Sikh imefunguka kwa umeme kukatika kikawaida lazima ukatike Mara 5 kila Sikh
Cha kushangaza kuna majitu yanamlaumu mzalendo January makamba,hivi hawajui mitambo ilikuwa imechakaa kipindi cha mwendazake
Makamba ni genius sana jamaa in kichwa mnooo
Kweli wewe chizi
 
Kwann mnakatakata umeme sana aisee? Ina maana enzi za hayati Magufuli hizo changamoto mlizokua nazo sasa hivi, kipindi kile hazikuwepo? Mbona mnamdharau Madam president kiasi kikubwa hivyo?

Au kwa sababu haongei na hafanyi tit for tat kama hayati Magufuli? 😡
 
Bhana Tanesco mbeya wamebadil kaz badala ya kufanya umeme upatkane wao wameamua kufanya kaz ya kukatata umeme usipatikane tena bila taarifa kila siku lazma umeme ukate shda nn hatupew taarifa sijui hii mnatusaidiaje
 
Anaupiga mwingi sana,kama kuna meneja nchii hii anayejali matengenezo ya mitambo basi nii yeye

Sehemu kubwa ya mwanza kila Siku haina umeme kisa mzalendo huyuu anahangaikia matengenezo ya mitambo chakavu

Apandishwe cheo haraka hataa wauza majenereta hapa town wanamkubali sanaaa
 
TANESCO wakazi wa Goba njianne nyuma ya ofisi ya KIURE hatuna umeme kwenye nyumba kadhaa.

Tunaomba msaada wa haraka usiku huu maana hili joto sio poa.
 
Tanesco naleta malalamiko kutoka kwa wananchi mitaa ya Mapalilo na kawawa ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa KIBAIGWA mkoa Wa DODOMA.

Octoba-2021 Ulikuja mradi wa REA wakasambaza nguzo kwa baadhi ya nyumbani na wengine wakaachwa kwa maelezo dhaifu ya upungufu wa nguzo lakini hata Wale waliopewa nguzo mpaka leo haijulikana mradi umekwama au laaah ukimya usio wa kawaida na hata wanapoulizwa baadhi ya wanohusika hawatoi majibu ya kueleweka.

Kutucheleweshea umeme ni kutucheleweshea maendeleo tunaomba muangazie maisha yetu kwa haraka.
 
Ngoja aje akuulize
wilaya
mkoa
Namba ya simu
Pamoja na maelezo yako mazuri ila Bado akija atakuuliza hayo maswali hapo juu.

Hivi Tanesco wanatuchukulia watanzania wote ni wajinga haiwezekani Kila mtu anawalalamikia wao utadhani huo umeme wanatupa bure, watanzania tuamke.
 
Tanesco wilaya ya Hai mna tatizo gani!?
Umeme unawaka na kuzimika mara kwa mara hamuoni mnaharibu mali za watu? Toka jana usiku hadi sasa umeme umekatika zaidi ya mara nne. Tatizo nini?
 
TANESCO Nina tatizo la makato ya Debt collected (Kodi ya pango) kwenye mita yangu ninavyojua malipo ni elfu 10 kwa mwaka Sasa nikipiga mahesabu nimeshalipia zaid ya hyo na bado wanaendelea kukata.

Lingine kwenye sehem ninayofanyia biashara wanafanya hivyo hivyo na hyo nyumba moja tunatumia mita 5 yan kula mtu na yake na wote tunakatwa naomba Kama unaweza kunipa ufafanuzi kidogo
 
Jamani tanesco wilaya ya kilombero (mlimba) mnatufanyia nini hiki? Kila siku za mpira hasa Simba na yanga mnakata umeme,,watu wanaishi kwa kutegemea vibanda umiza acha kufanya ivo tafadhali
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa hatua zaidi
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa hatua zaidi
Malipo yamekamilika.01318959580
9001220660845157097
Units 106.7KWH

Token 7355 9635 5842 0416 5357

Cost 31,147.55
VAT 18% 5,606.55
EWURA 1% 311.48
REA 3% 934.42
Debt Collected 2,000.00
TOTAL 40,000.00 07/03/22 08:45

 
Malipo yamekamilika.01318959580
9001220660845157097
Units 106.7KWH

Token 7355 9635 5842 0416 5357

Cost 31,147.55
VAT 18% 5,606.55
EWURA 1% 311.48
REA 3% 934.42
Debt Collected 2,000.00
TOTAL 40,000.00 07/03/22 08:45View attachment 2142093
Je tatizo ni nini hapo?Tafadhali tujulishe, umekatwa kodi ya majengo kwa muda wa miezi minne
 
Tuliaminishwa sana na viongozi kuwa mitambo ya Tanesco zilikuwa zikifanya kazi bila marekebisho kwa muda wa miaka mitano. Ndiyo maana umeme unakatika katika.

Tukaaminishwa tena na viongozi wazalendo wa nchii kuwa maji yamepungua kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme na hii imechangiwa na ukame ndiyo maan umeme unakatika katika ovyo ovyo.

Taseco ikatangaza siku 10 kwa ajili ya mate matengenezo ya mitambo ya umeme ili kumaliza kabisa tatizo la kukatika kwa umeme. Na hii ilifanywa kwa weledi mkubwa tukafunga mkanda siku kumi. Umeme unakatwa saa moja asubuhi unarudi kesho yake yaani saa sita usiku. Tumevumilia nchi ikiwa gizani na kuamini sasa lile tatizo la umeme kukatika katika ovyo inakomeshwa kisawa sawa.

Baada ya ukame mashee na mapadre na viongozi wakuu wa serikali na wananchi kwa ujumla wetu tukafunga na kumwomba Mungu atupe Mvua. Hakika Mungu akajibu maombi Yetu tukapata mvua mabwawa ya kufua umeme yamejaa, mpaka Leo mvua bado zinanyesha sehemu nyingi ya Tanzania.

Naomba kuuliza Tanesco tatizo nini sasa kama mitambo yamerekebishwa na mengine kubadilishwa na mabwawa ya kufua umeme yamejaa na maji. Kwann umeme unaendelea kukatika ovyo je bado kuna mgao wa umeme. Toka last week umeme maeno ya Tegeta mpaka wazo madale yote hayana umeme.

Leo toka asubuhi umeme hakuna shughuli zetu zimesisima. Waziri husika na wahusika wote wa Tanesco tatizo ni nini?

Kwanni mnatuonea sana sisi tabaka la chini?

Wengine hatuna pesa ya kununua Majenerata na solar mnatusaidiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…