TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mheshimiwa waziri wa nishati nakumbuka alidai kuwa bei ya kufungiwa umeme ni 27000,kwa sisi tulio vijijini na akadai kuwa ukishalipa hiyo nenda utulie usubiri kufungiwa umeme hbr za nguzo sio kazi ya mteja iweje tukienda ofcn twadaiwa kulipa hela ya nguzo?
 
Kuna tatizo la umeme maeneo ya karakata huku airport toka jana jioni umeme hauna nguvu unawaka na kuzima kwani hili hamjaliona?
 
REA wameweka line, nimefanya wiring na kuthibitishiwa na certified contractor kwenye form niliyoiwasilisha ofisi ya wilaya ya Ngara tangu March 2019, hadi sasa sijathibitishiwa kupatiwa umeme.. Kila siku wanafanya ukaguzi wa uthibitishaji wa lines.. Kwanini uunganishiwaji wa umeme unachukua muda mrefu kuliko ule mnaounadi kwenye vijarida na ofisini?
Mtaa: Munjebwe
Kata: Rulenge
Wilaya: Ngara
Mkoa: Kagera
 
Leo mwanza nzima no umeme [emoji23][emoji23][emoji23] kweli mnaangaza maisha
 
Nimelipia nguzo mbili tangu mwezi August mpaka leo sijaona nguzo wala umeme!
 
Kufanya hivi bila kutoa taarifa kuwa umempa nani au kumpa mtu ni kinyume na sheria tafadhali tufuate sheria na taratibu zilizopo
Mkitekeleza majukumu yenu ipasavyo, hakuna mwananchi atakayekuja Tanesco kulalamika, wala kutoa Rushwa.
 
Mheshimiwa waziri wa nishati nakumbuka alidai kuwa bei ya kufungiwa umeme ni 27000,kwa sisi tulio vijijini na akadai kuwa ukishalipa hiyo nenda utulie usubiri kufungiwa umeme hbr za nguzo sio kazi ya mteja iweje tukienda ofcn twadaiwa kulipa hela ya nguzo?
Mimi nilisikia Nguzo ni bure.
Ila hadi Leo ukienda ofisini unapigwa Dana Dana tu.
 
Kufanya hivi bila kutoa taarifa kuwa umempa nani au kumpa mtu ni kinyume na sheria tafadhali tufuate sheria na taratibu zilizopo
Nyie mko makao makuu nadhani hamjui adha ya umeme, wananchi wako hoi, wananchi wanahitaji sana umeme karibia kuliko kitu chochote, lakini kama mmgeamua Tanzania nzima mkaifunga umeme naamini mgekuwa mnavuna pesa za kutosha, ila umeme mmeufanya kwa ajili ya wateule wachache, hivi kwanini mtu kujivutia umeme kupeleka kijijini kwakwe mnamkadria mamilion ya pesa kisa umbali wa nguzo zitakazo tumika? Kwanini hizo gharama za umbali msizipunguze ili kila mwenye uhitaji akajivutia umeme bila kusubiria huo wa REA ambao umekuwa ukiongelewa kwenye makaratasi tu! NATAMANI NINGELIKUWA RAIS hili shirika la Tanesco NINGELIFUTA nikaruhusu mashirika binafsi yakasaidia kuwasambazia umeme watu vijijini. Nyie mmekuwa watu wa kushughulika mijini tu huku watanzania wengine huko vijijini wakiwa gizani kwani gharama ni ngumu. Rushwa na Tanesco ni km sehemu ya mikataba ya Tanesco, mnakera. Nyie mlioko huko makao makuu huenda ni waadilifu lakini huku chini ni uozo uozo uozo. Usifikiri watanzania wanapenda kutoa rushwa ila watanzania wanalazimika kutoa rushwa. Hivi uliwahi kusikia Mtanzania anatoa rushwa ili aweze kupata vocha ya kuingiza salio kwenye simu yake? Ni kwamba mitandao ya sim imetengeza mifumo kila anaye hitaji vocha ataipata kwa urahisi! Leo mnaweka mifumo migumu ya kupata umeme mnategemea watu wasitoe rushwa! Hivi vituko! Rais Magufuli naamini siku jicho lake likiwaangazia watanzania tutafurahi sana. Nafika hatua naona km vile hii Tanzania imekuwa ya baadhi ya watu huku wengine tuliko vijijini km vile tunasindikiza tu, hatuna maji, hatuna barabara, hatuna umeme, hatuna huduma za afya lakini tunafanya kazi ya kuwazalishia chakula mlioko mjini na mna kila huduma kibaya unajitutumua walau upate hata umeme ambao ungekurahisishia huduma nyingine km kujivutia maji, kilimo, ufugaji nk alafu unazungushwa kama mwenge wa uhuru.
 
Salaam mabibi na mabwana, Salaam Mh Kalemani, salaam Dada Subira Mgalu, Rea na Tanesco
Miaka nenda miaka rudi Tanesco mmejificha kwenye kivuli cha kuwa hamna nguzo ndiyo maana umeme wa REA na Tanesco hausambazwi vitongojini au vijijni km inavyotakuwa. Wateja wa Tanesco pia huambiwa na kucheleweshewa huduma ya kufungiwa umeme kwani mnadai hamna nguzo, si rahisi kusema hamna nyaya wala material nyingine bali mnasema hamna nguzo. Naomba kuelimishwa juu ya hili mana misitu yenye miti ni mingi sana hapa Tanzania lakini mnasema hamna nguzo. Mwanzoni niliamini kuna miti maalumu kwa kazi hiyo ndiyo maana mnasema hamna nguzo, nilistaajabu baada ya kuona nguzo ni miongoni mwa miti ya Karatusi ambayo imetapakaa kila kona ya nchi hii kuliko karibia mti wowote hapa Tanzania. Je, inakuwaje mnaseama hamna nguzo? Je,hizo nguzo mnazosema ninyi zina sifa zipi ambazo huwa vigumu kuzipata kwa wakati?
Ningeomba shirikia hili lije na majibu juu ya kero hii, serikali ilikuja na jambo jema sana la umeme wa REA lakini mpaka sekunde hii kati ya takribani vijiji 12,380 vya nchi hii vingi havina umeme japo inakadriwa ni karibia vijiji elfu 8 vina umeme tayari lakini huu ni umeme wa kwenye makaratasi! Na hii ningetamani Mawaziri, Makatibu na Viongozi wengine wajue hadi ikiwezekana na Mh Rais ajue kuwa umeme unasimikwa tu kwenye maeneo ya shule,zahanati nk sehemu muhimu kwenye kijiji lakini maeneo mengi yanabaki bila umeme. Unakuta kwenye kijiji ni kama 2% tu wanaopata umeme ila 98% wanabaki bila umeme. Ni vijiji vichache sana ambavyo hupata umeme kwa 100% na ukiona hivyo jua kuna msukumo flani nyuma yake. Ningeomba sote kwa pamoja tutafakari haya
1) Kwanini ukosefu wa nguzo umekuwa ni kigezo kikuu cha kusababisha watu wasipewe huduma hii muhimu?
2) Je, ni miti aina gani hutakiwa kwa ajili ya kupata hizo nguzo?
3) Hapa Tanzania hakuna uwezekano wa kupata nguzo hizo kwa urahisi?
4) Wakandarasi huelekezwa kusambaza umeme kwenye maeneo muhimu tu?
5) Kama nguzo za miti imekuwa changamoto hatuwezi kupata mbadala wa nguzo?
6)Kwanini kila mtanzania anayehitaji umeme asifungiwe umeme hata kwa mkopo alafu mkawa na mkataba wa jinsi ya kulipia taratibu?
7)Mbona huwa hatuambiwi hakuna nyaya, au materials nyingine tofauti na nguzo?
8) Mnajua umeme ulivyo nguzo muhimu sana katika kuinua maisha ya kila Mtanzania kuliko karibia kitu chochote?
9)Kama Tanesco inaelemewa kwanini wasitafute wasaidizi wengine?
Mh Kalemani na Mh Mgalu hii kazi ni ngumu kweli lakini jaribuni walau kuwa wazi kwa raia kuliko kuwa mnawapa matumaini hewa juu ya kila raia kupata huduma ya REA.
 
Hii nguzo inadondoka muda wowote ipo huku mivumoni,tumeripoti tanesco hawaji kubadilisha
IMG_20191022_084215_3.jpeg
 
Tanesco kwanini hamjibu suala la upatikanaji wa mita za three phases? Tumelipia muda mrefu, tatizo nini? Serikali inahimiza nchi ya viwanda Tanesco mita za umeme hazipo!!!
 
Umelipa tarehe ngapi na namba yako ya mita tafadhali, upo wilaya gani
 
Salaam mabibi na mabwana, Salaam Mh Kalemani, salaam Dada Subira Mgalu, Rea na Tanesco
Miaka nenda miaka rudi Tanesco mmejificha kwenye kivuli cha kuwa hamna nguzo ndiyo maana umeme wa REA na Tanesco hausambazwi vitongojini au vijijni km inavyotakuwa. Wateja wa Tanesco pia huambiwa na kucheleweshewa huduma ya kufungiwa umeme kwani mnadai hamna nguzo, si rahisi kusema hamna nyaya wala material nyingine bali mnasema hamna nguzo. Naomba kuelimishwa juu ya hili mana misitu yenye miti ni mingi sana hapa Tanzania lakini mnasema hamna nguzo. Mwanzoni niliamini kuna miti maalumu kwa kazi hiyo ndiyo maana mnasema hamna nguzo, nilistaajabu baada ya kuona nguzo ni miongoni mwa miti ya Karatusi ambayo imetapakaa kila kona ya nchi hii kuliko karibia mti wowote hapa Tanzania. Je, inakuwaje mnaseama hamna nguzo? Je,hizo nguzo mnazosema ninyi zina sifa zipi ambazo huwa vigumu kuzipata kwa wakati?
Ningeomba shirikia hili lije na majibu juu ya kero hii, serikali ilikuja na jambo jema sana la umeme wa REA lakini mpaka sekunde hii kati ya takribani vijiji 12,380 vya nchi hii vingi havina umeme japo inakadriwa ni karibia vijiji elfu 8 vina umeme tayari lakini huu ni umeme wa kwenye makaratasi! Na hii ningetamani Mawaziri, Makatibu na Viongozi wengine wajue hadi ikiwezekana na Mh Rais ajue kuwa umeme unasimikwa tu kwenye maeneo ya shule,zahanati nk sehemu muhimu kwenye kijiji lakini maeneo mengi yanabaki bila umeme. Unakuta kwenye kijiji ni kama 2% tu wanaopata umeme ila 98% wanabaki bila umeme. Ni vijiji vichache sana ambavyo hupata umeme kwa 100% na ukiona hivyo jua kuna msukumo flani nyuma yake. Ningeomba sote kwa pamoja tutafakari haya
1) Kwanini ukosefu wa nguzo umekuwa ni kigezo kikuu cha kusababisha watu wasipewe huduma hii muhimu?
2) Je, ni miti aina gani hutakiwa kwa ajili ya kupata hizo nguzo?
3) Hapa Tanzania hakuna uwezekano wa kupata nguzo hizo kwa urahisi?
4) Wakandarasi huelekezwa kusambaza umeme kwenye maeneo muhimu tu?
5) Kama nguzo za miti imekuwa changamoto hatuwezi kupata mbadala wa nguzo?
6)Kwanini kila mtanzania anayehitaji umeme asifungiwe umeme hata kwa mkopo alafu mkawa na mkataba wa jinsi ya kulipia taratibu?
7)Mbona huwa hatuambiwi hakuna nyaya, au materials nyingine tofauti na nguzo?
8) Mnajua umeme ulivyo nguzo muhimu sana katika kuinua maisha ya kila Mtanzania kuliko karibia kitu chochote?
9)Kama Tanesco inaelemewa kwanini wasitafute wasaidizi wengine?
Mh Kalemani na Mh Mgalu hii kazi ni ngumu kweli lakini jaribuni walau kuwa wazi kwa raia kuliko kuwa mnawapa matumaini hewa juu ya kila raia kupata huduma ya REA.
Ndugu mpendqa mteja wetu unaongelea eneo gani? Wilaya na namba yako ya simu tukujibu kwa kuzingatia kinachoendelea eneo husika
 
Nyie mko makao makuu nadhani hamjui adha ya umeme, wananchi wako hoi, wananchi wanahitaji sana umeme karibia kuliko kitu chochote, lakini kama mmgeamua Tanzania nzima mkaifunga umeme naamini mgekuwa mnavuna pesa za kutosha, ila umeme mmeufanya kwa ajili ya wateule wachache, hivi kwanini mtu kujivutia umeme kupeleka kijijini kwakwe mnamkadria mamilion ya pesa kisa umbali wa nguzo zitakazo tumika? Kwanini hizo gharama za umbali msizipunguze ili kila mwenye uhitaji akajivutia umeme bila kusubiria huo wa REA ambao umekuwa ukiongelewa kwenye makaratasi tu! NATAMANI NINGELIKUWA RAIS hili shirika la Tanesco NINGELIFUTA nikaruhusu mashirika binafsi yakasaidia kuwasambazia umeme watu vijijini. Nyie mmekuwa watu wa kushughulika mijini tu huku watanzania wengine huko vijijini wakiwa gizani kwani gharama ni ngumu. Rushwa na Tanesco ni km sehemu ya mikataba ya Tanesco, mnakera. Nyie mlioko huko makao makuu huenda ni waadilifu lakini huku chini ni uozo uozo uozo. Usifikiri watanzania wanapenda kutoa rushwa ila watanzania wanalazimika kutoa rushwa. Hivi uliwahi kusikia Mtanzania anatoa rushwa ili aweze kupata vocha ya kuingiza salio kwenye simu yake? Ni kwamba mitandao ya sim imetengeza mifumo kila anaye hitaji vocha ataipata kwa urahisi! Leo mnaweka mifumo migumu ya kupata umeme mnategemea watu wasitoe rushwa! Hivi vituko! Rais Magufuli naamini siku jicho lake likiwaangazia watanzania tutafurahi sana. Nafika hatua naona km vile hii Tanzania imekuwa ya baadhi ya watu huku wengine tuliko vijijini km vile tunasindikiza tu, hatuna maji, hatuna barabara, hatuna umeme, hatuna huduma za afya lakini tunafanya kazi ya kuwazalishia chakula mlioko mjini na mna kila huduma kibaya unajitutumua walau upate hata umeme ambao ungekurahisishia huduma nyingine km kujivutia maji, kilimo, ufugaji nk alafu unazungushwa kama mwenge wa uhuru.
Tunaomba kukusikiliza upo eneo gani? Wilaya gani na namba yako ya simu tafadhali.hii itatusaidia kukupatia mrejesho kamili
 
REA wameweka line, nimefanya wiring na kuthibitishiwa na certified contractor kwenye form niliyoiwasilisha ofisi ya wilaya ya Ngara tangu March 2019, hadi sasa sijathibitishiwa kupatiwa umeme.. Kila siku wanafanya ukaguzi wa uthibitishaji wa lines.. Kwanini uunganishiwaji wa umeme unachukua muda mrefu kuliko ule mnaounadi kwenye vijarida na ofisini?
Mtaa: Munjebwe
Kata: Rulenge
Wilaya: Ngara
Mkoa: Kagera
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali
 
Tanesco nililipia nguzo mblili toka january hadi leo sijapata huduma dasa yapata week ya tatu wameleta nguzo wameacha hapo na hawajasema chochita
Nipo moshi kituo cha huduma ni Himo
Jina: casian kundy wa kirua vunjo moshi
Msaada tafadhali
Mbona sijapata jibu hapa au tanesco wanachagua hoja?
 
Ndugu mpendqa mteja wetu unaongelea eneo gani? Wilaya na namba yako ya simu tukujibu kwa kuzingatia kinachoendelea eneo husika
Ndugu Tanesco, kuna maswali hapo juu ungetusaidia kutuongezea maarifa kwa kutuelewesha hapa hapa jukwaami maana hili tatizo la nguzo na gharama vimekuwa donda sugu kwa wengi. Namba nakutumia inbox.
 
Habari za muda huu, Nyumbani kwangu kuna tatizo la umeme ambalo linasababishwa na loose juu ya nguzo ikifikia kipindi km hichi cha mvua huwa napata tabu sana ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, mara ya kwanza nilitoa taarifa halikufanyiwa kazi sasa hivi nna siku ya tatu hakuna umeme unapofika katika mita yng, nilipiga simu emergency usiku kucha simu haipokelewi yaani hadi hapo sijaona umuhimu wa emergency calls ila sasa hali imezidi kuwa mbaya mita inarudisha umeme halafu inakata ht mara 10 siku nzima sasa sijui tanesco mnataka nitumie njia ipi sahihi ili niweze kupata huduma na kunusuru hali hii ya umeme kwangu taarifa nimetoa tangu jana baada ya kuona simu hazipokelewi nimeambatanisha na namba waliyonipa ofisini namba zangu za simu ni 0714434257 naishi kigogo mkwajuni
1571934162776.jpeg
 
Back
Top Bottom