TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Jamani tanesco chondechonde nisaidien kuppata umeme THIS IS UNBEARABLE
 
Mimi ni mkazi wa Kimara Dar, niliunganishiwa umeme tangu mwaka 2004, bahati nzuri ni kwamba nilikuwa nalipa bill zote kama kawaida pale ofisi ya Tanesco magomeni, mwaka 2012 nilifungiwa mita ya luku, nikiwa sina deni lolote.

Juzi nilinunua umeme wa sh 5000 nikapata unit 7, nikaenda mbezi Tanesco kuulizia kulikoni? nikaambiwa kuwa eti nadaiwa deni la tangu sijafungiwa luku.

Bahati nzuri kumbukumbu huwa haiozi nikarudi nyumbani nikachukua risiti zangu zote za mita ya zamani, kufika Tanesco wananiambia kuwa kweli risiti zinaonyesha nimelipa lakini msoma mita wao alikuwa anasoma kimakosa kwa hiyo hilo deni la sh 500000 (laki tano) ni lazima nililipe je nawauliza Tanesco hii ni sawa?

Nimekaa na kutafakari sijapata jibu sahihi wadau naombeni ushauri wenu.
 
Mimi ni mkazi wa Kimara Dar, niliunganishiwa umeme tangu mwaka 2004, na nilikuwa nalipa bila zangu za umeme pale Tanesco magomeni bila shaka yoyote. mwaka 2012 nilifungiwa mita ya luku, sasa mchezo umeanza juzi nilinunua umeme wa sh 5000 nikapata unit 7 nikawapigia customer care wa Tanesco Mbezi wakaniambia niende ofisini kwao kufika wakaniambia nadaiwa sh 500000 (laki tano) tangu wakati natumia mita ya kawaida.

bahati nzuri risiti zote za malipo ninazo kuawpelekea na wao kuziona mchezo ukabadilika wakasema, kweli risiti zangu ni sahihi lakini msoma mita wao alikuwa anakosea kusoma mita, nikawauliza kosa langu liko wapi?

wanasema maadam deni limeshaandikwa lazi nilipe. wadau wote pamoja na nyie wakubwa wa Tanesco najua mnapitia humu nifanyeje?
 
TANESCO tunakusubiri huku hatukuoni tunaomba majibu ya maswali yetu asante.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mkazi wa Kimara Dar, niliunganishiwa umeme tangu mwaka 2004, bahati nzuri ni kwamba nilikuwa nalipa bill zote kama kawaida pale ofisi ya Tanesco magomeni, mwaka 2012 nilifungiwa mita ya luku, nikiwa sina deni lolote. Juzi nilinunua umeme wa sh 5000 nikapata unit 7, nikaenda mbezi Tanesco kuulizia kulikoni? nikaambiwa kuwa eti nadaiwa deni la tangu sijafungiwa luku. Bahati nzuri kumbukumbu huwa haiozi nikarudi nyumbani nikachukua risiti zangu zote za mita ya zamani, kufika Tanesco wananiambia kuwa kweli risiti zinaonyesha nimelipa lakini msoma mita wao alikuwa anasoma kimakosa kwa hiyo hilo deni la sh 500000 (laki tano) ni lazima nililipe je nawauliza Tanesco hii ni sawa? Nimekaa na kutafakari sijapata jibu sahihi wadau naombeni ushauri wenu.
Tunaomba namba yako ya mita na namba ya simu tulifatilia na kukujulisha mpendwa mteja

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Tanesco mkoani kilimanjaro ni lini mtatuletea umeme wakazi wa kijiji cha shabaha kata ya mabogini ni karibu miaka mitatu sasa tunapigwa dana dana tu kijiji kina wakazi zaidi ya elfu moja.

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app

Kijiji kipo wilaya gani na namba yako ya simu tafadhali

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Moshi vijijini

Post sent using JamiiForums mobile app
 
kwa nini umeme unakatika mara kwa mara ktk maeneo mengi ya dsm haswa ktk wilaya ya ubungo kata ya kibamba?

naona hili shirika bora libinafsishwe maana limeshindwa kutatua kero za wananchi, kwa mwendo huu kweli tunaweza kuendesha viwanda??

hebu acheni kufanya kazi kimazoea badilikeni!!!
 
kwa nini umeme unakatika mara kwa mara ktk maeneo mengi ya dsm haswa ktk wilaya ya ubungo kata ya kibamba??
naona hili shirika bora libinafsishwe maana limeshindwa kutatua kero za wananchi, kwa mwendo huu kweli tunaweza kuendesha viwanda??

hebu acheni kufanya kazi kimazoea badilikeni!!!
Mpendwa mteja
Umeme upo vizuri maeneo yote ya jiji.tafadhali kama unatatizo la eneo lako au makazi yako tupatie namba yako ya simu na eneo lako wataalamu wetu wakufikie

Post sent using JamiiForums mobile app
 
TANESCO hongereni kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya,kwa kweli siku hizi mnatia raha!
NAOMBA mnijulishe matumizi yangu ya meter kama ninastahili kuwa T4

01343377394
 
TANESCO hongereni kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya,kwa kweli siku hizi mnatia raha!
NAOMBA mnijulishe matumizi yangu ya meter kama ninastahili kuwa T4

01343377394
Hahahaaa ukiwasifia kama hivi utapata majibu haraka sana lakini ukiuliza swali bila kuwasifia majibu utasubiri sana.[emoji24][emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maeneoo ya kongowe mwandege ifikapo saa 1:00 usiku takirba Siku tatu mnazima umeme bila ya tariha kuwa ka SAA 6:00 au 7:00 usiku kama siku tatu mfululizo Jana kuamkia leo alafu unasema upo vizuri. Vizuri gani

Sent using Jamii Forums mobile app
TUNAOMBA TAARIFA ZIFUATAZO MPENDWA MTEJA

MKOA.......

WILAYA...

MTAA AU KIJIJI....

NAMBA YA SIMU....


Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom