TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO nyie ni mojawapo ya mashirika ya hovyo Tanzania

Shukuruni Putin si rais wetu mngeshanyongwa siku nyingi
Ayaa kafungueni maji sasa kule kwenye mabwawa hili mseme hayajajaa.
 
Nina tatizo la umeme nyumbani pangu, ninawapigia Tanesco kuwajulisha wananipokea vizuri kisha wananipa semina, bonyeza moja, bonyeza mbili halafu wananipa maelezo ya ulipaji kodi ya jengo!

Kisha nimefuzu wananipeleka ukumbini kucheza bongofleva, itaimbaa itaimbaa itaimbaa halafu simu inakatwa, hapo ndiyo mwisho wa graduesheni.

Utapiga tena na tena na tena mambo ni hayohayo! Tanesco na sisi tunamambo mengi ya kufanya tuhudumieni kwa ule mpango mliouanzisha mkauua baada ya kuona unawaua njaa na tangazo lake mkalifuta.
 
Hawa ni kuwarekodi na kuweka hapa au yotubev hiyo call center yao inavyo sanifu wateja wenye shida za dharura
 
Call center yao haina maana yoyote, ni bora isiwepo tu. Unapiga simu mpaka unachoka, simu haipokelewi.
 
Hawa ni kuwarekodi na kuweka hapa au yotubev hiyo call center yao inavyo sanifu wateja wenye shida za dharura
Hivi karibuni kulianzishwa mpango uliowaondoa wateja kwenye ofisi zao, mpango huo ulitufanya tusionane na mafundi kitu ambacho mafundi walianza kufanjaa kwani simu za taarifa zilipokelewa na wengine huku wao wakipewa maelekezo tu. Kuona hivyo wameuhujumu mfumo huo na kuturudisha kwenye ofisi zao ili tuelewane!
 
TANESCO.
Kuna jambo linanishangaza. Tanzania ina misimu miwili ya mvua. Vuli na masika. Mabwawa yanaweza kujaa au yasijae.

Sasa kwanini TANESCO hawaoni umuhimu wa KUVUNA MAJI YANAYOTIRIRIKA BAADA YA KUFUA UMEME NA KUYAPUMP BACK KWENYE BWAWA NA KUACHA YALE TU YA ZIADA HASWA WAKATI WA MASIKA. UMEME NI WENU. UNACHOHITAJI NI KUYAKUSANYA NA KUYARUDISHA NA SIO KUYAACHA YA POTEE BAADAE UNAANZA KULALAMA.

AMKENI.

BWAWA LA MWALIMU NYERERE HILO LIFIKIRIWE MAPEMA.

HIVI KUKIWA NA UKAME MIAKA 3 NCHI HAITAKUWA NA UMEME?
Haiwezekani mkuu,,
Uzalishaji wa umeme unaenda sambamba na kutuza viumbe hai walioko mtoni na pembezoni mwa mto,,so ukiyazuia kabisa utawaua
 
Hampokei simu za wateja
Screenshot_20231214-084655.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi umeme mnaunganisha lini kutoka Ikungi kwenda Matongo? Tushatuma maombi miezi 6 sasa hamna anayejua nini mnataka, nguzo zimeshawekwa na umeme kuwaka hamtaki wateja sasa?! Au ndio mnasubiri muunge wakati wa uchaguzi? Tupeni umeme tunalipa kwa pesa zetu wengine hatuna mambo ya siasa mbovu hizo.
 
Back
Top Bottom