TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Wadau nimelipia umeme tar 11/9/2018 mpk tar 23/10/2018 nilitimiza siku 30 lakni nimefuatilia na simu nimepiga sana lakini hawajakuja kuniunganishia.
Naombeni ushauri jinsi ya kufanya kwa hawa TANESCO.
 
Eneo gani haswa na namba yako ya simu tukufikie
Napenda kujua hili:
Mwezi uliopita ulinunuliwa umeme wa Tshs 5,000, nikapewa units 41. Lakini sasa umenunuliwa umeme wa Tshs 5,900 umeme tumepewa units 38.4.
Je; sababu ni nini?
 
Wadau nimelipia umeme tar 11/9/2018 mpk tar 23/10/2018 nilitimiza siku 30 lakni nimefuatilia na simu nimepiga sana lakini hawajakuja kuniunganishia.
Naombeni ushauri jinsi ya kufanya kwa hawa TANESCO.
mimi nimelipia mwezi wa 8 bado sijawekewa umeme juzi tu nimeenda Tanesco mbezi nimeambiwa saiz wanashughirikia waliolipia mwezi wa saba. ndiyo hoja zao nilipoenda kuuliza mwanzo waliniambia wanadeal na waliolipia mwezi wa 4 - 6 saiz mwezi wa saba, ukienda utasikia tunadeal na waliolipia mwezi wa 6 labda wakukumbuke wakijisahau tu utapigwa sababu zilezile
 
Kwanini sio wa kweli kwasababu niliwahoji wakasema MITA na WAYA vipo zingi tu stoo.Sasa huu ni upuuzi wanaoleta kwanini walipokea pesa kwa haraka hivyo.
 
Tanesco kama kawaida yenu tunyoosheni sijui hii tabata tumewakosea nini au meneja wenu Ana mchepuko wake huku?
Kwanini mnatutesa hivi
 
Naomba kuuliza kama ref number ya kulipia service line imeexpire kuirenew inachukua muda gani?
 
Naomba kuuliza kama ref number ya kulipia service line imeexpire kuirenew inachukua muda gani?
 
Naomba kuuliza kama ref number ya kulipia service line imeexpire kuirenew inachukua muda gani?
Ndugu mpendwa mteja
Unapaswa kuwasiliana na ofisi ya eneo lako ili upatiwe nyingine
 
Tanesco kama kawaida yenu tunyoosheni sijui hii tabata tumewakosea nini au meneja wenu Ana mchepuko wake huku?
Kwanini mnatutesa hivi
Tabata eneo gani na namba yako ya simu tafadhali
 
Tanesco hivi watu wa ilemi darajani mtaa wa mwanfute mbeya mjini, wamewakosea nini kwanini kila umeme ukatikapo koote umeme huwa unawahi kurudi lakini siyo mtaa huu jamani,Leo inaenda Siku ya tatu ni Giza tuu kulikoni?
 
Mimi tatizo langu ni meter ya Luku, umeme unkata kwa masaa kila jioni kwangu tu au nyumba mbili lakini meter ziko tatu kwenye nguzo moja na huyo mmoja haujawahi katika. Kwa nini kwangu au kwetu tu. Kama umeme mdogo iwe nyumba mbili tu? Line hii kuna nyumba tatu za jirani umeme haukatiki. Ni Songwe hapa.
 
Walionitangulia ni wangapi!?. Ingekuwa vizuri msingetoa muda wa miezi miwili ya kusubiri baada ya kulipa kwa wale wenye nguzo mbili. Na hiyo mikataba yenu na wateja mbona mnaivunja!!!?? Au mnatumia mianya hiyo na kutoa visingizio na kutengeneza mazingira ya RUSHWA !!? Tafadhali TANESCO Makao Makuu nisaidieni (Kama kweli hakuna vifaa Tanesco Kigamboni pelekeni mtusaide)
Amakweli wenye sauti ni wenye pesa. Sisi tusio na uwezo hatusikilizwi. Yale majibu ambayo Mh. Raisi ameyakataa ya " Subiri na Njoo kesho" bado yana tawala TANESCO. Sijui nani atanisaidia. Tanesco Kigamboni kwangu imekua Kero. Tanesco Makao makuu naomba namba zenu jamani niwasiliane nanyi.
 
Naomba nibadilishiwe kwenda kwenye tarrif 4 manake matumizi yangu hayazidi units 40 kwa mwezi mita yangu hii 24219652385
 
Amakweli wenye sauti ni wenye pesa. Sisi tusio na uwezo hatusikilizwi. Yale majibu ambayo Mh. Raisi ameyakataa ya " Subiri na Njoo kesho" bado yana tawala TANESCO. Sijui nani atanisaidia. Tanesco Kigamboni kwangu imekua Kero. Tanesco Makao makuu naomba namba zenu jamani niwasiliane nanyi.
Hawa jamaa ni jipu
 
Tutakufungia umeme hauna haja ya kuwa na hofu wala kudhani tunahitaji chochote.hii ni haki yako na sisi ni wajibu wetu.upo kwenye orodha yetu
 
Kwalipi mpendwa mteja? Tumeendelea kusisitiza waliolipa wote watafungiwa umeme kwa kuzingatia wa kwanza kulipia wa kwanza kufungiwa hivyo tunaomba uvumilivu
Haya ni majibu kutoka kituo cha umeme Mbagala.

Mara ya kwanza;Walinijib kuwa mita na waya vipo na watakuja kufunga mwisho wa mwezi wa 10.

Mara ya pili;Walinijib kuwa watakuja mwanzoni mwa mwezi wa 11 amabao ndo huu na kuniomba nirud na kuendelea kuwasubiri.

Mara ya tatu;Baaada ya kumpigia Meneja wa umeme Pwani na Dar akaniomba nirudi tena kwnye hicho kituo ili nionane na meneja lkn kufika pale walinizuia kuonana nae na kudai hilo jambo liko ndani ya uwezo wao na kuniomba nisubir tena mwezi huu.

Sasa huo ndo utendaji kazi wenu ulivyo na kwann ukweli kwenu ni tatizo.
 
Back
Top Bottom