TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mteja anapo omba kuwekewa umeme akiwa mbali na nyaya za kusambaza umeme, anatakiwa kulipia gharama ya kuwekewa nguzo. Maswali;

1. Kwa nini mteja alipie gharama za kununua, kusafirisha na kusimika nguzo?

2. Kwa nini kuwepo na sheria au kanuni ya kumlazimisha mteja ya kuandika barua kwa Taneco kukiri kwamba nguzo hizo ni mali ya Tanesco ili hali kanunua/kalipia gharama za kuwekwa nguzo hizo?

3. Iweje alipie nguzo na akipatikana mteja mwingine aliyepo karibu na eneo hilo afungiwe bure bila kuchangia gharama za kuwekwa nguzo?

4. Tanesco haioni kuwa kuna mkanganyiko wa makusudi kwa matakwa namba 2 na 3 hapo juu? Kama nguzo ni mali ya Tanesco kwa nini gharama zake zisiwe za Tanesco wenyewe? Ona namba sita chini kama pendekezo.

5. Je, Serikali, Bunge, Tanesco hawaoni kuwa kuna haja ya kurekebisha sheria kuondoa utata huo hapo juu??

6. Kwa vile nguzo ni mali ya Tanesco na mteja kalipia gharama za nguzo hizo, kwa nini mteja aliye omba na kulipia kuwekewa nguzo asirudishiwe fedha yake hata kama ni njia ya kulipana kupitia matumizi yake hadi atakapo maliza gharama za kuwekewa nguzo?
 
Mkuu tariff 4 ndo nini?na inawezekana vipi 9,500 upate units 73,wakati Mimi nanunua wa 20,000 napata units 56.

Habari kwa uwelewa wangu mdogo watu wa TANESCO watanisaidia kama ntakuwa nakosea.

tarrif 4 ni wateja wadogo wa umeme vijijini na wenye matumizi madogo ambao kama sikosei ni watumiaji wa umeme wenye unit chini ya 75 kwa mwezi ambapo wananunua umeme kwa shilingi 108 bila kodi za serikali na wkundi jingine ni tarrif 1 ambao hawa TANESCO wanaita watumiaji wa kawaida wa nyumbani ambao matumiz yao ni zaidi ya unit 75 kwa mwezi hawa wananunua unit moja shilingi 292 bila kodi za rea, vat na ewura
 
Mbona mimi tangu nimeanza kutumia umeme (mita mpya, ina miezi 6/7 sasa hivi) sijawahi kuzidisha units 70 kwa mwezi na bado nalipa 10,000/- napata units 28 tu?

Hio tarrif 4 inapatikanaje?
Mimi pia nina tatizo linalofanana na hili, niliingizwa mojakwamoja kwenye tariff 1 na mita ni mpya tangu mwez august mwaka jana nilipofungiwa umeme, naomba msaada kubadilishiwa tariff toka hiyo tariff 1 kwenda tariff 4 meter no. 54 1305 1107 1
 
Tanesco naomba muangalie mita yangu
inakula sana hela wakati navyotymia ni vichache

namba ya mita 24 2109 3432 9

Niko Rwamgasa-Geita
Mimi ilishawahi ni kuta mita ilikuwa inakula sana umeme, Fundi alivyokuja akabadilisha Earth loads (Chuma ya Earth) baada ya hapo mambo mukidii mukide
 
Naomba kuelewa au kujua ni kwa nini eneo la Chang'ombe Maduka mawili pamoja na maeneo yote ya jirani na hapo umeme unakatika katika mara kwa mara hususani siku za mwisho mwa juma.

Kiukweli tunanyanyasika sana na hiyo hali na hata tupigapo simu kutaka kujua tatizo ni nini, line zote zinawekwa busy mpaka umeme utakaporudi.
 
Naomba kuelewa au kujua ni kwa nini eneo la Chang'ombe Maduka mawili pamoja na maeneo yote ya jirani na hapo umeme unakatika katika mara kwa mara hususani siku za mwisho mwa juma. Kiukweli tunanyanyasika sana na hiyo hali na hata tupigapo simu kutaka kujua tatizo ni nini, line zote zinawekwa busy mpaka umeme utakaporudi.
Aiseee kumbe huwa wanaziweka line zao busy
 
Habari kwa uwelewa wangu mdogo watu wa TANESCO watanisaidia kama ntakuwa nakosea.
tarrif 4 ni wateja wadogo wa umeme vijijini na wenye matumizi madogo ambao kama sikosei ni watumiaji wa umeme wenye unit chini ya 75 kwa mwezi ambapo wananunua umeme kwa shilingi 108 bila kodi za serikali na wkundi jingine ni tarrif 1 ambao hawa TANESCO wanaita watumiaji wa kawaida wa nyumbani ambao matumiz yao ni zaidi ya unit 75 kwa mwezi hawa wananunua unit moja shilingi 292 bila kodi za rea, vat na ewura
Mimi nipo katika iyo tariffs iyo apo na umeme nanunua kwa Tshs 20,000 kwa Units 56.20. Kwa bei ya kila units Tshs 355.87
lakini apo tunawekwa katika tariffs ambayo ina pesa nyingi na wakati matumizi yangu ayazidi iyo 56.2 units kwa mwezi
 
Habari mkuu.
Mwaka jana wakati navuta umeme nilimuambia jirani yangu ambaye tupo karibu naye kuwa tuchange pesa kisha tununue nguzo mbili kisha iwe rahisi kuvuta umeme. Yeye alikataa katakata tena kwa kiburi.

Wiki iliyopia nimeona tanesco wamekuja kusurvey katika nguzo zangu wakiwa wanataka kumvutia umeme. Mimi nataka kuweka pingamizi kuwa na yeye atafute nguzo zake au atumie line ya mtaa wa nyuma ili avute umeme ila sitaki atumie nguzo zangu.

Naomba muongozo wako katika hili mkuu
 
Naomba kujua umeme wa units 56.2 kwa mwezi inakuwa ni tariffs ipi?
habari Come27 unit sio tarrif, tarrif ni matumizi yako, wateja wote wanaweza kununua unit 56.2 inapotafautishwa na tarrif ni bei ya manunuzi.
 
Mmekuwa mkilalamika kwamba mnaendesha shirika kwa hasara, mnajua kama kuna baadhi ya watumishi wa shirika hushiriki kulihujumu shirika kwa kushiriki wizi wa umeme?

Mfano pale Kibamba CCM DSM kuna mita moja ya umeme inahudumia zaidi ya nyumba 3 lakini malipo ya umeme kwa mwezi si zaidi ya shilingi 10,000.

Pale Igogo Mwanza Mtaa wa mchafukoga kuna mtu anatumia umeme bila mita na yeye kafungua tanesco yake anawasambazia watu umeme majumbani kwa malipo yasiyozidi 10,000 kwa mwezi, akishapokea malipo hayo na yeye anawagawia wezi wenzie pale TANESCO Igogo,wezi wote hao wawili niliowataka walikuwa watumishi wa shirika hilo hapo kabla.

Je mnayajua hayo?
 
Nimeomba saveaTanesco tangu tarehe 17.3. Mkoani Kilimanjaro cha ajabu mpaka leo savea hajafika! Nilikuwa likizo mpaka likizo lmekwisha hakuna kitu kila ukienda unaambiwa tunakuja!
 
Nimeomba saveaTanesco tangu tarehe 17.3. Mkoani Kilimanjaro cha ajabu mpaka leo savea hajafika! Nilikuwa likizo mpaka likizo lmekwisha hakuna kitu kila ukienda unaambiwa tunakuja!
Jiongeze mkuu!


Mimi ilibidi nimpooze surveyor maana alitaka kunikomoa kwa kuniandikia nguzo pasipohitajika.

RUSHWA haiwezi kuisha na ukifupisha mkono mambo yako yatachelewa sana au kukwama kabisa japo uanaona unastahili kuhudumiwa.
 
Mmekuwa mkilalamika kwamba mnaendesha shirika kwa hasara, mnajua kama kuna baadhi ya watumishi wa shirika hushiriki kulihujumu shirika kwa kushiriki wizi wa umeme? Mfano pale Kibamba CCM DSM kuna mita moja ya umeme inahudumia zaidi ya nyumba 3 lakini malipo ya umeme kwa mwezi si zaidi ya shilingi 10,000. Pale Igogo Mwanza Mtaa wa mchafukoga kuna mtu anatumia umeme bila mita na yeye kafungua tanesco yake anawasambazia watu umeme majumbani kwa malipo yasiyozidi 10,000 kwa mwezi,akishapokea malipo hayo na yeye anawagawia wezi wenzie pale TANESCO Igogo,wezi wote hao wawili niliowataka walikuwa watumishi wa shirika hilo hapo kabla. Je mnayajua hayo?
Tanesco. Tumieni taarifa toka kwa whistle blower. Na mjue jinsi ya kuwalinda watu kama hawa. Biggy pongezi kwa kuwa mzalendo
 
Back
Top Bottom