TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
25ca59b86ceed9c2a429145c0b76166b.jpg
Mkuu uchukua muda gani kuunganishiwa toka yanapotumwa maombi?
 
Naomba kuuliza mradi wa kupeleka umeme kisongo wilaya ya monduli utaanza lini? Maana sasa pamekuwa mji na watu wengi wamejenga na kuhamia hapo nikiwa mmoja wapo.

Hivyo naombeni kujua hilo. Asanteni na ninawatakia kazi njema
 
Naomba kuuliza mradi wa kupeleka umeme kisongo wilaya ya monduli utaanza lini? Maana sasa pamekuwa mji na watu wengi wamejenga na kuhamia hapo nikiwa mmoja wapo. Hivyo naombeni kujua hilo. Asanteni na ninawatakia kazi njema
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja
 
Tanesco sasa hii ni kero kila siku mnakata Umeme Chanika nn shida au mpaka tuandamane mpaka kisarawe post..ndo mtupe majibu Maana hii sasa kero na watu wenu wa kisarawe wana majibi mabaya kweli
 
Tatizo langu la mita limeisha, nawashukuru sana JF kwani baada ya kuwapa data zangu, waliniletea mita mpya, nimeondokana na tatizo la giza. Viva JF
 
Tatizo langu la mita limeisha, nawashukuru sana JF kwani baada ya kuwapa data zangu, waliniletea mita mpya, nimeondokana na tatizo la giza. Viva JF
Tunashukuru san mteja wetu ushirikano wako wa utoaji taarifa vema ndio umetusaidia kukuhudumia kwa haraka
 
Tanesco sasa hii ni kero kila siku mnakata Umeme Chanika nn shida au mpaka tuandamane mpaka kisarawe post..ndo mtupe majibu Maana hii sasa kero na watu wenu wa kisarawe wana majibi mabaya kweli
Namba yako ya simu tafadhal,eneo lako na je ulijibiwaje na ofisin namba ngapi hata PM unaweza kutupatia taarifa
 
Hivi tatizo la hili transfoma hapa eneo la Mwakibete mtaa wa Itongo na Nyibuko- Mbeya jiji halina ufumbuzi wa kudumu mara kwa mara tunalala giza sababu ha hilo transfoma hata sasa mo giza......
 
Hivi tatizo la hili transfoma hapa eneo la Mwakibete mtaa wa Itongo na Nyibuko- Mbeya jiji halina ufumbuzi wa kudumu mara kwa mara tunalala giza sababu ha hilo transfoma hata sasa mo giza......
Namba yakonya simu na namba ya taarifa tafadhali
 
TANESCO makao makuu mnafanya kazi moja nzuri sana humu,
Mimi baada ya kufanikisha mambo yangu kupitia ukurasa huu
Nimewaleta humu jamaa zangu wengi sana
Na ninayo furaha kusema na wao wamesikilizwa na kero zao zimeanza kufanyiwa kazi
Ushauri wangu kwenu,
TANESCO hivi sasa anzeni kuwaondosha wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea hawa ndio wanaotufanya sisi au wateja wenu kwa ujumla tukimbilie humu kuja kutoa kero zetu
Ila nyuma yetu wapo watanzania wengi sana wana kero zao nyingi sana na awana pa kukimbilia
Awana smartphone awajui namna ya kujiunga JF
Ombi langu
Nendeni mkapeleke huduma kama hii facebook au Twitter
Angalau muwe mnatatua kero kupitia hizo kurasa za FB na twitter kwa wiki mara 2
Binafsi kiongozi aliyebuni ukurasa huu wa kero nampa hongera sana kwa ubunifu huu
Shirika la TANESCO hivi sasa linapata heshima kubwa kupitia uzi huu.
Aksanteni sana.
Nimetuma maombi ya kuunganishiwa umeme (nikajaza fomu) na kuahidiwa kuunganishiwa umeme baada ya wiki moja sasa unakaribia mwezi wa 2 sijauganishiwa umeme tatizo nini kama nguzo imeshawekwa ?
 
Hivi gesi ya Mtwara ni ya kichina hadi umeme ndani ya masaa 24 tunapata masaa mawili nayo ni kwa mbinde na zile kauli za umeme kukatika Mtwara na lindi itakuwa historia zilitoka ili ashangaliwe
 
Hivi gesi ya Mtwara ni ya kichina hadi umeme ndani ya masaa 24 tunapata masaa mawili nayo ni kwa mbinde na zile kauli za umeme kukatika Mtwara na lindi itakuwa historia zilitoka ili ashangaliwe
Mtwara kuna mashine ilipata hitilafu hivyo kupelekea ukarabati mkubwa
 
TANESCO, waya unapokatwa na gari/roli nikaripoti ofisini, Je, ni sahihi mafundi kufika nyumba husika na kuondoka bila kurekebisha huku wakidai mpaka nilipeleke gari lililokata waya while silifahamu?

Ni gharama zipi mteja anapasika kuingia kwa tatizo kama hili?
 
Inapotokea hali kama hiyo hatua ya kwanza ni kuondoa hatari kazi ambayo inafanywa na kundi letu la dharura baada ya hapo kazi ya kurudishia hali ilivyokuwa mwanzo inafanywa na kundi lingine,

Je ni wilaya gani na namba yako ya simu, eno lako haswa
 
Nguzo moja inauzwa kiasi gani?
Na unapoinunua inakuwa ni mali yangu.
Nitoe ushauri kwa TANESCO mnapotaka kutumia nguzo kumunganishia mteja wenu kupitia nguzo mliyoiuza kwa mteja mwengine mtapaswa muilipie ili muweze kuitumia.
 
Inaonekana sahivi nyie tanesco mna mgao wa umeme wa kimya kimya bora Mseme tu wananchi tuelewe?

Ova
 
Back
Top Bottom