TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Huu mgao wa umeme vipi? Au gas imekata?
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia.

Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme.

Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.

TANESCO inawaomba ushirikiano na kuwa waangalifu wakati wa zoezi hili.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017
 
nina shauri namba za huduma za dharura ziwe niza bure hata usipo kuwa na vocha iwe rahisi kutoa au kupata taarifa
 
nina shauri namba za huduma za dharura ziwe niza bure hata usipo kuwa na vocha iwe rahisi kutoa au kupata taarifa
Tumetoa njia nyingi za bure kama facebook, twitter jamii forum na website kwa wewe kutupatia taarifa bure kabisa
 
Kuna nguzo zinakaribia kuleta janga page kwenye daraja linalounganisha Pwani na Dar, barabara ya Bagamoyo. Fanyeni hima.
 
Tanesco nimeomba kufanyiwa survey tangu nwezi Jana nikaambiwa nitafanyiwa baada ya wiki moja cha kushangaza ni mwezi sasa sijamuona huyo anayeitwa surveyor wenu
 
Tanesco nimeomba kufanyiwa survey tangu nwezi Jana nikaambiwa nitafanyiwa baada ya wiki moja cha kushangaza ni mwezi sasa sijamuona huyo anayeitwa surveyor wenu
Hili la surveyor kutokuja ni jipu nadhan linatoa mianya ya rushwa
 
Tanesco nimeomba kufanyiwa survey tangu nwezi Jana nikaambiwa nitafanyiwa baada ya wiki moja cha kushangaza ni mwezi sasa sijamuona huyo anayeitwa surveyor wenu
Jina... mkoa.. wilaya.. eneo.., namba ya simu tafadhali
 
Tanesco watu wa mwasonga tunahitaji umeme mda mrefu ila usambazaji una urasimu sana. Mna mpango gani?
 
Nyie jamaa ni wasanii sana, mi niliwahi kulipia nguzo ga Umeme matokeo Yake ilichukua miezi mitatu kasoro kuniwashia Umeme, na hayo yote mlikuwa mnatengeneza mazingira ya kushikwa miguu! Mnakera sana
 
Nguzo moja inauzwa kiasi gani?
Na unapoinunua inakuwa ni mali yangu.
Nitoe ushauri kwa TANESCO mnapotaka kutumia nguzo kumunganishia mteja wenu kupitia nguzo mliyoiuza kwa mteja mwengine mtapaswa muilipie ili muweze kuitumia.
Nguzo haiuzwi. Tanesco wanatoa huduma ya umeme na sio kuuza vifaa.

Hiyo nguzo, meter, waya vinabaki kuwa mali ya Tanesco na ndio maana hata nguzo ikioza hubadilishwa bila wewe kutoa kiasi chochote cha hela.

Ukitaka kuuziwa hivyo unavyodai umevinunua basi natumaini umeme ungeuona kwa akina Bakhresa tu watu wa hali ya chini wasingekuwa na uwezo wa kununua nguzo, waya na meter.

Hizo gharama unazolipa ni gharama nafuu za serikali ili kila mtu aweze kuwa na umeme
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA MAENDELEO KAZI YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa kazi ya kusafisha bomba kubwa la gesi imekamilika, sasa hivi mafundi wanaendelea na kazi ya kuunganisha Kituo cha Kinyerezi II.

Umeme umerejea katika baadhi ya maeneo.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

Tunawaomba radhi Wateja wetu wa maeneo ambayo bado yanayokosa umeme.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017
 
Ivi shinyanga mnatumia umeme wa vumbi....
Maana kila unapofika wakati wa mvua umeme ni kero....leo siku ya pili isaka hamna umeme
Eneo gani na namba yako ya simu,je ni weww mwenyewe
 
Malalamiko yangu nikuhusu hapa ninapo ishi Maeneo ya lolovono mkoani Arusha mjini ambayo upande wote tume zungukwa na umeme katika kitongoji chetu tuu ndio hakina Umeme mpaka mtu binafsi atokee kununuanguzo ndipo hapo huduma humfikia
SASA naiuliza TANESCO mradi bila biasha Biashara utaiyanzaje...tisaidieni kwa hilo tuna hitaji sana Umeme...
 
Ulipotoa taarifa ofisi ya eneo lako uliambiwaje?
 
Back
Top Bottom