Nusu saa iliyopita mmeenda Manyuki Transfoma Manispaa ya Morogoro mjini mmekata umeme alafu mkaipiga shoti transfoma mkaamua kubeba ngazi na kurudi ofisini. Wananchi baadhi ya Laini hawana umeme VP mnampango wa kuwarudishia leoleo ama mmlikuwa na lengo gani?
Mnakoelekea siko kuzuri, yaani watu wanatumia umeme nyie mnafika mtaani kwao mnawakatia alafu inasikika shoti Kwenye transfoma ..mnabeba ngazi mnaondoka!!.. Hawa wananchi wanaowatizama kwa ujinga mnaowafanyia hadharani asubuhi kweupe...kuna siku mtalipa gharama za hasira zao.
Km kuna kitu mnakifanya toeni taarifa kwamba mnaipiga shoti transfoma na mtazima umeme.
Turudi Kwenye point, umeme leo watapata ama watalala giza Leo?? Km mnatengeneza mtatumia siku ngapi?