TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kuna sehemu kuna umeme wa kawaida na kuna maeneo kuna umeme wana sema ni wa sijui REA, ni nini tofauti kati ya Umeme wa TANESCO NA UMEME WA REA?
Je ENEO MOJA LINAWEZA KUWA NA UMEME WA TANESCO NA UMEME WA REA, kwa nini.
 
Hakuna tofauti yoyote ya umeme bali umeme wa REA ni mradi uliopo chini ya REA na wateja wanalipa 27000 tu kufungiwa umeme kipindi cha mradi kikiisha bei inakuwa ya kawaida tsh 177000 ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo ya umeme
 
Nashukuru kwa majibu mazuri.
Sasa kama ndivyo ilivyo, kwanini kna nguzo tofauti wakati msambaza umeme ni yule yule? mfano, utakuta kuna nyumba mbili tofauti zimepakana, moja wantumia umeme wa REa na mwingine anatumia hou mwingine?
 
Miradi ya REA inakuwa na umbali ulionyeshwa nje ya hapo inakuwa kawaida.tunaomba maelezo zaidi ya kwako ilikuwaje?na kiasi cha kulipa unaambiwa na ofisi husika wewe uliambiwa na nani
 
Miradi ya REA inakuwa na umbali ulionyeshwa nje ya hapo inakuwa kawaida.tunaomba maelezo zaidi ya kwako ilikuwaje?na kiasi cha kulipa unaambiwa na ofisi husika wewe uliambiwa na nani

Sorry, shida si malipo, maana sijadaiwa/sijaambiwa malipo tofauti na uliyo sema. Nilichokuwa naulizia ni kwamba unaweza kuta nguzo mbili maeneo jirani, Nguzo za REA maeneo ninayoishi zina bati fulani kwa juu. Sasa unakuta watu wa eneo hilohilo, mmoja kafungiwa umeme wa REA na wengine umeme wa kawaida.

Pia bei za unit zinatofautiana au?

NAashukuru
 
Mm ni mkazi Wa wilaya ya Mkuranga, kitongoji cha Mkokozi kwenye mradi Wa Umeme vijijini( REA) niliandika humu tatizo langu.

Mkaniomba namba za Simu nikawapa ! Nimesubiri mnipigie nimeona kimya, moja ya tatizo langu ni pale mliponipa namba za simu ambazo kila nikipiga naanza upya kujielezea na linakuwa na jibu hilohilo TUNASHUGHULIKIA.

sasa mliomba namba za Simu ndo mko kimya kabisaaa nilitegemea kupata ufumbuzi kumbe ndo mwanzo Wa mwisho.

Sasa msipate tabu ya kuniomba namba ya simu ni 0789443736.

Tatizo langu kwa kifupi "nimelipia mita 2, tarehe 25/7/2018 nimefungiwa mita 1, nimefuatilia na kuelezwa kulikuwa na makosa yatashughulikiwa hali ni kimya mpaka Leo.

Umeme huo ni kwaajili ya shughuli za kujiongezea kipato. Ucheleweshaji ni kuniongezea umaskini kwangu na jamaa zangu, majirani na Taifa. Dhana hapa kazi tu inakwamishwa.
 
Asante sana sana mkuu, nimeshahudumiwa na nimepigiwa simu nikachukue uniti 40 zangu. Big up sana Tanesco JF, sikutegemea kama nitahudumiwa haraka hivi, inatia moyo sana.
Karibu sana mpendwa mteja wetu
 
Mimi ni mteja niko Babati, nimefungiwa umeme siku kumi zilizopita nikapewa umeme uniti 10, umeme ukakaribia kwisha na nikaenda Tanesco nikaambia ninunue na kulipia uniti 50, ingawa hizo uniti 40 sikupewa. Nimelipia lakini ni zaidi ya wiki sasa hizo uniti 40 sijapata, na niliambiwa zikiwa tayari watanipigia simu ili nizifuate Tanesco na kusaini. Sasa sielewi uniti nimelipia halafu sipewi mpaka watakaponipigia simu!!? Hii huduma mbona inakera?
Mita no: 54182502994
Wilaya: Babati
Watakupigia simu watakupa hizo unit. Mimi mwnyewe nilipewa hizo 10 wakasema hizo 40 nitapewa ndani ya wiki ila umeme unaofuata baada ya hizo unit 10 kuisha inabidi nikanunue kwenye kituo chochote cha tanesco.
Baada ya wiki nikapiga simu, akanitajia token, nikaingiza na maisha yanaendelea. Hakukuwa na haja sijui ya kusaini hapana.
 
Salaam Tanesco, narudi kwa mara nyingine, niliwaeleza suala la REA kwenye kijiji cha Mabuye wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, niliwaeleza kuwa vitongoji vya KIJUKA na ITALA havijapata mhafaka juu ya kupatiwa umeme wa REA kwani inasemekana hamna ramani wala maelekezo yoyote juu ya vitongoji hivi hivyo vinaweza kurukwa bila kupata Huduma hii, mlihaidi kushughulikia na kuleta mrejesho lakini hadi sasa sijaona kitu. Nawakumbusha tena, sula hili limefikia wapi?
 
Asante sana sana mkuu, nimeshahudumiwa na nimepigiwa simu nikachukue uniti 40 zangu. Big up sana Tanesco JF, sikutegemea kama nitahudumiwa haraka hivi, inatia moyo sana.
TANESCO wanahitaji pongezi japo kuna watu wachache wanaojaribu kupoteza reputation yake
 
Salaam Tanesco, narudi kwa mara nyingine, niliwaeleza suala la REA kwenye kijiji cha Mabuye wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, niliwaeleza kuwa vitongoji vya KIJUKA na ITALA havijapata mhafaka juu ya kupatiwa umeme wa REA kwani inasemekana hamna ramani wala maelekezo yoyote juu ya vitongoji hivi hivyo vinaweza kurukwa bila kupata Huduma hii, mlihaidi kushughulikia na kuleta mrejesho lakini hadi sasa sijaona kitu. Nawakumbusha tena, sula hili limefikia wapi?
Mkuu tulikupatia mrejesho hapo awali kuwa tunaomba uvumilivu wakati swala lenu linafanyiwa kazi
 
Back
Top Bottom