TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
natamani apatikane waziri atakayeligawa shirika pawepo na shirika la uzalishaji umeme, usambazaji na mauzo ya umeme na si matamko ya kisiasa.

umeme ni Shida unakatwa DSM wajibika basi,
 
Wamebaki kukaririsha watu tu megawatts, Kilowatt na hakuna kitu kinachopatikana...
 
Yaani tanesco utadhani wananikomoa Mimi, vyuma vimekaza vby, nimewahi kurudi home ili nipoteze muda kwa kuangalia Mpira, lkn toka nimefika home umeme haupo! Cjui nitoke nikakope pombe!

Yaani wamnionea sana!
 
Serikali yenyewe mbovu sasa unategemea taasisi zake zitakuwa imara kwenye utendaji? Angalia Takukuru na taasisi nyingine mbali mbali zote ni hovyo hovyo tu.

Na Serikali ndiyo chanzo cha utendaji mbovu wa taasisi hizi kwa kuingilia maamuzi yao mbali mbali na kutaka wafanye vile itakavyo Serikali.

Yaani kama kuna shirika ambalo wakisema livunjwe hata leo nitashangilia ni Tanesco!
Mtu hata kama umeamua kupumzika na kumalizia weekend nyumbani watakulazisha tu utoke, imagine weekend kama hii unaangalia mpira man utd vs brighton huku unasubiria liverpool vs chelsea jamaa wanakata umeme? Mnasababisha twende bar bila kupenda na vyuma vimekaza!
Kazi mnayoweza tanesco ni kukata umeme tu.
Kwanza nilisikia waziri mpya kasema umeme kukatika ni marufuku...vipi mbona ndio anachochea umeme kukatika?!
Hamna shirika nalichukia kama Tanesco maanake hawapitishi siku bila kuniharibia siku!
 
Watu mnapenda tu kulalamika.

Sidhani Tanesco wanaweza kukata umeme maksudi ili tu watu wasiwe na umeme. Kazi yao ni kuuza umeme, bila kuuza maana yake hawawezi kupata pesa. Sitaki kuamini kama wao ni mataahira hawataki kupata pesa.

Katika sayansi ya umeme, umeme ukikatika ni hasara kwao, maana ukikatika na kule unazalishwa na huku hautumiki ni hasara maana umeme huwezi kusema ambao haujatumika unaweza kuuhifadhi uutumie baadae.

Wanakata umeme kwa sababu kuna shida au hatari inatakiwa iondolewe, pia inawezekana pia mti umeangukia nguzo ya tanesco, umeme unasense hatari unakatika wenyewe, kuna madereva wazembe wanaweza kugonga nguzo ikavunjika umeme lazima utakatika, nk nk.

Binafsi siamini kua wafanyakazi wa Tanesco wanaweza kukata umeme kwa kua tu wamejisikia kukata umeme. Tusisahau pia na wao wanatumia umeme huo huo, ni taahira tu anaweza kukata umeme ambao hata yeye anautumia.
 
Serikali yenyewe mbovu sasa unategemea taasisi zake zitakuwa imara kwenye utendaji? Angalia Takukuru na taasisi nyingine mbali mbali zote ni hovyo hovyo tu.

Na Serikali ndiyo chanzo cha utendaji mbovu wa taasisi hizi kwa kuingilia maamuzi yao mbali mbali na kutaka wafanye vile itakavyo Serikali.
I was impressed na UHAMIAJI. Nimefanya taratibu za ku-renew passport baada ya kujaza form na kukamilisha taratibu zote nimeenda pale saa mbili na nusu hadi saa nne nimekamilisha taratibu zote bila kutumia mtu au kishoka! Nasubiria tarehe waliyoniambia nikachukue.
 
Ni moja ya mashirika ya umma ovyo kuwahi kuwepo Tanzania. Sijui shida yao nini, monopoly could be, ila ni shirika ovyo sana, hawawezi kwenda na kasi ya dunia kwa sasa, if possible serikali iruhusu kuzalishwa na kusambazwa umeme kwa kampuni binafsi.
 
Moderator unafikiri hii thread ya Tanesco hatuioni? Humu ni sawa na vile visanduku vya maoni kwenye ofisi za serikali, unaweka maoni kuhusu hio ofisi anaefungua na kuyasoma anakuta yanamhusu unafikiri yatafanyiwa kazi?
Msipende kuunganisha thread hovyo hovyo
 
Huku Tandahimba umeme tangu ulipokatwa jana saa saba mchana mpaka muda huu haujerejea na hatujui tu watarudisha lini !!
 
Huko nako madudu kedekede naona ulikuwa na bahati ya mtende. Usisahau wahamiaji haramu kibao nchini wanaoongozwa na Chinese na hiyo idara kazi ya kudhibiti wahamiaji haramu imewashinda.

I was impressed na UHAMIAJI. Nimefanya taratibu za ku-renew passport baada ya kujaza form na kukamilisha taratibu zote nimeenda pale saa mbili na nusu hadi saa nne nimekamilisha taratibu zote bila kutumia mtu au kishoka! Nasubiria tarehe waliyoniambia nikachukue.
 
Watu mnapenda tu kulalamika.

Sidhani Tanesco wanaweza kukata umeme maksudi ili tu watu wasiwe na umeme. Kazi yao ni kuuza umeme, bila kuuza maana yake hawawezi kupata pesa. Sitaki kuamini kama wao ni mataahira hawataki kupata pesa.

Katika sayansi ya umeme, umeme ukikatika ni hasara kwao, maana ukikatika na kule unazalishwa na huku hautumiki ni hasara maana umeme huwezi kusema ambao haujatumika unaweza kuuhifadhi uutumie baadae.

Wanakata umeme kwa sababu kuna shida au hatari inatakiwa iondolewe, pia inawezekana pia mti umeangukia nguzo ya tanesco, umeme unasense hatari unakatika wenyewe, kuna madereva wazembe wanaweza kugonga nguzo ikavunjika umeme lazima utakatika, nk nk.

Binafsi siamini kua wafanyakazi wa Tanesco wanaweza kukata umeme kwa kua tu wamejisikia kukata umeme. Tusisahau pia na wao wanatumia umeme huo huo, ni taahira tu anaweza kukata umeme ambao hata yeye anautumia.
Hivi umekwisha wahi kuona TANESCO wakifanya kazi zao? Kiufupi wapo mafundi ambao ni ovyo kabisa!

Unakuta wamefika sehemu ya tukio na gari yao wanaangaliaa, kisha wataenda kwenye transformer kukata umeme na wakikata tu, ndio basi itachukua muda kurudi tena kwenye tukio kurekebisha.

Hawa TANESCO mafundi wao ndio tatizo.
 
Huko Tandahimba hakufai, nilikuwa huko week mbili zilizopita aise huu mgao wa kisasa ni aibu, tatizo serikali haitaki kukubali ukweli inaleta siasa tu.
 
Sisi kwetu igunga umekua ni kama kawaida wanakata vile watakavyo sijui serikali imekuwaje mkufuli na majipu sijui halioni jipu hili
 
sasa imekua kama desturi tanesco kyela kukata umeme kila hasubuhi na kurejesha sa tano usiku..hili tatzo lilianza toka mwezi wa tisa hapo umeme ulikua unakatika kwa muda unarudi.... Lakini sasa unakatika kabisa na kurejesha sa tano usiku...

Mbaya zaidi hatuambiwi tatzo ni nn na hali hii itatengamaa lini maana shughuli nyingi za kijamii zimesimama na tulio wengi tunategemea umeme kupata kipato.. MBUNGE WETU MWAKYEMBE NDIO HAMNA KITU WALA HASEMEI JAMBO HILI WALAU KUTUPOZA SISI WAPIGA KURA WAKE..

shughuli nyingi zimesimama tunataka mtuambie tatzo ni nn? Kwa hali hii nani atashawishika kujenga kiwanda nchini?

HIVI MIKOA MINGINE UMEME UPO?
 
Back
Top Bottom