TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco nipo dodoma mjini mtaa kizota ninachangamoto ya nguzo ya umeme ya mradi wa REA imechimbiwa ndani ya kiwanja changu bila kushirikishwa siku wanachimbia nilikuwa safarini ,SAsa nataka kufanya ujenzi nashindwa nguzo imechukua nafasi kubwa pamoja chuma zake mnazochimbiaga chini nguzo isiyumbe ,nataka isogezwe pembeni ni hilo tu
 
Tanesco mbona hamjibu nini shida?
Tanesco nipo dodoma mjini mtaa kizota ninachangamoto ya nguzo ya umeme ya mradi wa REA imechimbiwa ndani ya kiwanja changu bila kushirikishwa siku wanachimbia nilikuwa safarini ,SAsa nataka kufanya ujenzi nashindwa nguzo imechukua nafasi kubwa pamoja chuma zake mnazochimbiaga chini nguzo isiyumbe ,nataka isogezwe pembeni ni hilo tu
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali andika barua ya kuhitaji mita hiyo ihamishwe ambatanisha na taarifa zako muhimu kama jina lako, namba ya simu na eneo kiwanja kilipo pia kitu maarufu kama kipo nfano kanisa, msikiti, shule, hospital na uta scan barua hiyo na ututumie kupitia namba yetu ya whatsapp 0758346869 au kwenye email yetu ya customer.service@tanesco.co.tz, utapata huduma.^OK
 
TANESCO, JE ILE APPLICATION YENU YA NIKONNECT NI UHAKIKA????
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, app ya Nikonekt ni ya uhakika jihudumie kwa urahisi na haraka.^OK
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1. ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2. NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3. KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4. JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5. MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6. KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7. KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

NAMBA ZA SIMU ZA MADAWATI YA DHARURA YA TANESCO MIKOA YOTE

1. Ilala

0222133330/ 0784 768586/ 0715 768586.

2.Kinondoni Kusini (Magomeni)

0784271461/ 0715271461

3. Kinondoni Kasikazini(Mikocheni)

0784 768584/ 0716 768584

4. Temeke

0222138352/ 0732 997361/ 0758881055/ 0712 052720

5. Pwani
078 5122020/065 7108782/023 2402386

6. Mbeya
0759 777781/0787 023422


7.Arusha
0758174343/
0622612501/
+255 27 2506110

8.Tanga
0658 122 412/0687 677 667/ 027 2646 779

9. Kilimanjaro
0765 397 925/0682 771 310/ (+255) 272 755 007/8

10 Manyara
0689 795 599/ 0627938951

11. Mwanza
0759 777 786/0687 910 202/
(+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

12. Geita
0744 085 696/(+255) 28 2520330

13.Kagera
078 5 787 898 / 075 3 120 701/(+255) 282 220 061

14.Mara
0788 950 688/
028 262 2020/
0762 165 087

15.Simiyu
+255 282 700 180/0626383440/0745044072

16. Dodoma
0782 161 643/(+255) 262 321 728

17. Morogoro
068 4889272 /065 4829046/ (+255) 232 613 501/2

18 Singida
071 4 477 445 /0732 960 924 / 0689 373 757/(+255) 262 502 133

19. Tabora
0786 558 510 /0763 162 868

20. Shinyanga
0754 521 070/(+255) 28 2762120 /
0783 521 070

21. Kigoma
078 3720598/(+255) 2988226

22. Katavi
0688345200

23. Rukwa
0252161120/0768879813
24. Songwe
0684 611716/0763 430381.

25. Ruvuma
0252602281/0763 194 979/0787 758 986

26. Njombe
0744703988

27. Mtwara:
0789 999942/023 2333902

28. Iringa 0262702019/0739203015

29. Lindi
0752518247/0685692786


Kituo cha Miito ya simu/Call Centre Makao Makuu

0768 985 100/0222194400

Facebook
www.facebook.com/tanescoyetu

Twitter
www.twitter.com/tanescoyetu

Tovuti
www.tanesco.co.tz

Barua pepe
Customer.service@tanesco.co.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Salama, nahitaji kubadili jina LA umiliki wa mita na pili nataka kuunga umeme kwenye nyumna ambayo nguzo IPO ndani ya eneo langu naloishi haizidi mita 20. Je gharama ipoje kuunga umeme kwan umbali huo?
 
Habari TANESCO naomba msaada najaribu kuweka umeme kwenye MITA lakini ingoma yaani unit Zina reject naomba suluhisho
 
TANESCO SISI WAKAZI WA TINDE -SHINYANGA TUNASHINDWA KUELEWA NI KWANINI HAIWEZI KUPITA WIKI 1 KAVU BILA UMEME KUKATIKA..(Never) NI KWA VILE WATU WALIO NJE YA MIJI MIKUBWA WANAONEKANA HAWAWEZI KUPAZA SAUTI ZAO MITANDAONI HIVYO HAWANA MADHARA AMA SHIDA NINI ? Mnachosha
Namkumbuka Magu kwakeli yaani hili limekuwa tatizo sugu, kila siku umeme nikukatika na haijulikani ufumbuzi wake, tunaishi kijima sana
 
Kila la heri TANESCO ila hakikisheni mnaondoa tatizo la kukata umeme kutwa nzima bila taarifa, pia punguzeni gharama za umeme kwenye upande wa bei za kuvuta umeme pamoja na kushusha kidogo bei za units za umeme.
 
Kila la heri TANESCO ila hakikisheni mnaondoa tatizo la kukata umeme kutwa nzima bila taarifa, pia punguzeni gharama za umeme kwenye upande wa bei za kuvuta umeme pamoja na kushusha kidogo bei za units za umeme.
Usiku huu umeme huku Tabata giza kali shida sijui ni nini
 

Hivi ni kwanini nguzo za zege hazitumiki kama nguzo za umeme?​

Habari wana jamvi,
Kama heading inavyojieleza hizi nguzo za TANESCO ambazo zimetengewa kwa cement uimara wake ni mdogo na ni hatarishi hasa maeneo ya makazi na yenye watu wengi.

Awali nilijua labda zinatengenezwa ndani zinawekwa nondo na seng'enge ili kuongeza uimara kumbe ni tofauti ,hii ni hatari kwasababu kokoto na cement haihusiki kama mti unavyojishika, cement ina tabia ya kujiachia tofauti na nyuzi katika mti , ndio maana hata mti(nguzo ya mti) ikigongwa na kitu kizito uangukaji wake utakuwa tofauti na nguzo ya zege inavyodondoka

Nguzo ya zege inakatika vibaya ikiwa inashuka, unadondoka mithili ya jengo kuporomoka kwa maana itashuka ikiwa vipande vipande tofauti na ya mti ambayo inaweza ikaanguka ila bado imejishikza kidogo palipo katika

Iwapo TANESCO wameamua kutumia hizi za zege vizuri hata ziwekwe nondo ambayo italinda uporomokaji mbaya au kukatika hovyo.

Inasemekana moja iliwahi kuanguka maeneo ya Mwananyamala ikaua mtu.

Kuna haja ya kuziwekea nondo ziwe imara hivi hivi zitakuwa na madhara sana.
Source: ITV
 
TANESICO tz kwanza nawasalim kwa jina la jamuhuri,,mm nimepata Changamoto mwezi na nusu Sasa umepta na tatzo ni kupitia wafanyakaz wenu baaz kutokuwa waaminifu,, mm ni fund wa vitu kama laptops,simu nk,Sasa Kazini ninapojipatia riziki jirani yetu mwenye nyumba alimua kubomoa na Ili aboreshe Sasa sis tulikuwa tukipewa huduma ya umeme kutoka kwa jirani kwa sababu tulipo mwenye mita yeye hatak kushare umeme na mtu,Sasa baada ya aliekuwa anatupa umeme kubomoa na kuanza ujenz mm na baaz tulikoswa umeme.Nilikaa mda wa miezi kama Mitano nikifanya Kaz kwa shida,mwisho nikaamua nianze kujichanga Ili nije nifungiwe mita yangu.sasa Kuna siku alikuja mteja kazin kwangu akiwa na laptop mbovu kwa lengo la kutengenezewa nikampokea ila nikamuomba kuwa ntaenda jirani kukutengenezea coz hapa kwangu umeme kipengere jamaa akaniuliza Kwan shida nn mbona hauna umeme? nikamuweka waz Changamoto zote, jamaa akaniambia pole akaongeza kwa kusema yeye anafanya kazi TANESICO na anaweza nisaidia ,mm nikamwambi kwa Sasa si tunalipi kidigatal hakuna aja ya kuwafata unapakua app yao na kujiunga na kulipia na unaletewa huduma,,jamaa akaniambia napo ni sawa ,wakat naendelea kukagua Kaz yake jamaa akanipa wazo lingine akaniambia yeye alikuwa ana duka sehem na bihashara haikwenda sawa akabidi afunge Ili ajipange upya na alikuwa kafunga mita yake kuepusha Kero ya umeme dukan kwake kwahiyo kama Niko vizr anaweza niletea hiyo mita na Kunifungia niedelee na Kaz na akaenda mbali akasema ninaweza mm kwenda badil jina ikasoma majina yangu bas akatoa kitamburisho akanionyesha ,,tukaogea bihashara na mwisho akaniambia nmpe lak2 atakuja na vijana wafunge,nikamwambia anipe namba ntamtafuta nikkamilisha hiyo pesa,Nika pigana baada ya wiki nikamtafuta akaja akafunga nikaanza Kaz, na akaniambia kuwa baada ya mwezi ndio nilipie coz amelipia mwez mzm,nikamshukuru na Kaz Sasa zikaaza coz nilkuwa sifanyi Kaz vizr,,Sasa shida ilikuja baada ya wiki tatu kwenda nne hv kumaliza mwez, vijan ninaowafundisha Kaz walitangulia kufungua mm nilichewa kidogo, mida kama saa4 asubui ilikuja gari nyeupe yenye usajir wa sm namba sikumbuki, wakashuka mpk kazin wakawakuta madogo wakajitamburisha kuwa ni maafisa wa TANESICO na wanamashaka na mita ya umeme,basi wakafungua wakakagua wakadai mita inachepusha umeme kwahiyo Iko direct hailipii umeme,,wakaomba namba zangu nikapogiwa sim wakadai niwai mm nikamwambia kuwa bado Niko nyumba waliposikia hvyo wakasema utawakuta wadogo zako polis wakakata sim nikapga wakadai Nije polis pamba. Kiufup mm Niko mwanza na nafanyia shuguri zangu mjin,bas nakachukua boda mpk polis pamba baada ya hapo nilikuta madogo wako kituon,nilpofika niganganiwa nikapelekwa mpk kwa injinia kitengeo Cha upotevu wa mapato niongee nae,yeye alisema mita Ina miaka 4 haijalipwa umeme na pia mita ni ya wizi kwahiyo Nina kesi nying ikiwemo kuujum uchumi,Sasa Mimi nikamwambia kuwa twende kazin waulize mita inamda Gani imefungwa pale pili nikamwambia Aile nifungia mita namba yake hii hapa inapgiwa inaita na anapokea kwann nayeye asifatiliwe coz uko hewan na yupo hapa mwanza,wao wakadai wanadili na Alieshikwa na mita bas,dah waliniomba pesa nyingi Ili waweze kuniachia,nilipga cm nyumban ,kwandugu ,marafk niweze kutoa kias walichokitaka Nitoke mpk Sasa Nina maden mengi kisa hii kitu,,.Sasa kumbe yele jamaa alikuwa ameshafanyia watu wengi,anawafanyia hvyo Kaz wema pia wapo baada ya wiki jamaa akanitonya akaniambia Kuna mtu almfanyia kama mm ko kampata na yuko polis makao makuu mwanza,nikakimbia nikakuta ni yeye,kuwapigiwa wa TANESICO hawakunijal polis wakasema tuje badae au kesho tulikuwa watu wawil,kesho napigiwa simu na asikari wa Ile Kes ananiambia kesho nisiende atanitafu ,baada ya siku mbil nikapga cm hapokei kwenda kituoni Kona zikawa nyingi mwisho nikpenyezewa kuwa ni kishoka wao TANESICO Kes haipo,nililia sana.
 
Hivi kipindi Cha magufuli iliwezekanaje umeme kutosumbua kwa miaka yote akiwepo madarakani,Nini kimebadilika ambacho hakikuwepo kwenye utawala wake kimefanya mpandishe Bei ya umeme je nyinyi sio sehem ya HUDUMA na ni anasa kwa mtanzania ?
 
Tanesco UsaRiver, Arusha ,kitu mnachokifanya sio sawa kabisa.Mnazima umeme ,maji ya chai siku mbili mfululizo,usiku na mchana bila taarifa yeyote.Tafadhali mtufahamishe kama kuna mgao ili tuelewe!
 
Back
Top Bottom