TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Habari Tanesco. Eneo la Five ways bar Mikocheni mmeanza tena kutukatia kwa ubalozi. Tangu Jumamosi mnakata kila siku. Tukiuliza mnasema line yetu ina hitilafu. Hitilafu gani ina ratiba? Hairekebishiki miezi kadhaa sasa? Watu WA huduma kwa wateja hawapokei simu ukichagua option ya Kiswahili. Poa Wana majibu ya hovyo sana.
Kama line hii ina hitilafu, tuhamisheni kwenda kwenye hii laini ya pili isiyokatiwa umeme kabisa. Poa tunahofia usalama wetu na Mali zetu, maana tayari mtaa huu tulishaunguliwa na vifaa.
Tunaomba suluhisho la kudumu tafadhali.
 
TANESCO UsaRiver,Wilaya ya Arumeru, Arusha.
Mnakata umeme maeneo ya maji ya Chai,Imbaseny saa moja asubuhi na kurudisha saa 6 usiku.Huu mgao umekaaje.Sasa tutafanyaje shughuli za kiuchumi kwa huu mgao wa umeme Tafadhali tunaomba mlitazame hili jambo!
 
Tanesco nyie ni wababaishaji sana sijui mtaacha Lini Ubabaishaji yaani hilo shirika mnakera sana mnakata umeme miaka yote kasoro Magu alipokua madarakani
 
Mama kutamka miezi sita basi hatakama tatizo linarekebishika kabla ya huo muda ila hamtajali mtaendelea kukata hadi huo muda ufike, Najua bado hata baada ya muda kupita bado mtaendelea kukata maana viuno vyenu havina mfupa.
 
Nimenunua umeme kupitia tigo pesa...
Tokea saa 8 na dakika 10
Leo tar 20 .12 2023
Sijapewa token
Miter no ..24219180114
 
nyegezi malimbe mwanza kuna shida gani jana mmekata umeme asubhi jion ukarud dakika 30 mkapitia nao tenah umerud saa 6 usiku na leo saa 1 mshapita nao daah mtuone huruma aisee wegine biashara zetu tuna tegemea umeme aise
 
TANESCO kiboko. Umeme usiku kucha una fluctuate hii ni mara ya pili ndani ya wiki 1.
Mtaunguza vitu vya watu. Si muuzime tuu. Au ndio mmetumwa ili watu waingie hasara.
Nchi Ngumu Hii.
Kama tuko karne ya 17 . Ma Engineer gani awo walioajiriwa TANESCO. HII KITU CHA KUCHEKWA . LABDA KAMA NI MAKUSUDI KUWATIA WATU HASARA ILI WAKANUNUE VITU VIPYA KARIAKOO
 
Umeme una fluctuate ukimaanisha unakatika kila mara. Kwanini vijana wa siku hizi mnapenda vidhungu wakati hamvijui?? Si bora uandike kihehe tu
 
Umeme una fluctuate ukimaanisha unakatika kila mara. Kwanini vijana wa siku hizi mnapenda vidhungu wakati hamvijui?? Si bora uandike kihehe tu
Sii maanishi hivyo. We ndio hujuwi kizungu . Na maanisha unapanda na kushuka . "Power Fluctuation"
Hakika utakuwa CCM .
Ni haibu sana kwa kijana kama wewe kushindwa hata kutumia Google kujifunza kabla ya kujibu.
 
Hakuna kitu rahisi Duniani kama kuongoza wanachi Wasiojielewa, Wananchi mngekuwa mnajielewa haya mambo yasingetokea

HONGERA CCM.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hakuna kitu rahisi Duniani kama kuongoza wanachi Wasiojielewa. Wananchi mngekuwa mnajielewa haya mambo yasingetokea

HONGERA CCM.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Sasa wewe ndio mmoja wa wasiojielewa ambaye unashindwa ata kujuwa "Power Fluctuation" alafu unasema wenzio.
WE MILEMBE INAKUHUSU.
Na unasema ongera CCM..? ( kama sio "JANI" linazungumza basi sijuwi nini
 
TANESCO kiboko. Umeme usiku kucha una fluctuate hii ni mara ya pili ndani ya wiki 1.
Mtaunguza vitu vya watu. Si muuzime tuu. Au ndio mmetumwa ili watu waingie hasara.
Nchi Ngumu Hii.
Kama tuko karne ya 17 . Ma Engineer gani awo walioajiriwa TANESCO. HII KITU CHA KUCHEKWA . LABDA KAMA NI MAKUSUDI KUWATIA WATU HASARA ILI WAKANUNUE VITU VIPYA KARIAKOO
Injinia wa zamu Teneso week hii kitengo cha mgao.
 
Back
Top Bottom