TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nilitoa taarifa tabata tanesco kupitia simu kua nguzo iko ktk hali mbaya inaweza kudondoka nikapatiwa namba ya taarifa 3769 tokea hyo siku tarehe 21januari2018 mpaka Leo hakuna walichofanya pmj na juhudi zote za kuwakumbusha.........ifike pahala mtujali wateja wenu
 
Naomba namba za Tanesco Moshi mjini. Transformer imeharibika sasa inaelekea siku ya 5 hatuna umeme huku
 
Naambiwa kule Ngara/ Rulenge kuna tatizo kubwa sana la umeme. Ni Mwezi sasa umeme unaweza kuwa kwa saa moja tu au mawili kwa siku. Rulenge wameungwa kwenye grid kutoka kwenye majenerato, tangu wakati huo umeme ni shida sana. Ngara wanawasha jenereta umeme ukikatika wa grid, Rulenge, Benaco hapana hadi grid irudi. Saidieni
Eneo gani haswa na namba yako ya simu tulifatie
 
Nilitoa taarifa tabata tanesco kupitia simu kua nguzo iko ktk hali mbaya inaweza kudondoka nikapatiwa namba ya taarifa 3769 tokea hyo siku tarehe 21januari2018 mpaka Leo hakuna walichofanya pmj na juhudi zote za kuwakumbusha.........ifike pahala mtujali wateja wenu
Tumeipokea kwa hatua zaidi mpendwa mteja
 
habarini Tanesco, Mimi NI mkazi wa Tanesco mkoa wa ilala, Nyumba yangu iko ukonga, shida yangu kuu napenda kuuliza, nimepata tetesi kuwa wale tulikuwa na madeni na tukaingia katika mfumo wa malipo kwa njia ya LUKU mkoa wa ilala, tumefutiwa madeni je kuna ukweli wowote juu ya hili!? msaada Tafadhali namba yangu ya LUKU ni 24219542842
 
Ndugu mteja sio kweli madeni yote yapo pale pale isipokuwa wateja wanaolipa mara moja wanaweza kuomba kupunguziwa riba
 
ha ha ha, akijibu naomba unistue

Ameshindwa, yaelekea still yupo kwenye early 1980s maana ameng'ang'ania anataka namba zangu za simu vinginevyo tatizo hatalifanyia kazi ati inatafsiriwa kuwa uzushi, nami nimeachana naye mpaka yasikikike maafa labda watajiongeza na kujua kuwa kuna namna nyingi za kulifikia eneo la tukio zaidi ya namba za simu
 
Moja ya transformer iliyopo mjini kabisa. Uongozi na wafanyakazi wanapita hapa kila siku. Hii ni nini? Au mpaka rais alisemee!
20180427_103650.jpeg
20180427_103605.jpeg
20180427_103553.jpeg
 
Nimejaribu kuzigeuza nimeshindwa. Mnisamehee bure
Mkuu hizi Picha zako na jinsi ulivyoziweka hapa Kimwonekano hizi Shingo zetu zikipata matatizo kwa Kuuma kutokana na Kuzipinda ili tuzikodolee / tuziangalie vizuri utakuwa tayari kutununulia dawa za Maumivu?
 
nimehamia nyumba fulani sasa kumbe mita ilikuwa ina deni,tafadhali naomba niangalie ina deni kiasi gani ili nijipange kulipa,mita namba 43000839035
 
Habari ni kwanini mmeweka tofauti unit maana kuna matumiz madogo na matumizi makubwa kwanini mzingeweka kuwe na uniti sawaa kwasababu matumisi ya MTU ndio yatamfanya anunuee umeme
 
Salaam.
Naomba kufahamishwa kama kuna mabadiliko yoyote ya muda uliopangwa kwa mteja kuunganishiwa umeme pale anapokuwa amelipia gharama za service line.

Inafahamika kuwa baada ya mteja kulipia, TANESCO wanatakiwa kumfungia mteja umeme ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu (3). Lakini jambo la kusikitisha ni miezi zaidi ya mitano napewa maelezo ya kukosekana kwa nguzo hivyo kutoweza kufungiwa umeme.

Hakika jitihada za Serikali za kuhakikisha Watanzania wengi wanapata umeme zinakwamishwa na Mameneja wa TANESCO wa Wilaya.

Jimulikeni na mjirekebishe ili ndoto za Mheshimiwa Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, za Tanzania ya viwanda ziweze kutimia.

Mteja,
MADALE, Wilaya ya Ki-TANESCO ya TEGETA,
KINONDONI- DAR ES SALAAM.
 
Back
Top Bottom