TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nimebadilishiwa mita tangu tarehe 25 Nov'23 lakini hadi leo mita mpya Na. 24316665157 haiwezi kuingiza token na hivyo niko gizani kwa zaidi ya siku 10; Na. ya taarifa karibuni ni 4568614, kama kuna malipo niambieni
Boss umeenda Tanesco wanasemaje?
Muda huo wote uko gizani umeshindwa hata kupiga mtu huko Tanesco?

Huu sasa ujinga
 
Sishangai jamaa kukaa Giza siku 10, kwangu hata Jana nimelala Giza( Dar (suka ,golani mtaa casino) .. yani umeme huwa wakatika nyumba zetu ziko kama Kimi hivi,, na hata tukipigia emergency mara wapokee mara hawapatkani na wakipokea hawaji.. wakuta siku mbili haupo moja upo ..imefika hatua tumechoka mno..mi tatizo endelevu..na emergency hawana Maana Tena kwetu..
 
Kwenu Tanesco
Maeneo ya Maji ya chai,Imbaseny,Wilaya ya Arumeru,Mkoa wa Arusha,Kumekuwa na kukatika kwa umeme kwa masaa zaidi ya 24.Tunajua kwamba kuna mgao wa umeme nchi nzima lakini huku kwetu imekuwa zaidi ya mgao.Tafadhali wahusika Tanesco naomba mliangalie hili suala kwa umakini.Sisi tunaendesha shughuli zetu za kiuchumi kwa kutumia umeme.
Hapa ninavyoandika hapa hakuna umeme.
 
TANESCO. MISIMU YA MVUA NI MIWILI. VULI NA MASIKA. RATE YA KUFUNGULIA MAJI KWENYE MABWAWA NI KUBWA KULIKO KATE YA MAJI KUINGI. HIVYO MABWAWA NANAPUNGUA SANA MAJI.

SULUHISHO:
KILA BWAWA MBELE KIDOGO BAADA YA MAJI KUPITA KWENYE MAPOROMOKO YA KUFUA UMEME BASI KUWE NA KINGIO, ZUIO LA MAJI ILI MAJI YAWE PUMPED BACK BWAWANI NA YALE YA ZIADA TU YARUHUSIWE KUENDELEA NA SAFARI.

HAKUTAKUWA NA UHABA WA MAJI BWAWANI NA KINA CHA MAJI KUSHUKA.
 
Meter No: 24314740135
Nikinunua umeme najibiwa akaunti ya mpokeaji haipo, mita ni mpya.
 
Naomba kuuliza mimi niliwekewa umeme tarehe za katikati yaan tarehe 18 na nimebahatika kubadilisha kwenda kwenye tarifu 4
Sasa swali langu ni hili kuhesabiwa mwezi ni kila tarehe 18 mpaka 18 au au pale mwezi unapoanza kulingana na kalenda ndo nami naanza mwezi maana naogopa kuzidisha matumizi
 
mmesahau kukata umeme leo mbona ? au muda bado ?
kuanzia Gomes , Pugu, Kigogo Fresh, Chanika mpaka Mvuti
 
Mi nashauri hili shirika lifungwe kabisa nawaingie mkataba mpya na shirika jingine
 
Kwani nyie majamaa hiyo taasisi ina shida gani? Kwanini mnakata umeme kila kukicha? Kwanini ni hadi kila kitu hadi atokee mtu wa kuwapeleka puta, Je ni kwamba hamjitambui au hamtambui wajibu wenu au kwa kuwa ni jambo la kuhusu UMMA ndo sababu ya kufanya utumbo kila kukicha? Mwanzo mlisema upungufu wa maji ndo sababu ya umeme kupungua na kupelekea mgao ila sasa mvua zinanyesha na maji ni mengi lakini bado mnaendelea kukata umeme je, shida ipo wapi nyie watu wa hovyo mnaofanyia hiyo taasisi kazi? Ni lini rangi nyeusi itaweza kujisimamia kwa weledi bila huu upuuzi wa kuumiza wananchi kwa maslahi ya wachache? Mungu anawaona ama hakika na mtalipia ninyi na vizazi vyenu Gademit.

Shame on you TANESCO 's Leadership
 
Nimelipia umeme kwa gharma za nguzo tangu tarehe 27/10/2023 mpaka leo sijingiziwa huduma hiyo ni buyuni eneo mgelula,na kila siku naziona nguzo zinarudishwa ofisini.
 
Back
Top Bottom