TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO IMEWAPATIA WANAKIJIJI UMEME SHULE YA SEKONDARI HAINA UMEME.
nimekuwa nikijiuliza hivi uongoz wa kata na wilaya hauko serous na usambazaji wa umeme. Leo ni mwaka 3 shule ya sekondari Magubike haina umeme huko huduma zingine kama hospital walishapelekewa.waziri wa nishati na madin wanafunz hawapati muda wa kujisomea na kusababisha mimba kuongezeka kwa sababu wazazi hawawezi kuweka watoto hostel wakati umeme no.
Wahusika kama munaniskia shule ya sekondari Magubike haina umeme kabsa huku kipaumbele cha serikali ya awamu ya tatu ni kupata umeme..alishakuja meneja wa mkoa akafika akaangalia lakin hado kimya.

Njoon magubike ipo barabara ya Dodoma ukipita tu Dumila kama unaelekea Dodoma.
Je shule hii iliomba umeme? Taasisi mashirika au watu binafsi hupelekewa umeme mara baada ya kukamilisha wiring na kuleta maombi
 
Kwanza polen kwa kazi kubwa.

Mji mdogo wa Dumila morogoro utapata lini huduma ya REA yaan umeme upo njian tu tufanyeje tuotaka kufungua mashine za mpunga pembezon.yaan mji hauna umeme.
Njoon muangalie ukiwafuata Mvomero kila kitu gharama kuanzia nguzo,waya, mita tutafika kweli..ifike hatua mameneja wa tanesco token ofisi njoon kwa wananchi tunaumia ndugu zangu
umila umeme upo na maeneo ya karibu na hapo kuna miradi ya REA inayoendelea, tungepata mawasiliano ya mteja husika tujue ni eneo gani hasa analolizungumzia
 
TANESCO Nafahamu changamoto mnazopitia katika kazi zenu ni nyingi leo nawapa courage tu endeleeni kuchapa kazi.
 
Namba ngapi mpendwa mteja
Swali langu. Niliomba mniambie juu ya kijiji cha MABUYE na vitongoji vyake vya KIJUKA, MABUYE, RUHAMA NA ITALA, kata Kassambya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kama kitapata umeme wa REA au LA maana karibia vijiji vyote vilivyo kizunguka vina umeme ila chenyewe hakina japo kina sifa zote za kupata umeme. Pia kama kitapatiwa naomba kuambiwa ni lini na kama hakimo kwenye orodha ya kupewa niambiwe pia. Nitashukuru.
 
Tuliwahi kutolea ufafanuzi maeneo haya kuwa miradi ya rea inaenda kwa awamu sasa tupo awamu ya tatu hivyo tuwe na amani huduma itafika
 
Tuliwahi kutolea ufafanuzi maeneo haya kuwa miradi ya rea inaenda kwa awamu sasa tupo awamu ya tatu hivyo tuwe na amani huduma itafika
Nashukuru sana ngoja niendelee kufanya wiring ili siku ikifika niwe wa kwanza kupata nishati hiyo adhimu.
 
Naomba kufahamu ni sababu ipi imewafanya mpaka sasa kwa Moshi mjini mnawatoa wateja wenu kwenye tarif 4 nakuwarudisha kwenye tarif 1
Naomba maelezo juu ya jambo hili
Asanteni
 
Tanesco tunapata shida sana hapa Tabata matumbi mpaka dampo almost three days consecutively kila inapofika asubuhi mnakata umeme kurudisha jion ama usiku ...kuna mgao ama shida ni nini
 
Tanesco kumekua na kukatika katika kwa umeme maeneo ya Tabata matumbi mpaka dampo for almost three days consecutively mnkata umeme asubuh mnarudisha usiku na hakuna notification ....ni mgao ama shida ni nini Meneja was Tanesco ilala....
 
Aaaah jamani Tanesco hii sasa sifa, kwa nini mnatukatia umeme kila siku asubuhi halafu mnarudisha usiku maeneo ya gongo la mboto mpaka majohe? Leo ni siku ya 3 mfululizo, je ni mgao umeanza tujiandae kisaikolojia?
 
Na mimi nasubiri majibu nipo hapa tabata old dampo magerage leo siku ya pili tumekumbana na mgao wa umeme shughuli zimesimama alafu hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na Tanesco
Kama ni mgao semeni tujue na huu mgao utachukua muda gani ?
 
Tanesco mrgr wamelelala tang juz umeme umekatika mtaa wa karume hadi leo wamepiga kimya, mtaa upo ktkt ya mji giza limetanda mpaka aibu, inasemekana shoti ndio sababu kama ambavyo wahudum wa hapa gest iliopo mtaa nliofikia wanaelezea, kama wagen tumechoka na kero hii kwa siku mbili hiz vipi wenyeji c watakaa mwez mzima?
 
Yaani nguzo Arusha zimekuwa adimu zaidi ya dhahabu. Unaweza kuipata baada ya miezi kadhaa, hivi viwanda tutaendeshaje. Inaleta mianya ya urasimu.
 
Kwa muda wa wiki mbili sasa maeneo ya Gongolamboto, Pugu, Chanika na Kisarawe umeme umekuwa ukikatika asubuhi na kurudi usiku saa moja au saa mbili kiasi cha kuwatia hasara wananchi wanaotumia nishati hiyo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Tanesco wamekuwa wakikata umeme bila kutoa taarifa. Hakuna tangazo rasmi la katizo la umeme. Watu waliojiajiri kwenye viwanda vya Saluni ni waathirika wakubwa maana kwa wiki mbili nzima hakuna umeme. Walioweka samaki, matunda na vyakula kwenye majokofu wanaishia kumwaga tu vyakula sababu vinaharibika.

Hata usiku umeme unaporudi unakuwa ni wenye kukatika katika kabisa.

Tanesco tangazeni mgao wa umeme tuwaelewe
 
Tuliwahi kutolea ufafanuzi maeneo haya kuwa miradi ya rea inaenda kwa awamu sasa tupo awamu ya tatu hivyo tuwe na amani huduma itafika

Kwa nini ukitaka kuvuta umeme nguzo zikizidi mbili mnaita mradi na mteja ukipigiwa Bei zaidi ya nguzo mbili Bei inakuwa kubwa Sana
 
Back
Top Bottom