TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Surveyor ulimlipa? Maana mi naombwa pesa
Maelezo yenu ni mazuri ila watendaji wenu ni tatizo,nataka kuunganisha umeme kijiji(nyumbani) walikuja wakafanya survey,hadi leo sikuwahi kutumiwa control number,baada ya mzee wangu kufuatilia kwa muda mrefu akaambiwa zinahitajika nguzo tatu na anapaswa kulipia sh 3m ili kuunganishiwa umeme,hii ni halali?
 
Mimi Ni mteja wenu nipo Buza Sigara karibu na msikiti wa Mpeta, tarehe 14/06/2023 nilituma ombi la kubadilishiwa ya mita ya zamani na kupatiwa mita mpya,zinazotumia remote.na nilipatiwa ticket namba 2658529.Imetimia week mbili bado sijapata mrejeshe (feedback) au kufikiwa na wahusika.
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tunaomba namba ya mita kwa ufuatiliaji zaidi tafadhali.OK
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tunaomba namba ya mita kwa ufuatiliaji zaidi tafadhali.OK
Mita namba 04202838969 nyumba namba 02 barabara ya Tuamoyo karibu na msikiti wa Mpeta Mtaa wa Sigara
 
Asante tanesco huduma kwa wateja mmetatua changamoto yangu ya token ndani ya dk 8 umeme unawaka,keep good work
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tunaomba namba ya mita kwa ufuatiliaji zaidi tafadhali.OK
Muhonda /raha na mitaa kibao kwa nn umeme hakuna bila sababu ya msingi kulikoni?
 
LEO SIKUKUU HAMUONI AIBU KUTUKATIA UMEME WAKAZI WA TABATA KISIWANI?
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tunaomba namba ya mita kwa ufuatiliaji zaidi tafadhali.OK

Tanaseco naomba kuuliza kama kuba uhaba wa transformer maana meeneo mengi unakuta nyingi sana zinahudumiwa na transformer moja matokeo yake watu wanapata umeme mdogo.

Unakuta unahangaika na fundi ukidhani vitu vime haribika kumbe tatizo ni umeme mdogo,mnapo unganisha wateja wapya mnashindwa kujua transformer moja inatakiwa kuhumia nyumba ngapi!?

Au mnafaidika na umeme kua mdogo!?
 
Hello! Naomba kufahamu, Hivi mteja anayehitaji kuunganishiwa umeme anapaswa kumlipa surveyor ili kumfikia mahali pake?
Ukiafuata mwenyewe hapo utatoboka Tu
Ila wakija wenye nadhan hamna kitu
 
Tanaseco naomba kuuliza kama kuba uhaba wa transformer maana meeneo mengi unakuta nyingi sana zinahudumiwa na transformer moja matokeo yake watu wanapata umeme mdogo.

Unakuta unahangaika na fundi ukidhani vitu vime haribika kumbe tatizo ni umeme mdogo,mnapo unganisha wateja wapya mnashindwa kujua transformer moja inatakiwa kuhumia nyumba ngapi!?

Au mnafaidika na umeme kua mdogo!?
Unaposema umeme mdogo unamaanisha ni wa kiwango gani mkuu?
 
Anaeweza kuiba meter ndo anaweza kuiba mafuta kwenye transformer na hata kuunganisha umeme. Kwa hapo ni vigumu kumkamata mwizi maana wanajuana.
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
•Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
•Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
•Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
•Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
•Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
•Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= (REA)

Gharama hizi ni kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 18%
Ili upate gharama halisi ni lazima wapimaji wafike katika eneo lako.

TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU : 0748550000.
^ OK
Nipo umbali wa mita 140 kutoka kwenye nyumba yenye umeme, mimi nilipo nahitaji njia tatu kwa ajili ya kuendesha mashine, hii itagharimu kiasi gani?
 
Back
Top Bottom