TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tatizo LA kukata umeme wilaya ya kyela kila siku hasubuhi na kurudisha usiku wa sa tano linatokana na nini?
 
Ninatatizo la umeme nyumbani kwangu majohe tangu jana, nimewasiliana na emergency zaidi ya mara 7 mpaka sasa sijahudumiwa, kila nikipiga simu naambiwa mafundi watakuja tangu jana jioni hawajafika
 
naitwa datch. namba yangu ya simu 0738262024. na namba yangu ya mita ni 37142130279. niko mkoa wa Dsm , wilaya ya Temeke, kata ya Mbagala Kuu, mtaa wa Butiama.

MATUMIZI YANGU KWA MWEZI NI CHINI YA UNIT 75. niko kwenye tariff 1. nanunua umeme kwa tsh 292/= kwa unit, nahisi mnaniuzia bei kubwa kuliko matumizi yangu MSAADA TAFADAHALI .
 
Nimejikuta nakasirika sana hii tabia ya tanesco kukata umeme kila jumatatu maeneo ya Tabata shule.

Yaani hapa nilipo natamani kupasuka utadhani nimemezeshwa amira. Kwakweli Tanesco mnatia kinyaaa. Nilidhani ni tatizo la siku moja. Lakini naona imekua tabia kila jumatatu lazima mkate umeme
 
1.ENEO HUSIKA
(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)
2.NAMBA YA SIMU
(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)
3.KARIBU NA NINI
(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)
4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO
(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)
5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI
(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)
6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME


Kwakweli kitengo cha huduma kwa wateja na dharura bado wapo chini sana kwa kuitikia dharura labda wasikie moto ndiyo angalau watakuja kwa kuchechemea vinginevyo sioni kama mpo serious.

Kuna ndugu yangu amereport hitilafu kwenye eneo lake lakini halishughulikiwi, binafsi ningeshauri matatizo yote yanayohusiana na kero za watendaji mikoani ziwe reported kwa mtu au kitengo maalumu HQ, ili wao watoe agizo kwa meneja wa eneo husika, lakini kwa sasa hao wanaopigiwa simu mikoani wanachukulia kila jambo rahisi, na mbaya zaidi badala ya wao kupokea taarifa na kufanyia kazi wanaanza kubishana na mtu aliye kwenye tukio.

Vile vile ningependekeza kuwe na namna tofauti ya kuwasilisha taarifa maana hapa si vyema kuandika personal details za mtoa taarifa kwakuwa anaweza kujenga uhasama kati yake na watoa huduma, wengi wa wahudumu wenu Tanesco, hawachukulii taarifa zinazofikishwa kwenu kama ni msaada bali ni kama kuwachongea, kwa maana hiyo "ingependeza zaidi" kama kungekuwa na confidentiality ili kumlinda mtoa taarifa
 
Hapa nilipo wamekata dakika tano zilizopita......na hii ndiyo Tabia yao ikifika SAA moja na nusu kila siku wanakata umeme unarudi SAA mbili.....swali ninalojiuliza kwanini hiko kifaa kiharibike kila siku SAA moja na nusu usiku then baada ya nusu SAA kiwe freshi??? Sipati majibu wallah
 
yaani dakika 5 tu wewe unalalamika,..???!!! wakati huku kwetu tangu saa moja unusu asubuhi mpaka muda huu hakuna umeme.....!!!????

halafu ni kila siku sasa , dah, ni zaidi ya mateso sasa...
 
Mimi mita yangu imeunguwa na nimebadilishiwa mita jana na wakati mita inaungua kulikuwa na unit zaidi ya 100 je naweza rejeshewa unit zangu
 
Tatizo LA kukata umeme wilaya ya kyela kila siku hasubuhi na kurudisha usiku wa sa tano linatokana na nini?
Afadhali umeuliza na mimi nilitaka kuwauliza hivyo hivyo, maana nahisi Kyela ndio sehem pekee inayoongoza kwa kukatiwa umeme.
 
Kwenu TANESCO:
naomba kujua baadhi ya Key shortcut za LUKU ili nijue maana sisi wapangaji tunaoneana kwenye masuala ya kuweka umeme.

Kama mshajibu swali la namna hii hapa basi naomba mnitag kwenye jibu.

Nasema hivyo kwa sababu kuna wakati tunachanga hela za umeme lakini matumizi yake na kiwango cha umeme haviendani!

Mimi najua njia moja tu ya kubonyeza 07 halafu ENTER ndo najua Unit zilizopo, lakini napenda kujua zaidi ya hapo...
Matumizi ya Unit kwa siku, kama mtu kaweka umeme sipo labda wiki nikitaka kujua mara ya mwisho kaweka umeme kiasi gani, nk...
Naomba msaada wa hali na mali kwa hili please!

N.B: Kwa sasa nilipo tunatumia mita ya ukutani,siyo hivi vidogo vya kuweka betri na kuvichomeka kwenye chaji muda wote. Ni hii kubwa ya Ukutani! Ni hayo tu
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa niki report tatizo la umeme Hapa Savei.

Kama kawaida ya mafundi wa Tanesco hufika na kurekebisha baada ya sku 2 tatizo hurudi palepale, nimejaribu kufuatilia kwa umakin kujua tatizo ni nini nimegundua tatizo ni loose connection yaani.

Baada ya fuser kukatika kukiwa na tatizo mafundi wakishatengeneza hawabadilishi fuse wanachofanya ni kufunga waya sasa pale walipofungia kunakuwa na loose connection waya hupata moto na kutoa cheche baadaye umeme hukatika.

Jaman Tanesco fanyeni kazi kwa weledi sio kulipua kila sku tumechoka.
 
Jamani ivi TANESCO Busega mmejipanga kweli?Naomba makao makuu tusaidieni, hatuoni sababu ya kusubiri ujio wa Rais.

Nimelipia Meter wakanyamaza kimya nimejaribu kufatilia wanasema vifaa havipo.

Sasa nashindwa kuelewa ni vifaa au wanataka kitu kidogo? Maana hata Survey walikuja baada ya kuripoti makao makuu.
Jamani tusaidieni.
 
Jamani ivi TANESCO Busega jamani wamejipanga kweli. Naomba makao makuu tusaidieni, hatuoni sababu ya kusubiri ujio wa Rais.
Nimelipia Meter wakanyamaza kimya nimejaribu kufatilia wanasema vifaa havipo.
Sasa nashindwa kuelewa ni vifaa au wanataka kitu kidogo? Maana hata Survey walikuja baada ya kuripoti makao makuu.
Jamani tusaidieni.
Ndugu Mteja tunaomba namba yako ya simu
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa niki report tatizo la umeme Hapa Savei.
Kama kawaida ya mafundi wa Tanesco hufika na kurekebisha baada ya sku 2 tatizo hurudi palepale, nimejaribu kufuatilia kwa umakin kujua tatizo ni nini nimegundua tatizo ni loose connection yaani.Baada ya fuser kukatika kukiwa na tatizo mafundi wakishatengeneza hawabadilishi fuse wanachofanya ni kufunga waya sasa pale walipofungia kunakuwa na loose connection waya hupata moto na kutoa cheche baadaye umeme hukatika.Jaman Tanesco fanyeni kazi kwa weledi sio kulipua kila sku tumechoka.
Ndugu mteja tunaomba namba ya taarifa uliyo repotia na namba ya simu
 
Back
Top Bottom