TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO Ukonga. Nimepeleka maombi ya kuunganishiwa umeme tangu mwezi June mwaka huu, nikapewa account ya kulipia shilingi laki nane. Nikalipa, kisha nikaambiwa nisifike tena TANESCO kwani kuna foleni kubwa ya wateja, nitapigiwa simu. Mpaka leo ni kimya.

Je, inachukua miezi mingapi kwa mteja kuunganishiwa umeme?
Naona TANESCO mnachagua post za kujibu
 
TANESCO TUAMBIENI UKWELI LEO SIKU YA TATU TUNALALA BILA UMEME GONGO LA MBOTO , MAJOHE NA MAENEO MENGINE ...KUNA NINI????
 
Shirika la umma na moja ya taasisi kubwa na nyeti
 
Tanesco tunapata shida sana hapa Tabata matumbi mpaka dampo almost three days consecutively kila inapofika asubuhi mnakata umeme kurudisha jion ama usiku ...kuna mgao ama shida ni nini
Ndugu mpendwa mteja tulitoa taarifa ya ikarabati wa miundombinu eneo lako
 
Na mimi nasubiri majibu nipo hapa tabata old dampo magerage leo siku ya pili tumekumbana na mgao wa umeme shughuli zimesimama alafu hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na Tanesco
Kama ni mgao semeni tujue na huu mgao utachukua muda gani ?
Je leo hamna umeme?
 
Tanesco mrgr wamelelala tang juz umeme umekatika mtaa wa karume hadi leo wamepiga kimya, mtaa upo ktkt ya mji giza limetanda mpaka aibu, inasemekana shoti ndio sababu kama ambavyo wahudum wa hapa gest iliopo mtaa nliofikia wanaelezea, kama wagen tumechoka na kero hii kwa siku mbili hiz vipi wenyeji c watakaa mwez mzima?
Eneo gani na namba yako ya simu mpendwa.mteja wetu
 
Yaani nguzo Arusha zimekuwa adimu zaidi ya dhahabu. Unaweza kuipata baada ya miezi kadhaa, hivi viwanda tutaendeshaje. Inaleta mianya ya urasimu.
Umeomba umeme kwa jina gani na namba yako ya simu tafadhali
 
Kwa muda wa wiki mbili sasa maeneo ya Gongolamboto, Pugu, Chanika na Kisarawe umeme umekuwa ukikatika asubuhi na kurudi usiku saa moja au saa mbili kiasi cha kuwatia hasara wananchi wanaotumia nishati hiyo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Tanesco wamekuwa wakikata umeme bila kutoa taarifa. Hakuna tangazo rasmi la katizo la umeme. Watu waliojiajiri kwenye viwanda vya Saluni ni waathirika wakubwa maana kwa wiki mbili nzima hakuna umeme. Walioweka samaki, matunda na vyakula kwenye majokofu wanaishia kumwaga tu vyakula sababu vinaharibika.

Hata usiku umeme unaporudi unakuwa ni wenye kukatika katika kabisa.

Tanesco tangazeni mgao wa umeme tuwaelewe
Ndugu mpendwa mteja wetu tumepokea taarifa hii kwa ufatiliaji zaidi
Makao Makuu
 
Zile nyimbo na ngonjera za 'miundo mbinu chakavu' zimeshachuja na hazina mashiko tena katika zama hizi za Magufuli. Sina shaka Kigamboni ndio inayoongoza kwa ukatikaji wa umeme hovyo hovyo katika jiji la Dar, kwa wiki umeme unakatika mara tatu hadi nne kutegemea na siku hiyo wameamkaje; shida ni nini, mbona ni Kigamboni tu? Nani awajibishwe?
Kigamboni eneo gani na namba yako ya simu? Kigamboni ni miongoni mwa maeneo ambayo tumefanya kazi kubwa kuimarisha umeme na juma hili tumekuwa na katizo lililotokana na hitilafu ambapo wateja walijulishwa.tunaomba namba yako ya simu tukusikilize zaid
 
Kwa nini ukitaka kuvuta umeme nguzo zikizidi mbili mnaita mradi na mteja ukipigiwa Bei zaidi ya nguzo mbili Bei inakuwa kubwa Sana
Kila mteja anayefungiwa umeme anafungiwa kutokana na umbali aliopo na material yanayohitajika.
 
Kigamboni eneo gani na namba yako ya simu? Kigamboni ni miongoni mwa maeneo ambayo tumefanya kazi kubwa kuimarisha umeme na juma hili tumekuwa na katizo lililotokana na hitilafu ambapo wateja walijulishwa.tunaomba namba yako ya simu tukusikilize zaid
Kwahiyo unataka kusema ni juma hili tu ndio mmekuwa mkikatakata umeme hovyo? Nipo Kibugumo, umeme unakatika masaa mawili unarudi, unakatika masaa matatu unarudi, unakatika na kurudi bila utaratibu maalum, kama ni hitilafu irekebisheni mara moja, mbona ulaya hakuna haya mambo,rekebisheni hiyo hitilafu mara moja.
 
Tuleteeni umeme jamani,
Mbezi ya kimara huku, tumesimikiwa nguzo wiki ya 3 hakuna ujenzi wowote Wa waya wala ufungaji Wa mita.
Tumechoka kusubiri.
 
Tuleteeni umeme jamani,
Mbezi ya kimara huku, tumesimikiwa nguzo wiki ya 3 hakuna ujenzi wowote Wa waya wala ufungaji Wa mita.
Tumechoka kusubiri.
Ni kweli mpendwa mteja hatua ya kwanza ilikuwa kusimika nguzo kwa wateja wote wenye uhitaji wa nguzo kisha tunawaunganishia
 
Kwahiyo unataka kusema ni juma hili tu ndio mmekuwa mkikatakata umeme hovyo? Nipo Kibugumo, umeme unakatika masaa mawili unarudi, unakatika masaa matatu unarudi, unakatika na kurudi bila utaratibu maalum, kama ni hitilafu irekebisheni mara moja, mbona ulaya hakuna haya mambo,rekebisheni hiyo hitilafu mara moja.
Tunaomba namba yako ya simu
 
umeambiwa toa namba, msaidiwe
 
Ni kweli mpendwa mteja hatua ya kwanza ilikuwa kusimika nguzo kwa wateja wote wenye uhitaji wa nguzo kisha tunawaunganishia
mnategemea kuanza kutandaza wire na kuweka mita lini?? pia mbona siku hizi mnapenda kutumia meter za kutumia remote controller zile meter za kawaida hamzitaki tena???. maana hizi mita za kutumia remote kwa nyumba za mbalimbali ni changamoto umeme luku ikiisha kabisa
 
Back
Top Bottom