TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Masuala ya uwazi katika utendaji wa serikali kila nyanja yamepigwa marufuku awamu hii. Hivyo usitegemee kutaarifiwa kuwa umeme utakatika wala sababu za kuendelea kuwa na mgao
 
MAHANJU
Kuna taarifa imetumwa kwamba kumetokea hitilafu ktk Grid ya Taifa iliyopelekea umeme kukatika muda wa saa moja na dakika mbili leo asubuhi na tatizo hilo linashughulikiwa sasa wewe unayeongea sana mara CCM imefanya hivi, kwani hao walio nje ya CCM si na wao walikuwa CCM na bado matatizo haya ya umeme tulikuwa nayo.

Kipindi Lowassa akiwa Waziri Mkuu alisema ataleta umeme kutoka Indonesia sijui ulikuwa ni umeme wa kuchota na ndoo lkn hatukuuona hd anatimuliwa madarakani kwa ufisadi wa RICHMOND.

Sumaye huyo mlonaye ndo ziro kabisa kakaa kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu miaka kumi kuliko Mawaziri Wakuu wote tangu Tanganyika ipate Uhuru lkn hatukuona la maana alilofanya sasa leo hii ndo ataweza kutatua matatizo ya umeme?

Tujadili matatizo ni kwa namna gani tuyaondoe lkn ukiongelea chama mimi japo si mwana CCM lkn naona hakuna chama mbadala wa kuiongoza Serikali bali nawaona walioko huko upande wa pili ni makanjanja tu..!!!
 
Huku kwetu ni balaa yanii ni bora mtu uwe na taarifa. Ofisi yetu kwa mwezi umeme wa Tanesco tunalipa wastani was laki moja na nusu lakini tokea shida imeanza takribani wiki mbili sasa wastani kwa wiki tunatumia mafuta ya shs laki mbili kwa ajili ya kuendesha genereta na uzalishaji umepungua

Nidhamu ya woga ni mbaya sana.. Au kwa sababu ikulu kuna umeme 24/7 ndo manaana tanesco inaogopa kutangaza mgao was umeme? Watu wanaogopa kutangaza mgao wa umeme kisa kuogopa kutumbuliwa.
Kama mgao unauona kwanini mpk utangaziwe?
 
Kuna taarifa imetumwa kwamba kumetokea hitilafu ktk Grid ya Taifa iliyopelekea umeme kukatika muda wa saa moja na dakika mbili leo asubuhi na tatizo hilo linashughulikiwa sasa wewe unayeongea sana mara CCM imefanya hivi,kwani hao walio nje ya CCM si na wao walikuwa CCM na bado matatizo haya ya umeme tulikuwa nayo. Kipindi Lowassa akiwa Waziri Mkuu alisema ataleta umeme kutoka Indonesia sijui ulikuwa ni umeme wa kuchota na ndoo lkn hatukuuona hd anatimuliwa madarakani kwa ufisadi wa RICHMOND. Sumaye huyo mlonaye ndo ziro kabisa kakaa kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu miaka kumi kuliko Mawaziri Wakuu wote tangu Tanganyika ipate Uhuru lkn hatukuona la maana alilofanya sasa leo hii ndo ataweza kutatua matatizo ya umeme? Tujadili matatizo ni kwa namna gani tuyaondoe lkn ukiongelea chama mimi japo si maana CCM lkn naona hakuna chama mbadala wa kuiongoza Serikali bali nawaona walioko huko upande wa pili ni makanjanja tu..!!!
.....
.....zekikis era
 
Unapoandika jitahidi kufanya uchambuzi wa mambo unayoandika. Kuhusu suala la umeme, huoni jitihada zinazofanywa. Ule mradi wa stiglers george unazani utaingiza megawati ngapi katika gridi ya taifa? Tatizo vijana wa chadema kutamani jambo fulani litokee kama ndoto bila kuwekeza jitihada kufikia hiyo ndoto.
Hebu acha kutetea ujinga., hivi unajua ni jinsi gani kukatika huku kwa umeme tena bila taarifa kunavyowaathiri wananchi hususani wafanyabiashara wadogo wadogo? kwa hio hadi hayo yatendeke mnataka hawa vijana biashara zao ziwe zimekufa au vipi? nyie ndio mnaiharibu hii nchi kwa tabia yenu ya kujustify the unjustifiable
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA KWA WATEJA WALIOUNGWA KATIKA GRIDI YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa mnamo majira ya Saa moja na dakika mbili asubuhi imetokea hitilafu katika Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha Mikoa yote iliyo unganishwa katika Gridi kukosa umeme.

Jitihada zinaendelea kurejesha umeme kwa haraka na tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

30/11/2017
 
Naomba mtulie wananchi, Tanesco ipo kwenye mchakato yakinifu wa upembuzi wa miundombinu ya kuchakata umeme kwa kutumia mafuta ghafi yatakayoanza kuchimbwa Hoima, Uganda... kuweni wapole jamani
 
Back
Top Bottom