TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
jamani naomba kujua mwezi wa sita nimenunua umeme wa tsh.9500 nilipewa units 75 mwezi huu nimeshindwa kuelewa kabisa tarehe moja nimenunua pesa ileile tsh.9500 nikapewa units 26 naomba kuelewa tatizo ni nini niko Kagera Biharamulo
Itakuwa umehamishwa tariff kutoka Kwenye matumizi madogo kwenda makubwa.

Subiri utaeleweshwa vizuri zaidi mkuu
 
jamani naomba kujua mwezi wa sita nimenunua umeme wa tsh.9500 nilipewa units 75 mwezi huu nimeshindwa kuelewa kabisa tarehe moja nimenunua pesa ileile tsh.9500 nikapewa units 26 naomba kuelewa tatizo ni nini niko Kagera Biharamulo
Umebadilishwa kundi la magumizi kutoka tarif 4 kwenda tarif 1 hivyo tupatie namba yako ya mita tukushauri zaidi

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
MNATUMA NAFASI ZA FIELD VYUONI
HALAFU TUKIJA MNATUAMBIA NAFASI HAZIPO.... MFANO MBEYA UNIVERSITY MLILETA NAFASI ZA WATU WA MECHANICAL ENGINEETING MMECHUKUA WAWILI TU KATI YA SABA
 
HUWA MNALETA ZA NINI HIZO NAFASI WAKATI MNAJUA MNAHITAJI WATU KADHAA ...HUO NI UBABAISHAJI
 
Nipo Morogoro
MSAADA: Nimehamia nyumba ambayo inajitegemea mita, lakini kwa 5000 napata units 13 tu, kama naweza pata msaada wa kuirudisha mita yangu kwenye matumizi ya kawaida, maana matumizi yangu ni madogo sana kwa mwezi,. number yangu ya mita 22132674049
 
MNATUMA NAFASI ZA FIELD VYUONI
HALAFU TUKIJA MNATUAMBIA NAFASI HAZIPO.... MFANO MBEYA UNIVERSITY MLILETA NAFASI ZA WATU WA MECHANICAL ENGINEETING MMECHUKUA WAWILI TU KATI YA SABA
Nafasi za nafasi kwa mafunzo kwa vitendo zinatolewa nyingi sana lakini lazima pawe na ukomo wa idadi ya wanafunzo tutaowachukua.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Nafasi za nafasi kwa mafunzo kwa vitendo zinatolewa nyingi sana lakini lazima pawe na ukomo wa idadi ya wanafunzo tutaowachukua.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
NINYI HAMFAHAM IDADI YA WANAFUNZI MNAOWAHITAJI KATIKA BRANCH ZENU KABLA YA KUTOA NAFASI..... KUNA WANAFUNZI WAMEKUJA DAR ES SALAAM WAKIJUA WANAKUJA KUFANYA FIELD TANESCO HUKO DAR LAKIN WAMEFIKA HUKO KUTOKA MBEYA UNIVERSITY WANAAMBIWA HAKUNA NAFASI NA NAFASI MLILETA WENYEWE MNAHITAJI WATU KADHAA.... SASA MNALETA NAFASI ZA KUHITAJI WANAFUNZI LAKINI WAKIFIKA HUKO UBUNGO MNASEMA ZIMEJAA ZIMEJAZWA NA NANI SASA ...MTU KATUMIA NAULI ,AMEKUJA KWA NDUGU HALAF MNAMWAMBIA KIRAHIS NAFASI HAKUNA, SASA MTU UNAJIULIZA WAMELETA WENYEWE WANATAKA WATU KADHAA KUTOKA MUST SASA INAKUAJE NAFASI ZIMEJAA ALIEJAZA NAFASI NI NANI?
.......
 
Tafadhali wasilisha lalamiko lako kwa meneja muandamizi rasilimali watu ,TANESCO Makao Makuu, S.l.p 9024 Dar es Salaam

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Tafadhali wasilisha lalamiko lako kwa meneja muandamizi rasilimali watu ,TANESCO Makao Makuu, S.l.p 9024 Dar es Salaam

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
wewe muwasilishie lalamiko si umelisoma
ili tuokoe muda ...
 
Huku kwetu kituo cha mbagara charambe kuna usumbufu kweli hasa kwa wateja wapya kufungiwa umeme. Tunalipia 520,000 pamoja na nguzo unakaa miezi 6 bado ujaunganishiwa kilaukifuatilia wanakwambia nguzo hamna.

Sasa hii shida inajenga kabisa mazingira ya rushwa kwani kuna watu wanafanikiwa ndani ya muda mdogo sie walala hoi tunapigwa kalenda INAUMA SANA ILA CHA KUFANYA NDO HAMNA.
 
wewe muwasilishie lalamiko si umelisoma
ili tuokoe muda ...
Ungetupatia taarifa kamili ya majina ya waliomba,walichojibiwa,nafasi walizoomba na mawasiliano yako tungewasilisha kitengo chetu cha Hr kwa hatua zaidi.

Pamoja na hayo bado msimamo utabaki pale pale kuwa sio wote watakaomba kufanya field watapata kwa kuwa kila nafasi inahitaji watu idadi fulani

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Huku kwetu kituo cha mbagara charambe kuna usumbufu kweli hasa kwa wateja wapya kufungiwa umeme. Tunalipia 520,000 pamoja na nguzo unakaa miezi 6 bado ujaunganishiwa kilaukifuatilia wanakwambia nguzo hamna. Sasa hii shida inajenga kabisa mazingira ya rushwa kwani kuna watu wanafanikiwa ndani ya muda mdogo sie walala hoi tunapigwa kalenda INAUMA SANA ILA CHA KUFANYA NDO HAMNA.
Umelipia kiasi gani kwa jina gani na namba yako ya simu tafadhali

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Huku kwetu kituo cha mbagara charambe kuna usumbufu kweli hasa kwa wateja wapya kufungiwa umeme. Tunalipia 520,000 pamoja na nguzo unakaa miezi 6 bado ujaunganishiwa kilaukifuatilia wanakwambia nguzo hamna. Sasa hii shida inajenga kabisa mazingira ya rushwa kwani kuna watu wanafanikiwa ndani ya muda mdogo sie walala hoi tunapigwa kalenda INAUMA SANA ILA CHA KUFANYA NDO HAMNA.
Mkuu umelipia mwezi gani. Utaratibu ambao upo tunafuata mtiririko wa kwanza kulipia wa kwanza kufungiwa. Kama kuna mtu unamfahamu amefungiwa mbele yako tutaomba ushirikiano wako lakni pia kuna wimbi la vishoka ambao wapo tayari kuwatapeli wateja hivyo epuka sana kutoa hela

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Nahitaji msaada wa kuwekewa umeme. Wiring imefanyika 2015,shule niliyopo ina umeme lakin nyumba za walimu hakuna na ni eneo moja, tumejaribu kuomba msaada lakin bado. Tanga, wilaya Mkinga

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
tanesco tbr inampango gani kusambaza umeme maeneo ya mail tano.

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Nahitaji mnieleweshe kuhsu tariff 1 na tariff 4.....
Tarrif 1 ni wateja wa majumbani ambao matumizi yao ni kati ya unit 75 hadi 7500 kwa mwezi ambapo bei ya unit moja ni shillingi 292 bila kodi za serikali ambazo ni Vat, Rea na Ewura

Tarrif 4 ni wateja wadogo sana ambao wengi wao wanapatikana vijijini ambao matumizi yao ni chini ya unit 75 kwa mwezi ambapo wananunua umeme kwa shilingi 100 bilamkodi za serikali.

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Nahitaji msaada wa kuwekewa umeme. Wiring imefanyika 2015,shule niliyopo ina umeme lakin nyumba za walimu hakuna na ni eneo moja, tumejaribu kuomba msaada lakin bado. Tanga, wilaya Mkinga

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
Chukua fomu ya maombi ya awali katika ofisi ya TANESCO iliopo karibu na wewe ni bureee

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Kutopatiwa umeme kijiji cha Mwaholo kata ya Kanyelele,tarafa ya usagala,wilaya ya misungwi

Sent from my HUAWEI RIO-L01 using JamiiForums mobile app
 
Tarrif 1 ni wateja wa majumbani ambao matumizi yao ni kati ya unit 75 hadi 7500 kwa mwezi ambapo bei ya unit moja ni shillingi 292 bila kodi za serikali ambazo ni Vat, Rea na Ewura

Tarrif 4 ni wateja wadogo sana ambao wengi wao wanapatikana vijijini ambao matumizi yao ni chini ya unit 75 kwa mwezi ambapo wananunua umeme kwa shilingi 100 bilamkodi za serikali.

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Mm nipo mjin na matumizi yangu kwa mwezi hayafiki unit 75,
Je naweza kufungiwa kwenye system ya tarrif 4?
 
Back
Top Bottom