TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mnampango gani katika kuongeza matumizi ya personal luku ili kupunguza kero kwa watanzania wanaoshare luku?
 
Huku Masasi kwa siku umeme unaweza kukatwa na kurudishwa hata mara 10 kwa siku tatizo ni nini?
unatusababishia hasara kubwa sana.
 
Tunaomba namba ya taarifa uliyopewa ipo kwenye hicho kikaratasi ulichopewa imaeanza na Tb... Kst 052017-.......
Nmb ya kikaratasi ni 2259 niliyopewa, eneo ni magomeni mtaa wa ndugumbi karibu na msikitini nyumba ya ghorofa Ina frame mbili za maduka
 
Nmb ya kikaratasi ni 2259 niliyopewa, eneo ni magomeni mtaa wa ndugumbi karibu na msikitini nyumba ya ghorofa Ina frame mbili za maduka
Ulichoulizwa kingine na ukichojibu kingine. Taja hiyo namba inayoanza na hizo namba ulizopewa. Sasa hayo ya karibu na mataa nani kakuuliza?
 
Mnampango gani katika kuongeza matumizi ya personal luku ili kupunguza kero kwa watanzania wanaoshare luku?
Mpango upo na shirika linatoa huduma hio lakni kwa sasa tumejikita kutoa huduma kwa wateja ambao hawana kabsa umeme na baada ya kupunguza wale ambao wamelipia ndio tunaendelea na kuwafungia wateja mita ya pili
 
Jamani hapa mail 35,kabla hujafika visiga mji umekuwa sana lakini Nyumba zipo gizani, shida kubwa ni kuwa wananchi wengi wanaokaa hapo ni wa kipato cha chini sana ila wanatamani kuwa na umeme je mnawasaidiaje hao wananchi,maana ni tabu balaaa
 
Challe maige mita 24214220774 Kama ni manunuzi inanitia wasiwasi, Mimi nimeingia kwenye matumizi hayo muezi uliopita. Tare' 9/5/2017 nimenunu umeme wa sh 10000 nikapata unit 77 je nitatolewa? Naomba ufafanuzi
 
Utatolewa endapo wastani kwa miezi mitatu utazidi unit 75
 
Challe maige mita 24214220774 Kama ni manunuzi inanitia wasiwasi, Mimi nimeingia kwenye matumizi hayo muezi uliopita. Tare' 9/5/2017 nimenunu umeme wa sh 10000 nikapata unit 77 je nitatolewa? Naomba ufafanuzi
Ngoja tuangalia kwenye mfumo alafu tutakupa majibu
 
Tanesco hapa pongwe toka jumatatu umeme umekatika. Taarifa zinadai kuwa kuna watu waliiba nyaya za shaba kwenye transfoma.

Ajabu mpaka leo tupo kizani na mvua hizi. Nasikia mnadai mpaka tuwataje wezi. Hebu toeni ufafanuzi tuwaelewe.
 
Tanesco hapa pongwe toka jumatatu umeme umekatika. Taarifa zinadai kuwa kuna watu waliiba nyaya za shaba kwenye transfoma. Ajabu mpaka leo tupo kizani na mvua hizi. Nasikia mnadai mpaka tuwataje wezi. Hebu toeni ufafanuzi tuwaelewe.
Tunalifuatilia...
 
Tanesco mnazingua sana nimelipia umeme mnifungie ila week ya pili hii hamuonekani.. mnataka nikae giza mpaka lini!!??
 
Nimelipia kuunganishiwa (three phase-Dar es Salaam) umeme toka tarehe 18/4/ 2017 mpaka leo sioni dalili yoyote. Siku 30 za kusubiri zinatoa mwanya kwa mtu kupita mlango mwingine. Badilikeni, punguza hizo siku.

Kama mteja haitaji nguzo siku saba zinatosha kumpa umeme.
 
Tanesco hapa pongwe toka jumatatu umeme umekatika. Taarifa zinadai kuwa kuna watu waliiba nyaya za shaba kwenye transfoma. Ajabu mpaka leo tupo kizani na mvua hizi. Nasikia mnadai mpaka tuwataje wezi. Hebu toeni ufafanuzi tuwaelewe.
Leo tulifanya kikao na madiwani na kuwaomba watusaidie katika ulinzi wa hio transfoma kwa sababu imeibiwa Mara kadhaa hapo.

Tunafuatilia kwa sababu ipo maeneo ya biashara za watu yaani maduka. Pia changamoto ya mvua ilikuwa tatizo kubwa lakni kwa sasa mafundi wapo eneo hilo kuhakikisha huduma inarejea kwa wakati
 
Back
Top Bottom