TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Ni masaa 19 mpk ivi sasa hamna dalili ya umeme kurudi, I guess tunalala giza tena na leo huku Makongo siku ya pili mfululizo, Nchi ya viwanda wananchi wanakaa bila umeme 2days, Mi ngekuwa waziri wa nishati ngetumbua Tanesco yote afu nieke team mpya! Mvua zikinyesha wanasingizia mvua, labda na leo Jua limezidi-;:!?””’*^_
Nahisi Kuna mgao, sisi walirudisha saa kumi Tangu saa mbili wameshauchukua
 
Masaa 24 yametimia umeme bila bila, mi nahama hiii nchi!
Bora aisee....ukipata opportunity huko usinisahau
Eti tren ya standard gauge....kwa umeme upi haswaa, Tanzania tunachekesha sana, wa majumbani tu umewashinda sembuse wa viwanda[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Nikilifikiria joto la usiku nakosa amani kabisa
 
HABARI NDG TANESCO
JANA TAREH 01/04/2018
NILINUNUA UMEME KWA TIGOPESA 0655673456
KWA Tsh 9,200/- nikapata unit 75.2
KWA BAHATI MBAYA NIKADELETE TOKEN ..
NAOMBA MSAADA WA ILE TOKEN
KTK MITA 24212706774
natanguliza shukrani
 
Mkuu kwa usahihi zaidi nunua tu kwenye benki au kwenye kibanda/wakala/wa/ cha Tanesco.
Yani safari hii ni mnyooko wa nguvu wallah...

Hata hizo machine wengi zitatushinda coz kama kwenye lak1 faida unapata mia5 si tutakaa sana!?

Kwenye cm nako mfano tigopesa ndohivo wanakata na ziada
 
HABARI NDG TANESCO
JANA TAREH 01/04/2018
NILINUNUA UMEME KWA TIGOPESA 0655673456
KWA Tsh 9,200/- nikapata unit 75.2
KWA BAHATI MBAYA NIKADELETE TOKEN ..
NAOMBA MSAADA WA ILE TOKEN
KTK MITA 24212706774
natanguliza shukrani
Wapigie tigo wqkutumie masege tena
 
Tetesi nilizoziskia ni kwamba Tanesco wamesitisha kununua LUKU,kupitia mitandao ya simu,ni kutokana na yule Mfanyabiashara maarufu aliyefungwaga jela akatoka na aliwahi kuwa M/kiti yanga na pia aliwahi kuwa Mh Diwani wa Mbagala kumiliki Hisa kubwa kwenye mitandao ya simu.

Tanesco je hizi tetesi zinaukweli ndani yake???
 
naomba msaada tafadhali,luku yangu number 24218162899 ina shida kubwa,wakati imeweka ilikuwa inafanya kazi vizuri lakini ghafla units za umeme zilianza kwisha kwa kasi ya ajabu, nilitoa taarifa tanesco kilimanjaro kuhusu tatizo hilo ushauri walionipa nicheki wiring ya nyumba nzima zoezi hilo lilifanyika lakini kulikuwa hakuna linkage yeyote, sina matumizi makubwa ya umeme, ni mhumini mkubwa wa energy save, naomba nijue labda nko tarriff gani?

lakini pia tatizo ni nini unit 28 kutumika ndani siku 12 wakati units hizo hizo 28 kwenye nyumba yangu nyingine yenye matumizi zaidi zinatumika zaidi ya wiki 3
 
Tetesi nilizoziskia ni kwamba Tanesco wamesitisha kununua LUKU,kupitia mitandao ya simu,ni kutokana na yule Mfanyabiashara maarufu aliyefungwaga jela akatoka na aliwahi kuwa M/kiti yanga na pia aliwahi kuwa Mh Diwani wa Mbagala kumiliki Hisa kubwa kwenye mitandao ya simu.
Tanesco je hizi tetesi zinaukweli ndani yake???
Ndugu mpendwa mteja, acha kufata taarifa za tetesi sikiliza na pokea taarifa zetu kutoka kwetu, tulitoa taarifa kamili hapa kwenye thread yetu
 
Nimepitia uzi wenu wa 'zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na Tanesco'. Kwenye huo uzi mmesisitiza baada ya surveyor kupita, malipo ili kuvutiwa umeme yatafanyika bank tu.

Pale Himo ofisi ya Tanesco, ukifika hawakupi hiyo reference number ya kwenda kulipia bank. Wanakwambia hivi sasa network imekata, so inabidi ulipie palepale Tanesco.

Then wanakuandikia risiti wao, wanaigonga muhuri. Hili swala limekaaje kwa ofisi zenu za mikoani. Sababu kwa jinsi mlivyotoa msisitizo wa kulipia bank, hapa naona kuna kitu si cha kawaida. Kunawatu huko mikoani wanajipigia tu hela ya serikali na wananchi.

Pale himo fomu ya maombi unauziwa, pia unatakiwa utoe na hela ya surveyor. Funny enough surveyor akija anakuomba pesa ya nauli. Anakuja na pikipiki ya kukodi. Ila ukiangalia vizuri hakuna dalili za kukodi, ni mradi wake au wanagawana pesa na yule kijana anayeendesha ile pikipiki.

Vitu vitu vyote hivyo ni kinyume na maelezo yenu.
 
naomba msaada tafadhali,luku yangu number 24218162899 ina shida kubwa,wakati imeweka ilikuwa inafanya kazi vizuri lakini ghafla units za umeme zilianza kwisha kwa kasi ya ajabu,nilitoa taarifa tanesco kilimanjaro kuhusu tatizo hilo ushauri walionipa nicheki wiring ya nyumba nzima zoezi hilo lilifanyika lakini kulikuwa hakuna linkage yeyote,sina matumizi makubwa ya umeme,ni mhumini mkubwa wa energy save,naomba nijue labda nko tarriff gani?lakini pia tatizo ni nini unit 28 kutumika ndani siku 12 wakati units hizo hizo 28 kwenye nyumba yangu nyingine yenye matumizi zaidi zinatumika zaidi ya wiki 3
Tunaomba namba ya simu na eneo lako
 
habari ya mchana! nimenunua umeme luku wa sh 100,000.00 kinacho nishangaza, units zimepungua na kuna makato ya fee. swali langu hayo ni makato ni mpya?
 
habari ya mchana! nimenunua umeme luku wa sh 100,000.00 kinacho nishangaza, units zimepungua na kuna makato ya fee. swali langu hayo ni makato ni mpya?
Umenunua kwa njia gani mpendwa mteja wetu
 
Back
Top Bottom