TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tukuelezee wapi zaidi mkuu
Umezungumzia tariff 1 mara mbili katika maelezo yako ya mwisho. Alafu matumizi ya units 75 mfululizo kwa miezi mitatu si bado nitabakia tariff 1? Je nikizidisha hapo napelekwa tariff gani na gharama kwa units moja nitakuwa nalipia kiasi gani mkuu?

Naomba kujua hizo gharama za manunuzi ya units kwa tariffs mbalimbali
 
upload_2017-5-3_8-45-19.png
 
Kuna nguzo iligongwa na gari ikakatika kabisa chini bahati nzuri iyo nguzo ilishikiliwa na waya inayoenda kwenye nyumba tatu(mfano wa T) kwahiyo haikudondoka lakini ilitokea shoti kubwa mpaka tanesco wakaja na wakasema watabadilisha hiyo nguzo (ilikuwa mwaka jana) lakini mpaka leo hawajabadilisha. Sasa sijui mpaka iangukie nyumba yangu iue watu ndio watakuja ama vipi.
MKOA: TANGA
WILAYA: TANGA
KATA : NGUVUMALI
MTAA: MWAMBONI
MITA YA NYUMBA ILIYO KARIBU NA HIYO NGUZO: 43000279844
 
  • Thanks
Reactions: ADK

NAMBA YAKO YA SIMU?
 
TANESCO ninawapongeza sana kwa hatua hii japo mumechelewa sana.
Ushauri wangu tu muelekeze nguvu zenu katika uboreshaji wa ukusanyaji madeni na kudhibiti wizi.

haingii akilini shirika linaulouza umeme Tanzania ni moja tu na Mahitaji ya umeme Tanzania ni makubwa halafu munejiendesha kwa hasara no way.

Hii inatokana na uzembe wenu huko nyuma wa ukusanyaji madeni ninaamini kulikua na udanganyifu mkubwa sana ndio maana ukiangalia wafamyakazi wengi wa Tanesco wa enzi hizo ni matajiri wa kutupa hasa wale waliokua wanasoma mita.

Tunaelewa Gharama za uzalishaji umeme zimekuwa kubwa kuliko mapato lakini jaribuni kuwekeza katika ufanisi wa ukusanyaji madeni na udhibiti wa wizi na mwisho wa siku matokeo mutayaona
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Mpendwa mtejaTunaomba namba yako ya simu hata kwa private mesage ili tuweze kushirikiana nawewe kubaina tuhuma hizo nzito ulizotupatia.Tunashukuru san kwa taarifa hizi muhimu
Niwape namba zangu za simu ili mnihujumu na kunisabanishia matatizo..!! Namba siwapi ila fanyeni uchunguzi ktk maeneo niliyoyataja nikiwaongezea na eneo lingine la Sahara kule Mwanza
 
hapa tunawasiliana na nani maana MIMI NAUDUMIWA TANESCO MAGOMENI NILIRIPOTI NGUZO KUKTIKA TOKA TRH 24/ 5/ 17 NIKAPEWA TB NO 3476 WAKELETA NGUZO TRH 26 wakachimba KULIKUWA HAMNA MVUA HADI LEO NGUZO HAIJABADILISHWA VIFAA WAMEACHA NYUMBA YA JIRANI NGUZO IPO TU HAPA NIMEPIGA CM EMEGENCE WAKADAI ET NIENDE NO 6 WAO NDO WATAJUA NINI SABABU NIMETUMA VIDEO TWEETER HAKUPATA MSAADA HUU NI UZEMBE MKUBWA TATIZO HILI LIPO TANDALE CHAMA NJIA YA KUELEKEA KWA MANJUNJU NGUZU INANINGINIA IMESHIKILIWA NA WAYA ZILIZOPELEKA UMEME NYUMBA YA JIRANI NO 0657 424445
 
Kwenye nguzo zenu kuna shoti nyumba kama mbili hazina umeme tukiwapigia mnasema mko bize sababu hizi mvua shoti kila sehemu mara mnasema mnakuja hamji tuelewe lipi tunataka umeme.

Tuko Mburahati
 
Maeneo ya Kiluvya gogoni/ hondogo ktk Kata Ya Kibamba wilaya ya Ubungo Umeme hauna nguvu, watumiaji Wa Umeme wameongezeka lkn transformer bado chache hivyo nguvu ya Umeme kupungua.

Tunahitaji Umeme wenye nguvu ili wananchi wenye Machine ziweze kufanya kazi vizuri.
 
Tanesco mtaanza lini kutufungia umeme sisi tuliolipia umeme tangu January? Niko kwembe ubungo Dar es salaam
 
Tanesco mnatakiwa kujirekebisha kwa kweli! Mm nimelipia gharama ya kufungiwa umeme nyumbani kwangu tangu december mwaka jana hadi leo hii kila nikienda ofisini kwenu napigwa kiswahili tu kuwa nguzo hakuna na wanahudumiwa watu wa miezi ya nyuma kwanza...eneo langu linahitaji nguzo mbili
 
Nimepewa karatasi ya kwenda kulipia bank kwa ajili ya kuunganishwa huu mwezi wa tatu sijaenda kulipa( hali ya maisha imekuwa ngumu), je nitapigwa penati?
 
Nimepewa karatasi ya kwenda kulipia bank kwa ajili ya kuunganishwa huu mwezi wa tatu sijaenda kulipa( hali ya maisha imekuwa ngumu), je nitapigwa penati?
Sidhani kama kuna penati kama siyo deni mkuu
 
Back
Top Bottom