TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nimefika nyumbani no umeme .Hivi wakitutangazia mgao inakuwaje. Nimesema Tena Tanzania tujiandae na recession ya kufa mtu Mungu tusaidie.

Na CCM watu wataendelea kuwapigia makofi.Viwanda tunaanzishaje Kama hali yenyewe ya umeme Ni hii. Mapato lazima yashuke. Naona tunaelekea Zim
 
Stupid people like you are still alive. Nani alikudanganya maendeleo utapata kupitia chama. Nani alikwambia tz haitakuwa na majanga. Hivi Kwa lugha Kama zako. Wewe huwezi Kama mfanyakazi kuhujumu mitambo. Kama midomo na akili yako imeisha hapo Heri tumia viungo Vingine kuongea
Ulichoandika hakieleweki unataka ujibiwe nini?
Kama una shaka na uelewa wako waachie wenyewe wajibu wee pita kimya kimya.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA KWA WATEJA WALIOUNGWA KATIKA GRIDI YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa mnamo majira ya Saa moja na dakika mbili asubuhi imetokea hitilafu katika Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha Mikoa yote iliyo unganishwa katika Gridi kukosa umeme.

Jitihada zinaendelea kurejesha umeme kwa haraka na tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

30/11/2017
Sio wa gridi ya taifa tu hata sisi wa gesi tunapata shida hasa Masasi mpaka mangaka imekuwa kero unakaa siku tatu hujaona umeme hili linakera
 
Tulikua tukiambiwa mgao ni kutokana na bwala la mtera kukauka kwa maji
Hivi sasa ni Masika nchi nzima, sababu imekua mitambo ya gesi.

Cha ajabu LUKU yako ikiisha papo hapo umeme unakatika hamna hata nyongeza ya nusu saa ili ununue LUKU
NINGESHAURI TU,,SERIKALI IKARUHUSU KAMPUNI BINAFSI ZA UMEME KUWEKA NCHINI, kama walivoruhusu MAKAMPUNI BINAFSI YA SIMU DHIDI YA TTCL
 
Mimi ni mkazi wa chanika zogoali sio mbali kutikea chamika standi au ume ulipo ishia natakilibani miaka miwili nilipo mpaka sasa umeme hauja fika na majina yaliandikishwa kwa wale tunao hitaji umeme mpaka sasa hakuna maendeleo yoyote . sijui mtatusaidia vipi.
Tumeipokea kwa hatua zaid
 
Nyie tanesco rujewa mbeya kila siku lazima mkate umeme mtuambie km ni mgao
 
Mnatuharibia mifumo nyie kima ni makatili wa maendeleo mtaficha sana lakini tutaujua ukweli
 
Wakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.. Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k

Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?

Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?

nchi ya viwonder
 
Back
Top Bottom