TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Ivi kauli ipi ni sahihi? Waziri kalemani kasema tukihisha lipia service line tufungiwe ndani ya wiki moja wkt tanesco mnasema tusubiri zaidi ya mwezi m1, mbona mikanganyiko?

Muhudumu wa tanesco tuondolee hii sintofahamu. Mimi niko kigambon Dar, nikisubili kufungiwa umeme kwan nimeishalipia km bwana kanyigo apo juu,
 
Ivi kauli ipi ni sahihi? Waziri kalemani kasema tukihisha lipia service line tufungiwe ndani ya wiki moja wkt tanesco mnasema tusubiri zaidi ya mwezi m1, mbona mikanganyiko? Muhudumu wa tanesco tuondolee hii sintofahamu.
Mimi niko kigambon Dar, nikisubili kufungiwa umeme kwan nimeishalipia km bwana kanyigo apo juu,
Tunashukuru sana, ipo miradi ambayo mteja anaweza kufungiwa haraka, lakini kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja mteja anafungiwa umeme ndani ya siku 30 kama yupo ndani ya mita 30, siku 60 zaidi ya mita 30 mpaka100 na siku 90 zaidi ya mita 100 , siku zote ni za kazi
 
Kwanza ilikuwa 0.3% ikaja 2.5% now imekuwa 0.5% biashara ya kuuza umeme ishakuwa mbovu sana inamaana ukiuza umeme wa laki faida sh 500
Hii ni hatari kubwa sana.kodi ya pango 200,000,Dada wa kuuza 70,000,mlinzi 5000,taka 5000,umeme 30,000.....badoTRA.kumbuka umechukuwa fedha benki na interest ni 5% and above?he kuna kujiajiri kweli?Je tutapona.hii ni kwamba wauzaji wa umeme wataacha hii kazi na wateja wataenda tanesco.

MTU anataka umeme wa buku 2 na anapakia gari LA 800.tanesco wanmuda maalum wa kuuza.wengine wanasema tutumie simu.huku mjini umeme lazima risit kwa vile wanachanga.ni vyema wafanya maamuzi waangalie mtumiaji wa mwisho sio max wala selcome
 
mkuu kuna ada wamekukata mbali na hela ya huo umeme mm nimenunua hapa wa buku tatu nimekatwa 33 kama ada sasa sijui ni kote au pia sijatumiwa mpaka sasa hvi
SERIKALI ISHAANZA KUWAIBIA WATU,IWEJE UNUNUE UMEME WA BUKU 3 UKATWE THS 33? KWAHIYO SERIKALI INAKATA TENA 1.1%,SASA HIYO VAT YA 18% INAENDA WAPI? MBONA KODI MBILI MBILI? HIYO 18% YA VAT nA HII 1.1% NANI ANACHUKUA? ZINAENDA SEHEMU MBILI TOFAUTI?
 
we TANESCO kuwa na adabu. umeme hakuna Dar nzima ulikatika. pili wanaojaribu kununua haununuliki. mna uchuro gani???
 
Tanesco toeni muongozo umeme haununuliki huku kila njia haiwezekani nimeninua kwa tigo mmekata hela na hakuna chochote
Umeme unanunulika mpendwa mteja umenunua wa tsh ngapi na kupata ujumbe ganj
 
Mteja anakatwa vat 18% rea 3% na ewura 1% hakuna makato mengine kwa t1 na d1
 
we TANESCO kuwa na adabu. umeme hakuna Dar nzima ulikatika. pili wanaojaribu kununua haununuliki. mna uchuro gani???
Umeme upo mkuu isipokuwa makongo changanyikeni na maeneo ya jirani ambapo napo utarejea hivi punde
 
Umeme unanunulika mpendwa mteja umenunua wa tsh ngapi na kupata ujumbe ganj
Nimenunua kwa Tigo pesa hela wamekata na hakuna ujumbe wowote nimejaribu kwa m pesa imegoma nikaenda selcom naambiwa kuna tatizo
 
Tanesco toeni muongozo umeme haununuliki huku kila njia haiwezekani nimeninua kwa tigo mmekata hela na hakuna chochote
Mimi pia nimenunua muda si mrefu Kwa TIGO pesa..hela imekatwa cha ajabu msg ya token hairudi.
 
Kwa kuwa tuu naheshim maadili na kutumia lugha isiyo na staha siyo jambo jema ila nimachoweza kusema ni kuwa Tanesco mnakera sana kwa huduma zenu mbovu
 
Umenunua kwa njia gani na ukapata ujumbe gani mpendwa mteja
Mie sijanunua umeme, nina unit Zach kutosha tu, shida yangu mmekata umeme tangu jana saa tatu usiku hadi ninanvyoandika hapa umeme haujarudi, tunaomba mrudishe umeme
 
Mteja anakatwa vat 18% rea 3% na ewura 1% hakuna makato mengine kwa t1 na d1
Tanesco hapa nianvo kwambia nimenunua umeme kwa tigopesa wa elfu 3 nimekatwa sh 33 mbali na hyo buku tatu kama ada kitu ambacho cijawahi kukatwa nimepiga cimu mpaka tigo nimeongea na muhudumu wao kanambia ni utaratibu mpaya ambao umeanza kutumiaka na mpaka sasa hvi cijapata token nimeambiwa mnamatatizo kwenye upokeaji wa malipo kutoka kwao hapa nabiashara imebidi nifunge tuu
 
Mteja anakatwa vat 18% rea 3% na ewura 1% hakuna makato mengine kwa t1 na d1
TANESCO MSITUFANYE WAJINGA,FUATILIA UMEME WANAKATA TENA 1.1% UKIONDOA,VAT 18%,REA 3% NA UWERU 1%,HAYO MAKATO MAPYA YA 1.1% YAMETOKA WAPI? NIMENUNUA KWA TIGO PESA UMEME NIMEKATWA FEDHA YANGU ILIYOPO KWENYE TIGO PESA AMBAYO NI 1.1% YA UMEME NILIONUNUA,NIMENUNUA UMEME WA BUKU 10 TIGO PESA WAMEKATA JUMLA 10,110/= HILO KATO LILILOONGEZEKA LINAENDA KWA NANI 110/=? HUU SI WIZI? MBONA MWANZO UKINUNUA WA ELFU 10 INAKATWA HIYO HIYO ELFU 10?
 
Back
Top Bottom