TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Sitaki kujua kama ni kwa wote au ni Kigamboni pekee au Dar es salaam yote, kama ni huu mtaa wangu pekee au ni Kigamboni yote, but kiukweli hii service yenu inaboa kupitiliza. Tuambieni kama umeme tutakuwa tunapata kila siku kuanzia jioni saa 12 au saa moja hadi asubuhi saa tatu au saa nne na mseme kabisa kwamba hiyo ndio ratiba ya kudumu.

Nafkiri pengine viongozi mnaohusika au kusimamia kwa kuwa haukatiki majumbani mwenu au kwenye site zenu basi hamyaoni haya, mnatutia umaskini usio wa lazima vitu vinaozea kwenye majokofu kwa kushinda kutwa nzima bila umeme, kwani hamjui kuwa wengine biashara zao umeme ndio kila kitu na mnazifahamu mnataka ziwe zinafunguliwa jioni na kufungwa asubuhi?

Matengenezo gani kila siku hayaishi? Yani inafikia kipindi umeme ukirudi basi mtaa mzima unapiga yowe za shangwe na madebe kabisa as if wameona mvua ambayo ilikuwa imekata kwa miaka mitano, Hatakama kuna moja mbili tatu tangazeni basi tunashtukia tu umeme umekata, utafikiri ni kitu tunachopewa bure

Sasa kituko kingine kama leo umekatika saa nne umerudi saa nne nasu saa tano kasoro ukakatika tena mpaka saa moja jioni umerudi saa moja na nusu baada ya dk 10 ukakatika tena ukaja kurudi saa mbili tena, mtatuunguzia vitu nyie watu, maisha yenyewe yako wapi ya kununua vitu vya electronics mara mbili mbili na cha mwisho weekend ndo kabisa kuucha umeme bila kukata hamjisikii vizuri, sijui ina nini nanyie hiyo weekend.

Badilikeni Aisee kama wahusika mnapita humu na kuyaona haya yafanyieni kazi.
 
Kwa three phase unaweza kufika ofisi inayohudumia ujaze fomumili upewe access ya kuona online matumizi yako aidha unaweza kutupatia namba yakonya mita na ya simu tukujulishe hilo
0655048302

Namba ya mita 43146855093
Ndo hiyo.
 
Ukweli ni kwamba kuna mgao wa umeme ila Tanesco hamtaki kusema kweli, inakera, inaudhi na inauma umeme kuwa mafungu mafungu na joto hili la Dar.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA MAENDELEO KAZI YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa kazi ya kusafisha bomba kubwa la gesi imekamilika, sasa hivi mafundi wanaendelea na kazi ya kuunganisha Kituo cha Kinyerezi II.

Umeme umerejea katika baadhi ya maeneo.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

Tunawaomba radhi Wateja wetu wa maeneo ambayo bado yanayokosa umeme.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017
 
Sitaki kujua kama ni kwa wote au ni Kigamboni pekee au Dar es salaam yote, kama ni huu mtaa wangu pekee au ni Kigamboni yote, but kiukweli hii service yenu inaboa kupitiliza. Tuambieni kama umeme tutakuwa tunapata kila siku kuanzia jioni saa 12 au saa moja hadi asubuhi saa tatu au saa nne na mseme kabisa kwamba hiyo ndio ratiba ya kudumu.

Nafkiri pengine viongozi mnaohusika au kusimamia kwa kuwa haukatiki majumbani mwenu au kwenye site zenu basi hamyaoni haya, mnatutia umaskini usio wa lazima vitu vinaozea kwenye majokofu kwa kushinda kutwa nzima bila umeme, kwani hamjui kuwa wengine biashara zao umeme ndio kila kitu na mnazifahamu mnataka ziwe zinafunguliwa jioni na kufungwa asubuhi?

Matengenezo gani kila siku hayaishi? Yani inafikia kipindi umeme ukirudi basi mtaa mzima unapiga yowe za shangwe na madebe kabisa as if wameona mvua ambayo ilikuwa imekata kwa miaka mitano, Hatakama kuna moja mbili tatu tangazeni basi tunashtukia tu umeme umekata, utafikiri ni kitu tunachopewa bure

Sasa kituko kingine kama leo umekatika saa nne umerudi saa nne nasu saa tano kasoro ukakatika tena mpaka saa moja jioni umerudi saa moja na nusu baada ya dk 10 ukakatika tena ukaja kurudi saa mbili tena, mtatuunguzia vitu nyie watu, maisha yenyewe yako wapi ya kununua vitu vya electronics mara mbili mbili na cha mwisho weekend ndo kabisa kuucha umeme bila kukata hamjisikii vizuri, sijui ina nini nanyie hiyo weekend.

Badilikeni Aisee kama wahusika mnapita humu na kuyaona haya yafanyieni kazi.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA MAENDELEO KAZI YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa kazi ya kusafisha bomba kubwa la gesi imekamilika, sasa hivi mafundi wanaendelea na kazi ya kuunganisha Kituo cha Kinyerezi II.

Umeme umerejea katika baadhi ya maeneo.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

Tunawaomba radhi Wateja wetu wa maeneo ambayo bado yanayokosa umeme.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017
 
Tanesco kuna sehemu inaitwa mail 35 mbele ya misugusugu kibaha pwani nyumba zimeshakuwa nyingi ila huduma ya umeme hamna yaani watu wanaishia kununua visolar uchwara mnawasaidiaje wakazi wa hapo
 
Mtapatiwa huduma ya umeme pale mradi wetu utakapofika eneo hilo mpendwa mteja
 
Tumechoka na hiyo taarifa ndefu unaitoa kila wakati "MAFUNDI WAMEKAMILISHA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI" kwa mimi naomba isiitoe tena, mnairudia sana.

Tunataka taarifa itakayosema kuanzia saa tatu na nusu tutakata umeme mpaka saa kumi na mbili jioni ili tupange ratiba nyingine kama za kwenda beach kupunga upepo. Mmekata umeme dakika tano zilizopita, hakuna taarifa yoyote. TOA TAARIFA HAPA UMEME UTARUDI SAA NGAPI???
 
Kwatabia hii ya kukata kata umeme hovyo, ndo ya nchi yenye viwanda ya Mh. Rais, inafifia.

Umeme umefikia mahali unakatika hovyo bila hata tangazo. Tangazo linatolea tayari wameshakata umeme. Namna hii, uzalishaji unakua hauopo na gharama zinapanda.

Kwamfano, kutoa kopi, kwa umeme wa tanesco inakua 300 na umeme wa jenereta ni 500, hapa tayari gharama zinapanda. Huu ni mfano mdogo tuu jinsi gani kuta umeme hovyo kunavyo adhiri uzalishaji.

Basi kama kuna mgao, twambiwe ili sie malofa tujue tujipange vipi kuendesha maisha.

Hili shirika litafute mmbiya moja au wawili wasaidizane kuendesha hili shirika. Serekali inatoa hela nyingi kweli kuliendesha hili shirika, lakini jitihada zote za serekali ni kama ni bure.

Matatizo ya kukatika umeme yako palepale, nikama hela inayowekezwa hapo tanesco haina tija kabisa. Tumechoka wananchi kwa kweli. Viwanda kustawi nipamoja na kuwa na umeme wa uhakika, bila umeme viwanda zitabaki ndoto.
 
Kweli mkuu umevurugwa sana katika hili, kiasi naweza liona hilo katika uandishi wako.

Sema nini, ujumbe wako uwafikie hawa jamaa maana makatizo ya umeme kiukweli yamezidi sana, nadhani mojawapo ya vitu

vinavyokwamisha/vitakavyokwamisha maendeleo na uanzishwaji wa viwanda Tanzania ni Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika.
 
Maadam tunajiandaa kwa uchumi wa kati, ninaomba hili tatizo la kukatika ghafla umeme lichunguzwe kwa makini.

Mimi ni malala hoi nimechukua mkopo nikanunua vifaa vinavyotumia umeme, kukatikajatika kunaharibu vifaa vyangu, na mtu kama mimi ni kigezo katika kufikia uchumi wa kati.

Kama ni nnje ya uwezo wa Tanesco sawa lakini kama jipu litumbuliwe haraka. Kuwe na ushindani au Tanesco ibinafishwe.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA MAENDELEO KAZI YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa Wataalamu wetu wanaendelea na kazi ya kuunganisha Kituo cha Kinyerezi II usiku na mchana ili kuhakikisha umeme unarudi katika hali yake ya kawaida.

Kazi hii inatarajiwa kukamilika mapema siku ya Jumatatu Novemba 20, 2017.

Umeme umerejea katika baadhi ya maeneo.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

Tunawaomba radhi Wateja wetu wa maeneo ambayo bado yanayokosa umeme.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 19, 2017
 
Kweli mkuu umevurugwa sana katika hili, kiasi naweza liona hilo katika uandishi wako.
Sema nini, ujumbe wako uwafikie hawa jamaa maana makatizo ya umeme kiukweli yamezidi sana, nadhani mojawapo ya vitu vinavyokwamisha/vitakavyokwamisha maendeleo na uanzishwaji wa viwanda Tanzania ni Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA YA MAENDELEO KAZI YA KUSAFISHA NA KUUNGA BOMBA LA GESI - KINYEREZI I, MAANDALIZI YA KUUNGA KITUO CHA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa Wataalamu wetu wanaendelea na kazi ya kuunganisha Kituo cha Kinyerezi II usiku na mchana ili kuhakikisha umeme unarudi katika hali yake ya kawaida.

Kazi hii inatarajiwa kukamilika mapema siku ya Jumatatu Novemba 20, 2017.

Umeme umerejea katika baadhi ya maeneo.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi.

Tunawaomba radhi Wateja wetu wa maeneo ambayo bado yanayokosa umeme.

TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo.

Kwa mawasiliano
Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu
twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 19, 2017
 
Mtapatiwa huduma ya umeme pale mradi wetu utakapofika eneo hilo mpendwa mteja

Ni lini hii huduma yenu itafika hapa, na wakati mji wa mbele ya maili 35 una umeme? Pia ni lini na tutajuaje kuwa ndo mnaleta umeme. Au sisi wananchi tufanye nini ili mlete hii huduma kwa haraka hapa maana ni shida tupu
 
Miezi kadha wa kadha kumekuwa na kata-rudisha, kata-rudisha,....ya umeme utafikiri wanafurahia mchezo huo! Zoezi hilo limeanza pale tu alipojiuzulu Prof Muhongo na imekuwa ikitokea hivyo kila anapojiuzulu Prof Muhongo!m

Yaani inakera sana, umekaa tu kuandika kazi zako kwenye Computer mara paaap, wamekata. Unaenda kupunga upepo kidogo unarudi, unaanza kazi mara paaap wamekata, utafikiri wanakuona na hawataki utumie huo umeme!

Hivi ndio tuliambiwa tatizo la umeme litakuwa "Historia?" Au walimaanisha nini?

Hiyo Tanzania ya Viwanda (wengine huwa wanasema "vi-wonder") ni utani tu wa mkubwa au hao wawekezaji akina Dr Shika watakuja na umeme wao?

Na hiyo treni ya umeme, ni huu huu au itakuja na umeme wake?
Au hawa TANESCO walipoambiwa " Hapa Kazi tu" walifikiri ni kazi ya kukata na kurudisha umeme wakati wiwote ule wanavyotaka wao? Maana mara nyingine mnaletewa umeme saa tisa usiku, ikifika tu saa12 asubuhi unakatwa, huyo "mkata umeme" huwa hakosei, anaijua kazi yake barabara!

Inawezekana wamempa mafunzo ya kutosha!
Mkubwa anapotumbua sijui anamkwepa wapi "mkata umeme," tunajua asiyetumbilika nchi hii ni Bashite, baaaaasi! Au mwingine "mkata umeme" kaongezeka?
Mnakera sana nyie TANESCO!!!
 
TANESCO this is too much jamani jana tangu asubuhi mpaka sasa hakukua na umeme... leo pia kuanzia asubuhi mpaka muda huu. hii nchi ya viwanda inakujaje kweli??? wenye biashara zinategemea umeme wanaishije kwa hii kata umeme?

mtu unasema weekend upumzike nyumbani ukiamka tu hakuna umeme.Last weekend ilikua hivyo pia.. achana na siku za katikati ya week ambayo kwa upande wangu nakua katika mihangaiko ya maisha

INAKERA SAAANA
 
TANESCO this is too much jamani jana tangu asubuhi mpaka sasa hakukua na umeme... leo pia kuanzia asubuhi mpaka muda huu. hii nchi ya viwanda inakujaje kweli??? wenye biashara zinategemea umeme wanaishije kwa hii kata umeme?? mtu unasema weekend upumzike nyumbani ukiamka tu hakuna umeme.Last weekend ilikua hivyo pia.. achana na siku za katikati ya week ambayo kwa upande wangu nakua katika mihangaiko ya maisha

INAKERA SAAANA
Polee [emoji36]
 
Back
Top Bottom