SIM
JF-Expert Member
- Oct 25, 2011
- 1,795
- 1,304
Yaani hili shirika wanafanya kazi kimazoea sana, unaweza mkata mtu makofi eti. hapo utakuta umepewa majibu mepesi mepesi tu huku jamaa anabinya binya kismart phone chake yupo facebook[emoji24][emoji24]Inasikitisha kuwa pale mnapotaka kutimiza matakwa yenu basi mko radhi kudanganya ili yenu yatimie. Siku ya Ijumaa walikuja watu wa Tanesco ofisini kwangu Pugu Road kwa madai ya kuwa wanabadili meter za zamani kuweka mpya. Ni jambo jema na nilitoa ushirikiano. Eneo langu lina meter 3 zote za 3 phrase maana ni industrial area.
Niliuliza mara mbili mbili juu ya upatikanaji wa units baada ya kubadili na nikahakikishiwa na Mtu wa Tanesco (Jerome - 0712 830 930) kuwa Jumamosi nitaweza kununua units na Jumatatu nitaweza kuclaim units zangu (Kila meter ilikuwa na si chini ya units 2000).
Cha ajabu Jumamosi kwenda ofisi zote za Tanesco naambiwa hizo meter mpya hazipo kwenye system bado. Hii inamaanisha toka Jumamosi nalazimika kutumia Generator (si chini ya laki 6 kwa siku). Leo hii Jumatatu naambiwa yale yale kuwa siwezi kununua umeme maana sijasajiliwa.
Kosa langu ni kukubali kubadilishiwa meter ambapo kumepelekea kuingia gharama zaidi? Kwanini nidanganywe kuwa nitaweza kununua umeme siku ya pili tu ilhali si kweli? Je hizi gharama za uendashaji kwa kutumia generator kwa kosa ambalo si langu ni za haki? Kuweni wa kweli kuzingatia na hali halisi ya kiuchumi. Mpaka dakika hii bado naendesha kazi kwa generator.
Number za meter mpya zilizobadilishwa ni
43153681812
43153688411
43153692736
Naushad
Royal Furnishers
0658427994
TANESCO
Sent using Jamii Forums mobile app