo kutoa elimu hio.
397d84d081e681d243f570a18d6d361b.jpg
159289bd92bd92b351f7ca1c3d990b4b.jpg
2fb15df1acf3f4f2d9f51a69c163658e.jpg
a1b88d35a0b55b3998b7b779475b0594.jpg
 
Tumeipokea mpendwa mteja tutawasiliana na wewe kwa ufatilaiaji zaidi

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
[HASHTAG]#TANESKO[/HASHTAG].
NITALETA MREJESHO WA UFUATILIAJI WENU, NAKILA KITU KILIVYO KWENDA HAPAHAPA.

NAAMIN threads HII ILIANZISHWA KWA LENGO LA KUPOKEA MALALAMIKO YA WATEJA ,MAONI NA USHAURI,NA KUSHUGHULIKIWA NA IDARA HUSIKA,,NA SIYO KWA LENGO LA KUICHAFULIA TANESKO KWENYE MITANDAO KAMA INAVYO FASILIWA NA BAADHI YA WAAJIRI WENU MNAO WATUMA KUJA KUSHUGHULIKIA KERO ZETU.

[HASHTAG]#Tanesko[/HASHTAG]
 
Basi mueke hizo remote kama za decoder ikiharibika unaenda dukani unanunua mwenyewe....sasa napata shda kumbe mmeziweka juu makusudi ili zikiharibika mtuuzie tena remote kwa hiyo tsh 70,000?

Na sijui kwanini mpaka Leo mpo peke yenu...maana kila kitu tumelipia bado Leo mtulipishe na hivi viremote vyenu...
 
Mi niko Arusha umeme kwangu umekata tokea mchana jirani angu tunaeshea line anao naomba mje kunirekebishia, niko makao mapya jengo ni LIMPOPO karibu na KEN GARDEN. naomba sana
 
Nawakilisha wananchi wa maeneo ya Mtaa wa Shewa, Kata ya Mwakibete (karibu na kwa masista), Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoani Mbeya:

Shida yetu: umeme bado haujafika maeneo ya kwetu. Tuliwahi kufuatilia TANESCO kuhusu kuvutiwa umeme hadi eneo letu, na kupeleka barua rasmi, lakini walivyokuja watu wa TANESCO wakasema kuwa eneo letu ni la mradi wa REA;

Baada ya muda kidogo wakaja hao watu wa REA, wakaweka nguzo kwa eneo kidogo, kisha wakapotea, hadi leo ni zaido ya miezi 9 sasa hakuna kinachoendelea.

Tukifuatilia TANESCO, hakuna jibu la maana tunalopewa, tafadhali sana tunaomba mtufikirie, na sisi tunatamani na kuhitaji sana umeme.

Namba ya balozi wetu ni 0754312532, analifahamu vizuri hili suala kwa kuwa tulishirikiana nae hatua kadhaa za kufuatilia ofisi za TANESCO.
tunaomba mlishughulikie hili swala.
TANESCO
 
Nipo mkoa wa mwanza wilaya ya misungwi juzi TANESCO wamekuja kuniwekea Huduma ya UMEME nyumbani kwangu ila cha ajabu walipoondoka nilipokuja kuchunguza namba ya mita na iliyopo kwenye card imezidiana kwa namba moja mf iliyopo kwenye meter inasomeka hivi 37154734976 na ya Card ni 37154734976 5. Sasa hapo sijajua namba sahihi ni IPI nisije kununua UMEME kumbe nanunua kupitia namba ya MTU mwingine
 
Nipo mkoa wa mwanza wilaya ya misungwi juzi TANESCO wamekuja kuniwekea Huduma ya UMEME nyumbani kwangu ila cha ajabu walipoondoka nilipokuja kuchunguza namba ya mita na iliyopo kwenye card imezidiana kwa namba moja mf iliyopo kwenye meter inasomeka hivi 37154734976 na ya Card ni 37154734976 5. Sasa hapo sijajua namba sahihi ni IPI nisije kununua UMEME kumbe nanunua kupitia namba ya MTU mwingine
Tunaomba namba yako ya simu
 
Nawakilisha wananchi wa maeneo ya Mtaa wa Shewa, Kata ya Mwakibete (karibu na kwa masista), Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoani Mbeya:
Shida yetu: umeme bado haujafika maeneo ya kwetu. Tuliwahi kufuatilia TANESCO kuhusu kuvutiwa umeme hadi eneo letu, na kupeleka barua rasmi, lakini walivyokuja watu wa TANESCO wakasema kuwa eneo letu ni la mradi wa REA; Baada ya muda kidogo wakaja hao watu wa REA, wakaweka nguzo kwa eneo kidogo, kisha wakapotea, hadi leo ni zaido ya miezi 9 sasa hakuna kinachoendelea.
Tukifuatilia TANESCO, hakuna jibu la maana tunalopewa, tafadhali sana tunaomba mtufikirie, na sisi tunatamani na kuhitaji sana umeme.
Namba ya balozi wetu ni 0754312532, analifahamu vizuri hili suala kwa kuwa tulishirikiana nae hatua kadhaa za kufuatilia ofisi za TANESCO.
tunaomba mlishughulikie hili swala.
TANESCO
Tumeipokea mpendwa mteja
 
Back
Top Bottom